Mkuu mshukuru Mungu huyo mke wako anakutunzia watoto wako na wewe anakutimizia mahitaji kama mke. Huko maofisini unakotana kumleta mke wako si kuzuri, kuna mambo mengi tunayaona na kuwafanyia wake za watu yasiyostahili. Kama hana munkari wa kazi au biashara au shule haina maana ni mke kilaza. Tafuta kitu atakachofanya kitakachokuwa na interest kwake. Lakini usimhukumu after 7 years, lazima kuna mazuri uliyaona kwake. Wewe ndio baba na kidume kwenye familia, kutunza familia ni jukumu na wajibu wako. La msingi waandalie mazingira mazuri wanao endapo Muumba ataamua kukuita mbele ya haki wangali wadogo. Tusifananishe wake zetu na wake wa marafiki zetu kwani hujui wao wanaumiza vichwa kwa lipi.