Msaada. Makadirio ya kodi kutoka TRA

Halafu bado kuna ile 10% ya kodi ya pango. Mfano unalipa kodi 100k na wewe umelipia labda miezi 6. TRA watataka uwalipe ten percent ya kodi ya pango kwa mwaka mzima hivyo utalipa 120k kwa mwaka ..wao hawajui umelipa pango kwa Muda gani..
Hivyo chukua 250,000+120,000 ndonupate tax clearance.
Ili kukupooza wanakwambia lipa kwa awamu nne..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwa biashara mpya unaandika wapi?
 
Mkuu acha tu. Mimi natakiwa kulipa 60,000 ya pango.
 
Sawa mkuu. Hii ni nchi pekee ambayo ukiwa honest unapigwa fine. Mimi naacha hii biashara nitawapa sababu za kuacha sina sababu za kukaa chini kuwalalamikia watu wasio jielewa. Wao vichwa vyao ni kodi tu. Na sidhani kama manager wao anaweza kuwa na mentality tofauti.
 
Yaani unaacha biashara kirahisi hivyo



Wewe huwezi biashara. Kaa chini na wadau na wazoefu wa baishara wakupige msasa. Usione Wafanyabiashara wanatembelea ma-Vogue mijini udhani Mambo ni smooth Kama unavyofikiri. Nchi hii ni mchakamchaka.
 
Ukienda kwa wale jamaa kwa uwaminifu kabisa unakuwa kama mbuzi uliyejitoa kafara. ..tafuta wazoefu kwanza kabla ya kuanza biashara. Halafu usiache biashara mkuu ..wee fungua tu kwanza fanya kazi maswala ya malipo ni baadae huko

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Ni bora umuone Manager wao kuliko kuacha biashara. Halafu hao ma officer wana mabosi wao pia ambao kazi yao ni kurekebisha makosa yao. Ingekuwa mimi kama sipati jibu nalotaka nitafika hadi kwa Commissioner General na mtaji wangu wa laki 7. Jiamini.
 
Mkuu kwa biashara mpya unaandika wapi?
Nunua hata counter book
Mfano umeanza biashara leo basi utakapouza page ya kwanza juu kabisa andika February then chini piga mistari yako mitatu kutengeneza kijumba cha tarehe, bidhaa uliouza, na chumba cha mwisho nia kiasi cha ulichouzia bidhaa
 
Mimi siwezagi kabisa kukaa niongee kwa kulia lia never.
Hivi viduka havina faida kabisa. Sasa huo muda nitacheza draft kuliko kusubiri mteja wa kiberiti faida yote niwape wao.
 
Mimi hata assistant manager simwoni. Wapuuzi sana hawa jamaa. Wakikadiria kodi unachukua kama ilivyo. Hawakupi muda wa kujieleza
Ni bora umuone Manager wao kuliko kuacha biashara. Halafu hao ma officer wana mabosi wao pia ambao kazi yao ni kurekebisha makosa yao. Ingekuwa mimi kama sipati jibu nalotaka nitafika hadi kwa Commissioner General na mtaji wangu wa laki 7. Jiamini.
 
Nitajipanga tena upya nitaanza. Ila silipi hii hela walahi.
 
Mkuu mimi nakumbuka ilichukua miezi mitatu Hadi nafanyiwa makadirio nilianza biashara mwezi wa kumi nikaenda tra waliniambia nifanye biashara kwanza mwezi January mwaka huu wakanikadiria kodi ambayo nalipa kila baada ya miezi mitatu
Una jina la gari yangu pendwa....
 
ulienda kufanya nn huko tra au ulikuwa unawapima mmeshaambiwa km biashara zenu hazizidi mtaji wa 4mil chukua kitambulisho cha machinga kaa nacho hapo dukani kwako hakuna atayekusumbua..
 
Ni kweli ila kwa sababu wengi hawajui wanapewa.makadirio ya ovyo hata.mimi nilipopata mtaalamu ndio akanifungua macho.
Kitu muhimu ni kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi kitu ambacho wengi hawafanyi.
Acha wendawazimu Mkuu, umeambiwa ndio kwanza ana anza biashara. Hizo kumbukumbu anazitoa wapi? CCM acheni upuuzi wenu aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…