Msaada kwa uso wenye mafuta

Toto mol

JF-Expert Member
Oct 18, 2022
2,412
3,583
Habari wadau kwema, niende moja kwa moja kwenye mada, ipo hivi naomba kujua ni mafuta gani? Yatanifaa kwa mtu kama mimi mwenye uso wenye mafuta,

Chunusi zinanisumbua kila nikipaka mafuta usoni, basi zitatoka balaa zinavimba, nisipopaka mafuta uso unarudi vizuri tu, ila shida inakuja kwenye mdomo unapauka kweli na kutoka magamba,

Inabidi nirudi tena kupaka mdomo, napo inakuwa sawa ila chunusi inakuja na kwenye mdomo yani, mnisaidie mafuta yatakayoukubali uso, ni mimi kijana wa miaka 27 tu
 
Kama usipopaka usoni hakuna changamoto basi acha kupaka. Mdomoni, ili kuleta unyevu unyevu na kuzuia midomo kupasuka, basi tumia Lip Balm au moisturizer.

Hizo hazitakuletea chunusi. Usiogope dhana pia ya kuwa wanawake ndiyo hupaka.

Kumbuka, siyo lipstick. Ni lip BALM. Yenyewe haiachi rangi, ni clear. Pakaa kisha utakapoona tena lips zako zinaanza kukauka, unapaka tena. Kumbuka pia kunywa maji mengi ili kuleta unyevu mdomoni.
 
Kama unapaka lotion acha, pakaa vaseline for men... kama mwanaume lakini
 
Attachments

  • 20231020_131642.jpg
    20231020_131642.jpg
    55.8 KB · Views: 26
Kama usipopaka usoni hakuna changamoto basi acha kupaka. Mdomoni, ili kuleta unyevu unyevu na kuzuia midomo kupasuka, basi tumia Lip Balm au moisturizer.

Hizo hazitakuletea chunusi. Usiogope dhana pia ya kuwa wanawake ndiyo hupaka.

Kumbuka, siyo lipstick. Ni lip BALM. Yenyewe haiachi rangi, ni clear. Pakaa kisha utakapoona tena lips zako zinaanza kukauka, unapaka tena. Kumbuka pia kunywa maji mengi ili kuleta unyevu mdomoni.
hivi vyakula pia haiwez kua inachangia hiyo hali?
mathalalani asubuh chai ya maziwa maarage na chapati mbili, mchana ugali samaki, usiku wali maharage na nyama vyote ni mafuta.
 
Mi sipaki mafuta usoni sababu nina mafuta ya kutosha...

Nang'aaa

Ila Sina chunusi ni msoft...

Nakushauri usipake mafuta usoni...

Mdomoni paka vaceline ya mdomo...
 
Habari wadau kwema, niende moja kwa moja kwenye mada, ipo hivi naomba kujua ni mafuta gani? Yatanifaa kwa mtu kama mimi mwenye uso wenye mafuta,

Chunusi zinanisumbua kila nikipaka mafuta usoni, basi zitatoka balaa zinavimba, nisipopaka mafuta uso unarudi vizuri tu, ila shida inakuja kwenye mdomo unapauka kweli na kutoka magamba,

Inabidi nirudi tena kupaka mdomo, napo inakuwa sawa ila chunusi inakuja na kwenye mdomo yani, mnisaidie mafuta yatakayoukubali uso, ni mimi kijana wa miaka 27 tu
Mkuu kwenye upande wa lips tumia asali na turmeric (manjano) hizo manjano zipo za aina mbili ukifika mwambie nataka ile ya vipodozi sio ya kupikia mchuzi. Changa asali na manjano in ratio ya 1:2 yaani kijiko kimoja cha manjano kwa vijiko viwili vya asali au zaidi ya hapo kwa kuzingatia ratio hyo paka kwenye lips ukitaka kulala usiku (lazima) na asubuhi ukienda kwenye shughuli zako.

Kwenye suala la ngozi yako kuna vitu viwili kuna ngozi yenye mafuta na ngozi isiyo na mafuta na kuna aina mbili za ingredients kwenye vipodozi kuna (AHA'S & BHA'S) wewe unatakiwa utumie vipodozi vyenye au mafuta yenye BHA'S ndio yatakusaidia.

AHA'S- kirefu chake ni Alpha hydroxy acids kama:citric acid na lactic acid ni plants and animals derivative hii ni hydrating agent.

BHA'S-Kirefu chake ni Beta hydroxy acids kama:salicylic acid hii ndio inakufaa kwasababu ni dehydrating agent.

Kwa hyo tafuta yenye ingredients ya BHA'S Ungekuwa karibu ningekufundisha kutengeneza mwenyewe unatakiwa upate facial serum mkuu na lotion yenye ingredients hzo.
 
1. Paka mafuta ya Vaseline Men ya lotion.
2. Usiguse uso wako mara kwa mara na mkono(kiganja) ambao haujausafisha.

3. Usilale ukiwa umepaka mafuta.
Kila ukiamka usiku safisha uso wako.

4. Kunywa maji mengi lita 2.5-3-5

5. Kwa wiki mara moja paka Magadi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom