Kwenu wataalam wa magari naomba msaada wa kubaini chanzo cha miguu ya mbele ya probox kutoa mvumo mkubwa kiasi ikifika speed 80 km/h hata redio huwezi kusikiliza.
Tatizo lilianza mwaka mmoja uliopita tukashauriwa kubadili bearings tulifanya hivyo haikusaidia, kisha tukanunua used nacoz complete tukafunga ikatulia kidogo. Ila mwezi uliopita tumebadilisha shock-up tatizo limerudi!!!
Naomba msaada wenu wajuzi nini tatizo na utatuzi wake ni nini?
Asante