Msaada mita ya TANESCO

Olsea

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
452
250
Habari wadau wa jukwaa la Tech,juzi ilinyesha mvua kubwa na radi iliyopelekea umeme kukatika.Cha ajabu umeme ulivyorudi kwangu uligoma kabisa ikabidi kuwaita TANESCO kuangalia wakadai mita imeharibika mpaka kubadilisha kuwauliza watakuja lini kubadili sio chini ya siku 10..hapa nawaza namna ya kuishi siku zote hizo bila umeme na nipo likizo nyumbani,hakuna alyewah kutana na changamoto hii na je aliitatuaje?
 
Hahaha... mkuu..
Sisi tulikaa giza more than a month hadi tukazoea kabisa.
This is what happens, watakuja watasema hyo mita n mbovu .
Then atakuja mwingine ambae atadema a different problem.
Atakuja wa tatu ambae attakuja kukagua kama panfaa kuwekwa mita n.k.
Yaan n mizunguko kibao ndugu yangu.
Cha kukishauri, we piga simu ili waje kila siku. Ukiamka asubuh piga sim una tatizo, watakuja watarudi. Wakichoka unafungiwa mita. Leo asubuh nenda ofisini waambie unafanya biashara ya samaki na wanaoza kwenye fridge kwaio wanakutia hasara.
Asipokuelewa mwambie nataka kuongea na meneja (ni haki yako).
Mkubwa akisema, wanakuja wanakimbia
 
Mkuu jana wamekuja wakaangalia wamesema ni mita imekufa..unanishauri nn cha kufanya hapo?
 
Mkubwa akisema, wanakuja wanakimbia

Hili la kumface Meneja niliwahi kulitumia kwenye taasisi fulani baada ya watumishi kuzingua.

Yule officer alipozingua nikwambia Meneja yuko wapi nikamieleze tatizo langu, akanionesha. Nikaenda kumueleza akanielewa then akampa go ahead yule officer aliyekataa. Nikapata huduma
 
Piga tena simu leo. Waje tena mara ya pili. Na hapo yjiandae kisaikolojia, hakuna watakachofabya hadi j4 after sikukuu.
njia ya mwisho, (kama tanesqo wanasoma huu uzi na huko juu umetaja ulipo then umeumia.). Piga simm waje, wakifika, nyoosha maelezo kwa huyo fundi mwambie wazi vitu vinaoza ndani, mpe elf 10, anakuungua direct nje yamita. Hapo utatumia bure hadi walete mita yako. Hakuna wa kukuletea mayowe maana taarifa tayari iko kwenye system yao, akileta mdomo unamwambia hujui jina la fundi aliekuungia lakn alikusaidia maana samaki zinaoza ndani na wao hawaleti mita mpya
 
Duh pole hiyo kitu ilinitokea kama miezi miwili hivi mita Yao iligoma tu kwa makusudi kuingiza token. Nilikuwa napiga simu sijui inapokelewa Dodoma kwanza halafu wao ndio wanawaambia watu wa huku nipo aisee nadhani nilipiga simu zaidi ya mara 50 ndani ya wiki mbili nilizokaa giza. Kwanza walikuja emergency wakasema ishu mita hivyo wanapeleka taarifa kitengo cha mita hapo ndio mziki sasa wale jamaa wanakupigia simu kabisa tunakuja halafu hawaji ukipiga simu unaambiwa tupe namba ya taarifa baadae unaambiwa taarifa yako haionekani ngoja tufungue taarifa upya hapo umeshakaa wiki mara utatumiwa ujumbe tatizo lako limeshughulikiwa huku hata fundi hajafika mwisho wa siku niliamua kwenda ofisi Yao kuu ya kanda nikamuona boss wao nikamwambia waje wang'oe mita Yao kabisa nitafanya application upya na nilikuwa na hasira maana wale jamaa wa emergency walipokuja walinisimanga sana mara njia yenu mabovu mnatia hasara kwa serikali kuja huku mara unanunua umeme mdogo unatakiwa kuweka umeme wa kuanzia 50K .baada ya kumuona boss wao hapo hapo alipiga simu kwenye ofisi yao inayohudumia sehemu nilipoona ndani ya saa moja mafundi mita walinipigia simu wapo jirani na kwangu nikawaelekeza yaani ni kitu cha dakika 10 wameshabadirisha mita umeme unawaka na wakasema mita ilikuwa imechoka
 
Huku nimeambiwa hadi taarifa itumwe ndyo mita mpya isajiriwe halafu iletwe ikifika ndyo watakuja kufunga..sasa hapa nawaza huo mlolongo naona kabisa sio issue ya leo wala kesho.
 
Back
Top Bottom