Msaada: Mke wangu mvivu kupindukia!

Msaada: Mke wangu mvivu kupindukia!

Seriously..yalinikuta haya (uliyohadithia yamefanana sana). Unfortunately kwangu yaliongezeka na mengine nikashindwa vumilia nikabwaga manyanga. Surprisingly, now ameajiriwa anafanya kazi na anachakarika na biashara kuongeza kipato. Lakini maji ndio yameshamwagika tena. pole sana..I know how frustrating can this be.

Duhq kumbe kuachwa somtym ni dawa!?
Though cfurahii kuachana!!
Ss km anchakarika,c umrudie Riwa jamani,atakuwa kajifunza
 

hahahaaaa!!kashika pabaya aisee
mama mkwe ndio rafiki yake,kazi ipo
labda umweleze mama jinsi unavyokereka
kwa kua ni mtu wake wa karibu na ni mzazi
ajaribu kuongea nae,dunia ya leo sio ya
mwanamke kubweteka,ukitoweka ghafla
ataishije na watoto,kweli kwny miti hapana wajenzi!!


inawezekana hapo ndiyo anafuata ushauri wa mama mkwe...........

huyo mke wake atakuwa anafaa sana............
 
Id yako inasadifu vya kutosha ulio yaandika... Sizani kama mwanaume mwenye misimamo thabiti na uzoefu na mkewe kwa muda wote uo, anaweza kuja lalamika juu ya jambo dogo kama hilo... Msimamo wa mwanaume na hamu ya kufanya maamuzi magumu ni funzo tosha kwa mwanamke yeyote yule hapa duniani.

Wasukuma wanamsemo kuwa! "Umbanza atatindagwa" manake ni kwamba Mwanaume ambaye hajaoa he is always a winner! Utasikia Mimi!!!! Mwanamke!!!!!!!! Akifanya hivi na hivi na mafanya kitu mbaya!!
 
Duhq kumbe kuachwa somtym ni dawa!?
Though cfurahii kuachana!!
Ss km anchakarika,c umrudie Riwa jamani,atakuwa kajifunza

Dada @christine ibrahim..nimesema na mengine yaliongezeka nikabwaga manyanga. Hayo mengine yaliyoongezeka ndio kikwazo!
 
pole saaana,huyo mwanamke kwa kweli akili F,na degree yake,anatafutiwa kazi anachoka,masters hataki kisa hawezi kuamka mapema,huyo mwanamke ni aibu kwetu sie wanawake ambao tunafanya kazi/tunataka kufanya kazi na kujiendeleza badala ya kuwa dependant..naona watu wengne wanakusema kwamba we mwanaume na blah blah nyiiingi,ila hata kama ukimsetia maisha vizuri alafu ikafika mda wa kwenda kwa Muumba jua huku chini hiyo hela itapotea bila la maana kufanyika...ongea na wazee wamueleweshe,waoneshe na waambie wazee umuhimu wa yeye kujishughulisha sana sana pale wewe utakapo endelea mbele,waambie manung'uniko yako,unaweza kuta hajua hata mna magari makubwa mangapi...saddening...sasa wewe jenga msingi kwa watoto wako (kike/kiume),waoneshe umuhimu wa kusoma na kufanya kazi,maadali ya maisha
 
Pole sana bro hali hiyo ni serious sana kwani leo upo kesho jee itakuaje??
Inaelekea umejitahidi sana ila mama yako anachangia katika upuuzi huu.
Mimi ninadhani kutibu ugonjwa huu inabidi uwe na roho ngumu sana cha kwanza cha kufanya mwambie mama yako unachotaka kufanya na kumuomba asiingilie kwenye hili. Anza kwa kupunguza budget ya nyumbani by 15% [mwambie biashara haiendi vizuri] kama pesa zikiisha kabla ya wakati kula jiwe na kama mambo yanakuwa magumu peleka watoto boarding. baada ya muda punguza tena by 10% na ikifika hapa mwambie itabidi naye afanye kazi na ikibidi mwajiri wewe mwenyewe na umtreat kama employee aone uchungu wa kutafuta hela na ubaya wa matumizi ya hovyo kama unaona anabadilika kaa naye umuulize anataka kufanya kitu gani cha kuingiza hela na umueleze kuwa this time akishindwa basi budget ya nyumbani itabidi iendelee kubana.


Gooood! Huu ushauri mzuri pia.
Nakubaliana na ww
 
Ushauri wangu ni ivi
hsegal arudi kwao ndo mama aanze na kazi za hme Ata huo mshahara usimpe tena gari chukua atumie daladala aone jinsi gani anapoteza opportunity! Ivi hajui wengine wanatamani hiyo nafasi yeye anaichezea!
 
Habari zenu ndugu zangu, ahsanteni sana kwa ushauri wenu mzuri. Nimesoma kwa kina ingawa kuna baadhi ya vitu utekelezaji wake kidogo unaweza kuwa mgumu ila ntajitahidi. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kila aliyenipa ushauri kwenye hili. Ntajitahidi kujibu hoja za wote ingawa nyingine huenda zikajirudiarudia.
 
Hili wazo gumu na kiufupi haliwezekani. Ingawa ukoo wetu umeshika dini, haijawahi tokea ndugu yangu yeyote akaoa zaidi ya mke mmoja. Ntaonekana wa ajabu sana na huenda nkatengwa na kupigwa vita ile mbaya. Wako walio wahi kuoa wakaacha na kuoa tena lakini si kuoa mke zaidi ya mmoja. Hii ni hatua ya mwisho kabisa baada ya yote kushindikana na sidhani kama ntafikia huko.

mtafutie mke mwenzake!
 
Kakushika pazuri kweli, yan mama yako ndo rafiki yake mkubwa!! Huyo dada nampa salute

Unajua mama yangu ni mtu mzima na hana mawazo kama yangu. Akili ya mama ni kuwa mwanamke nafasi yake ni nyumbani na kulea watoto na mimi simlaumu kwani hiki ndicho kilikuwa kizazi chake ila hajui kuwa maisha siku hizi yamebadilika.

Wengi mmeshauri nisimpe pesa mwisho wa mwezi. Tatizo wazazi wangu mimi bado wanajiweza kiuchumi hivyo nikionyesha msimamo wangu nisimpe walishawahi kutishia kuwa wao watampa kila mwisho wa mwezi. Matokeo lengo langu halitotimia na sana sana ntajenga tu uhasama baina yangu mimi na wao. Siku hizi kuna njia nyingi za kumpa mtu pesa ni vigumu kuzuia pesa zisimfikie. Hivyo hili nalo halitowezekana.
 
duh!!!!! very sory,yani sina hata la kusema kwan kutokana na elimu yake naamini anajua changamoto zadunia ila amejitoa ufahamu tu,jaribu kumpa ukweli na mweleze anavyo kukera.
 
Mkuu mshukuru Mungu huyo mke wako anakutunzia watoto wako na wewe anakutimizia mahitaji kama mke. Huko maofisini unakotana kumleta mke wako si kuzuri, kuna mambo mengi tunayaona na kuwafanyia wake za watu yasiyostahili. Kama hana munkari wa kazi au biashara au shule haina maana ni mke kilaza. Tafuta kitu atakachofanya kitakachokuwa na interest kwake. Lakini usimhukumu after 7 years, lazima kuna mazuri uliyaona kwake. Wewe ndio baba na kidume kwenye familia, kutunza familia ni jukumu na wajibu wako. La msingi waandalie mazingira mazuri wanao endapo Muumba ataamua kukuita mbele ya haki wangali wadogo. Tusifananishe wake zetu na wake wa marafiki zetu kwani hujui wao wanaumiza vichwa kwa lipi.


Kujibu tu swali lako,

Watoto anawapenda sana na ndio roho yake. Kuhusu majukumu yake kama mke kusema ukweli nisipate dhambi hana tatizo kwenye hilo na huenda labda ndio maana nimemvumilia miaka yote hii.
 
Amekaliwa na mashetani, Peleka kanisani akaombewe, ni kwenye kanisa linalohubiri wokovu sio kanisa ilimradi kanisa

Asante kwa ushuri ila imani yangu iko tofauti na wala siamni hili hata chembe na sitokaa nije niamini hicho unachokisema.
 
unapata shida bure coz mkeo anaelimu japo ya degree kinachotokea nianaona kwanini nijisumbue wakati mume wangu mpenzi yupo ila ukiondoka leo au hali yako ya kiuchumi ikisumbua tu jua akili itakaasawa wala wanao hawatashindwa kuishi.labda kama alilelewa kwenye mazingira ya mambosafi kama hapo ila naamini. hawezishindwa kufight anapolazimika
 
muulize yeye anataka nini katika maisha, nini anataka achive, mmpe black and white na mustakabali mzima wa maisha mtishie kuwa wewe unasafiri na magari ikatokea siku ukapata ajari? atufyekwa! may God forbid! yeye ataisheje? mpe challenge hadi atie akili then atafika point atasema kweli lakini!

Nshakaa naye sana nshahubiri weeee mpaka nimechoka. Hobby aliyonayo ni kuangalia Bongo Movie na tamthilia za kizungu. Anaweza akaangalia movie 3 za kibongo kwa siku bila tabu. Nkimuuliza yeye anachotaka utasikia ntakujibu. Ukimng'ang'aniza sana ndio mara nipeleke nikasome masters alafu naishia kutupa tu hela. Ukimlazimisha biashara nayo anaharibu. Nikikaa nisubiri aje kuniambia anachokipenda yeye ntasubiri miaka 100.
 
kumbe kuna kulipana mishahara ndani ya ndoa aiseee!!!

Unajua toka mimi mdogo hadi leo, baba alikuwa akifanya hivi kwa mama. Na mimi nimekuwa nikijua kuwa hivi ndio maisha yalivyo. Ni kama kautamaduni flani nilikokazoea kukaona nikashauriwa nikaendeleze na wazee.
 
Hebu mdadisi aliwezaje kumfanya mama yako mzazi awe rafiki yake mkuu halafu uje utupe feedback?

Biashara yangu na ya baba ni sawa hivyo mama ndio aliyeamua kumuweka karibu na kumfundisha jinsi ya kukabiliana na matatizo yatokanayo na kazi zetu. Mfano naweza nikarudi nyumbani nimenyong'onyea labda gari limeanguka, sometimes madereva nliyowazoea huenda wakafa na ajali au matatizo meeengi. Mtu unarudi nyumbani umenyong'onyea au una hasira sana. Mshauri wake mkubwa wa kulea familia (Ndoa) yangu alikuwa ni mama na hivyo ndivyo walivyozoeana.

Back to the topic. Hivi wewe ndugu ni nini hasa kilichokufanya ukaamua kuoa? Ni sura, elimu, mautamu ya ngono zembe za kabla ya ndoa, au matarajio ya kazi ya mke?

Tabia ndugu wakati ule alikuwa anasifika kwa ndugu na jamaa kwa tabia yake ya utulivu, heshima na kutokua na mambo ya kishenzi.
 

Ingawa huyo shemeji yetu anasemekana kuwa ni mvivu, nashawishika kuandika kwamba anayo mazuri pia hasa katika management ya familia. Hakuna kazi ngumu na muhimu kama kutunza familia kamanda.

Jukumu la msing la mke/mama ni kutunza familia, kama ataweza kulifanya hilo kwa ufanisi mkubwa zaidi kuliko sasa ni bora zaidi.

Masuala ya economics za familia ni yako kaka. Acha mawazo ya hovyo ya eti nikifa kesho...what if akifa yeye...utaweza kufanya kazi anayofanya leo ya kutunza familia?? au unajua kutafuta fedha tu na kuacha mezani...acha hizo...unaweza kuta hata tarehe ya kuzaliwa first borne wenu umeisahau...!!! na yeye aje huku kulalamika????

TAFAKARI

Mkuu umenifumbua macho umenifanya Nifikirie tofauti lakini mimi binafsi nataka japo ajaribu ikionekana majukumu ya kulea familia yanamshinda kwa sababu ana kazi ataacha. Huenda anaweza mudu vyote tu. Just because analea familia haimaanishi kuwa asichakarike. Mwisho wa siku hakuna kitu muhimu kwangu kama Familia yangu na yeye akiwemo ndani ya hiyo familia.
 
Back
Top Bottom