Acha papara mdogo wako yuko darasa la sita na aendelee na darasa la sita,aliyekwambia jina ni mali ya mdogo wako ni nani? Majina hufanana,mdogo wako atafanya mtihani mwakani period.Wakuu habari zenu? Mmeshindaje?
Sasa Wakuu kuna shida kidogo nahitaji ushauri wenu kuna mdogo wangu alikuwa anasoma Arusha shule ya msingi sasa kule kulitokea shida kidogo akaamishwa shule akaletwa Ukerewe.
Wakati anaamishwa alkuwa darasa la sita lakini shuleni alipohamia Mwalimu Mkuu akakataa kumpokea mpaka arudishwe darasa la tano, basi ikawa hivyo dogo akarudi darasa la tano.
Sasa maajabu yameibuka leo baada ya matokeo kutoka dogo bado yupo darasa la sita mwakani anamaliza darasa la saba lakini jina lake limetoka kwenye matokeo kwamba amefaulu kwa daraja B.
Baada ya hapo nikafanya kuulizia marafiki wakadai Mwalimu Mkuu aliuza jina kwa mrudiaji. Sasa nahofia hatima ya mdogo wangu mwakani atakapofika darasa la saba itakuwaje?.
Kwa wanasheria ebu mnishauri nifanye nini kwa mjibu wa sheria, maana kinachoniuma ni mtu mwingine kumiliki jina la ukoo wetu.
Wanasheria na wakuu naomba kuwasilisha
Acha kumpotosha.Mnunulie vifaa vya shule aende kuriport halafu ndo kitaumana kuanzua hapo
Achana na hizo fikra muache mtoto aendelee na darasa la sita.Hilo jina la Arusha achana nalo.hapana mdogo wangu hakuwa mtoro kabisa isipokuwa walimu walicheza mchezo haram
Mtoto akirudia darasa taarifa zinaenda mamlaka husika na anapata kibali.Kama utaratibu ulifuatwa hakuweza kuwa na tatizo.Ushauru,mleta mada kamuone mwalimu mkuu wa shule anayosoma sasa mdogo wako ndo atakupa majibu mujarabu,ikishindikana nenda halimashauri kwa Afisa Elimu.Ushauri wangu .naomba ufuatilie sasa usipofuatilia alafu ukakuta hilo jina ni la mdogo wako. Tatizo kubwa Moja litatokea mwakani wakati anasajiliwa ili afanye mtihani was taifa drs la 7 ni kwamba itahitajika matokeo yake ya mtihan wa taifa drs la 4 na necta kule itaonekana jina Hilo limeshamaliza drs la 7 hivyo dogo hataruhusiwa kufanya mtihani. Siku hizi hakuna udanganyifu necta wapo kidigital mzee hakuna uhuni uhuni.
Muulize Baba yako kwa upole hekima busara adabu na heshima huenda nae ni mdogo wako mwingineshule ni hiyo hiyo na majina ni yote matatu yamefanana
ww umejuaje kama walicheza mchezo mkuu.
Usijazwa upepo mkuu mambo mengine sio ya kukurupuka, kumbuka jina halina dhamana yeyote anaweza kujiita kadili anavyopendezwa.
.
hapana mdogo wangu hakuwa mtoro kabisa isipokuwa walimu walicheza mchezo haram
Je, jina la mdogo wako kutoka limefaulu mwaka huu, linamzuia yeye kuchaguliwa kuendelea na masomo mwakani kama atafaulu? Aliyefaulu kwa jina hilo achana naye, wala usiwe na kinyongo nayeWakuu habari zenu? Mmeshindaje?
Sasa Wakuu kuna shida kidogo nahitaji ushauri wenu kuna mdogo wangu alikuwa anasoma Arusha shule ya msingi sasa kule kulitokea shida kidogo akaamishwa shule akaletwa Ukerewe.
Wakati anaamishwa alkuwa darasa la sita lakini shuleni alipohamia Mwalimu Mkuu akakataa kumpokea mpaka arudishwe darasa la tano, basi ikawa hivyo dogo akarudi darasa la tano.
Sasa maajabu yameibuka leo baada ya matokeo kutoka dogo bado yupo darasa la sita mwakani anamaliza darasa la saba lakini jina lake limetoka kwenye matokeo kwamba amefaulu kwa daraja B.
Baada ya hapo nikafanya kuulizia marafiki wakadai Mwalimu Mkuu aliuza jina kwa mrudiaji. Sasa nahofia hatima ya mdogo wangu mwakani atakapofika darasa la saba itakuwaje?.
Kwa wanasheria ebu mnishauri nifanye nini kwa mjibu wa sheria, maana kinachoniuma ni mtu mwingine kumiliki jina la ukoo wetu.
Wanasheria na wakuu naomba kuwasilisha
Unaweza fananisha majina matatu maana mtu anatambulika kwa jina lake la baba na la ukoo kwahyo yote yafanane au umetoka kuchambia pilipili umekuja kutafuta unga wa ngano tukakusugueMajina yanafanana, umejuaje ni la mdogo wako.