Msaada lodge/motel/hotel nzuri Morogoro mjini

Msaada lodge/motel/hotel nzuri Morogoro mjini

Unajuaga kabisa kuwa sikoseagi goli nikipewa mpira.....we subiri matokeo.
Kitimoto ya kwa mama Kamche itatukoma.
Duuuu muda sana nimemiss eneo muhimu hilo
Nikija likizo toka hapa mafichoni lazima nitinge pale huku nikivinjari kanisa la kakobe

Shida ya wadau huwa hatutafutani,ujamaa wenu mwisho jf tu..
 
Wakuu habari zenu. Nimepata safari ya kikazi Morogoro na mimi ni mgeni.Naomba mnijuze lodge Nzuri maeneo ya mjini. Uwezo wangu ni Elfu 20,000/= kwa siku na nina tegemea kukaa kwa siku 5.
Natanguliza shukrani.
 
Nenda Tripple Double iko mkundi mjini ina huduma nzuri ikiwemo chakula chips za kuchemsha, mayai ya kobe na pilipili zenye sukari. Vyoo vyake ni vyeusi ila maji mekundu. Bafu zake ni za rangi ya Kijani na kuna picha ya duduwasha mlangoni. Kitanda cha mfinyanzi na godoro la chuma.
 
nategemea kwenda morogoro mjini mwezi June mwanzon. tafadhali naomba wenye uzoefu waniambie ni lodge/motel/hotel gani nzuri, usafi wa kutosha, yenye usalama wa kutosha, utulivu na bei kati ya sh 25,000 hadi 35,000/ per day
Mkuu umeshapata kibali cha kuja Morogoro? Siku hizi ukitaka kuja Mji kasoro bahari unatuma maombi kwa mkuu wa mkoa, halafu utembee na cheti cha ndoa kabisa maana ukikutwa chumbani uko na mwanamke bila cheti cha ndoa unalo!!
 
zipo nyingi tu morogoro mjini kianzia masika.. ukiuliza b1 lodge utaoneshwa.. mazingira ni mazuri na ulinzi wa uhakika
 
Wakuu habari zenu. Nimepata safari ya kikazi Morogoro na mimi ni mgeni.Naomba mnijuze lodge Nzuri maeneo ya mjini. Uwezo wangu ni Elfu 20,000/= kwa siku na nina tegemea kukaa kwa siku 5.
Natanguliza shukrani.
Nenda tabora motel, pazuri, pasafi na bei nafuu. google tabora motel utapata namba zao na bei za vyuma.
 
Nenda MATU LODGE ipo mtaa wa Mlapakolo ukivuka Mount Uluguru hotel mbele kuna Blue Palm bar hlf hesabu km nyumba tano upande wa kushoto utaiona,bei nafuu haizidi sh 10,000/= na ulinzi upo wa kutosha
 
Wakuu nawashukuru Sana. Nimefikia Star wings iliyopo kihonda. Nimepapenda ni pasafi Sana na vyumba vyao ni full AC
 
Nenda MATU LODGE ipo mtaa wa Mlapakolo ukivuka Mount Uluguru hotel mbele kuna Blue Palm bar hlf hesabu km nyumba tano upande wa kushoto utaiona,bei nafuu haizidi sh 10,000/= na ulinzi upo wa kutosha
matu lazma uondoke na kunguni kama luanda inn
 
Back
Top Bottom