Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
1,146
2,000
Habari wakuu mke wangu ana dada yake ambaye kazalishwa mtoto mmoja na Dada yake hayuko katika ndoa, hajaolewa na aliyemzalisha alikuja akaoa mwanamke mwingine

Sasa basi mimi na mke wangu tuna mtoto mdogo wa umri sawa na mtoto wa Dada yake.. mke wangu amekuwa akimchukua mtoto wa Dada yake kila Ijumaa na kumrudisha Jumapili kwa Dada yake

Sasa akiwa anataka kumrudisha mtoto hataki kurudi kwa mama yake anataka kuendelea kuishi nasi wakati huo baba wa mtoto hana muda na mtoto wake kwa mahitaji ya mtoto yaani hamuhudumii.

Mama wa mtoto hataki hata siku moja kumpelekea mtoto kwa baba yake sababu ana mke mwingine atamtesa, Sasa amekuwa akimsukumia kwangu kwa kigezo cha kuja kucheza na mwenzake

Je, ni sawa baba wa mtoto yupo na mama wa mtoto kukataa mtoto kwenda kwa baba kutembea kwa kisingizio Cha mama wa kambo atamtesa hivyo kuona ni sahihi aende kwa mama yake mdogo hali ya kuwa baba yupo na anajichana na maisha?
 
Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
18,389
2,000
Si ajabu hata huyo mtoto wako utasema kwanini anashinda hapo kwenu kila siku.

Watoto ni baraka, ukipata nafasi ya kulea mtoto tangu angali malaika (miaka 2 hadi 10) shukuru Mungu maana ni baraka. Ila kuanzia miaka 10+ wanakuwa na tabia tayari inakuwa ngumu kuishi nae unavyotaka wewe.

Kila la kheri.
 
Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,699
2,000
Una element za uchoyo. Kama unaweza kumsaidia msaidie tu unless uwe huna uwezo au mtoto ana tabia ya kishenzi na huko kulia kwake ni watoto ndivyo walivyo.

Au mwisho wa yote mkataze asije kabisa kama humuhitaji kwako kuliko kuishi nae huku unachukia
 
Mkuu lengo siko uko mtoto kashaanza kubeba tabia za kike sababu ya muda mwingi yupo na wakike na mama harekebishi kwake ni sawa
 
malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
1,146
2,000
Una element za uchoyo. Kama unaweza kumsaidia msaidie tu unless uwe huna uwezo au mtoto ana tabia ya kishenzi na huko kulia kwake ni watoto ndivyo walivyo.

Au mwisho wa yote mkataze asije kabisa kama humuhitaji kwako kuliko kuishi nae huku unachukia
Mkuu tatizo sio kuishi tatizo ni kuwa mtoto kashaanza kuadapt tabia za kike na mama tu haoni shida kwake
 
malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
1,146
2,000
Una element za uchoyo. Kama unaweza kumsaidia msaidie tu unless uwe huna uwezo au mtoto ana tabia ya kishenzi na huko kulia kwake ni watoto ndivyo walivyo.

Au mwisho wa yote mkataze asije kabisa kama humuhitaji kwako kuliko kuishi nae huku unachukia
Mkuu Hana tabia za kishenzi Ila tatizo ni kuwa mtoto kashaadapti michezo ya kike maana hata umletee vitu vya mchezo wa kiume havitumii muda wote unakuta anacheza michezo ya kike na mwezie Sasa kwangu naona ni tatizo Hilo maana mama mtu Hana habari kwake nisawa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom