Mwenye uso wa mafuta, tumia mafuta ya ubuyu hutajutia

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,373
Wakuu,

Kwa wale wanaosumbuliwa na uso wa mafuta hasa ule ambo ni rahisi kupata chunusu (acne prone skin), tumia mafuta ya ubuyu bila kuchanganya na chochote utakuwa umemalizana na tatizo lako na uso wako utakuwa nyororo na wenye afya.

Kwanini Mafuta ya ubuyu yatatibu tatizo lako la chunusi;

Sababu kuu za mtu kupata chunusi ni hizi zifuatazo:

Mafuta kuzidi(excess oil production).
Bacteria.
Kuziba kwa vitundu vya ngozi (clogged pores)
Kutowiana kwa homoni (hormonal imbalance)

Kwahiyo ukitumia mafuta sahihi kwenye ngozi yako utaondoa sababu 3 kati ya nne zinazosababisha chunusi kwa sababu baadhi ya mafuta ni anti-bacteria na pia anti-infalamatory na yanarekebisha uzalishaji mafuta (sebum production).

Tafiti zinaonyesha kwamba watu wanaosumbuliwa na chunusi wana kiwango kidogo cha linoleic acid (hii acid ndiyo husaidia kurekebisha kiwango cha uzalishaji wa mafuta kwenye ngozi), kwahiyo ukiwa nayo kidogo ina maana ngozi yako itazalisha mafuta kwa wingi na hivyo kuziba vitundu vya ngozi na kuleta chunusi.

Kwahiyo ukitumia mafuta ambayo yana hii linoleic acid nyingi yatarekebisha (balance) uzalishaji wa mafuta na hivyo kuzuia chunusi.

Kwahiyo mafuta mazuri kwa watu wenye ngozi za chunusi ni ambayo;

Yanarekebisha uzalishaji wa mafuta.

Hayazibi vitundu vya ngozi (low on comedogenic scale, hapa ina maana mafuta mazuri ni yale ambayo kwa kipimo cha uzibaji vitundu (comedogenic scale) yapo kati ya 0-5 na si zaidi.

Kwahiyo kwa ngozi ya mafuta yenye kupata chunusi kirahisi mafuta yatakayofaa ni yenye kiwango kikubwa cha linoleic acid na kiwango kidogo cha oleic acid.

Hapa ndipo tunasema mafuta ya ubuyu yanafaa sababu katika comedogenic scale yanasomeka 2 (kumbuka kipimo ni kuanzia 0-5) kwa hiyo mafuta haya wanayawekwa katika kundi la non-comedogenic (hayawezi kuziba vitundu vya ngozi na pia yana kiwango kizuri cha linoleic acid (kurekebisha uzalishaji mafuta kwenye ngozi) yaani sebum production.

Hizi hapa faida za mafuta ya ubuyu kwenye Ngozi;

Yana vitamini zaidi ya nane 8;
1. Vitamin A- Kuweka unyevu kwenye ngozi.

2. Vitamin B1 (Thiamine) - Kuondoa mikunjo.
Vitamin B2 (Riboflavin) - Kurekebisha ngozi.
Vitamin B3 (Niacin) -Kinga ya ngozi.

3. Vitamin C (Ascorbic acid) - Kuondoa sumu, na ina vitamin C mara 6 zaidi ya chungwa.

4. Vitamin D - Kukuza na kukarabati seli za ngozi.

5. Vitamin E (Tocopheral) - Kulainisha ngozi.

6. Vitamin K - Kuongeza uwezo wa ngozi kupona majeraha.

Madini yaliyomo, yana Madini 7;

1. Calcium- Kurekebisha uzalishaji mafuta.
2. Manganese - Kurekebisha PH ya ngozi.
3. Iron - Kukinga na mionzi ya jua.
4. Pottasium - Uzalishaji seli za ngozi.
5. Zinc - Kuondoa miwasho ya ngozi.
6. Phosphorus - Kukarabati tishu za ngozi.
7. Amino acids - Kusambaza unyevu.

Fatty Acids
Pia yana acids zaidi ya 9;
1. Omega 3 (Linolenic acid)
2. Omega 6 (Linoleic acid)
3. Omega 9 (Oleic acid
4. Palmitic axcid
5. Stearic acid
6. Dihydrosteraulic acid
7. Stecuric acid
8. Malvalic acid
9. Arachidic acid

Faida ya hizi acids ni kwamba, hizi kitaalamu wanasema ni antinflammatory, maana yake ni kwamba yana uwezo wa kupambana na maambukizi ya ngozi kama vile miwasho, mba n.k, na pia kuzuia mionzi ya jua (UV rays).

Collagen
Collagen inasaidia ngozi kujivuta na kuzuia kuzeeka kwa ngozi. Jinsi tunavyokua kiumri uzalishaji wa hii collagen hupungua, hivyo mafuta ya ubuyu huongeza zaidi uzalishaji wake kufanya ngozi isizeeke.

Mimi nina ngozi ya mafuta na nilikuwa mhanga wa tatizo hili, ila baada ya kuanza kutumia mafuta ya ubuyu nimeondokana kabisa na tatizo la chunusi na sasa naifurahia ngozi yangu, kwani hata yale makovu ya chunusi yameisha kabisa.

Uzuri wa haya mafuta unaweza kujipaka kuanzia kichwani hadi kwenye unyayo, kwani yana faida lukuki kuanzia kwenye nywele ikiwemo kusaidia kukuza na kuzipa afya nywele, kwenye ngozi ya mwili yanasaidia kuing'arisha ngozi na kuondoa mabaka na weusi (hapa kina dada ule weusi katikati ya mapaja) na kurudisha rangi asili ya ngozi yako.

Pia kwenye kucha inasaidia kuzuia kucha kukatika hasa za miguuni. Kuna wale watu ambao kucha zao hupasuka au kukatika, mafuta haya ni suluhisho lake. Pia wale ambao wanasumbuliwa na kupasuka visigino inasaidia, paka kisha vaa viatu vyako.

Nilipoanza kutumia nilikuwa na weusi fulani mikononi, hasa vidole na hii inasababishwa na kutumia sabuni za unga, lakini nikashangaa ule weusi uliondoka na ngozi ikarudi katika rangi yake ya asili.

Pamoja za faida zote nilizotaja hapo juu, uzuri wa mafuta haya ni ya asili hivyo hayana madhara kwa afya yako, na hata asiye na ngozi ya mafuta anaweza kutumia pia.

Tupende kutumia mafuta ya asili, mafuta mengi ya viwandani yana kemikali zinazoathiri ngozi na hata ukiona wameandika mfano kuna vitamin E, bado huna uhakika kama ni kweli ipo au hata kama ipo ni kwa kiasi gani cha kuisaidia ngozi.

Mwisho, ukitaka kutumia haya mafuta ya ubuyu nunua ya humu nchini Tanzania (mengi yanatoka Dodoma) sababu ukinunua ya kutoka nje unaweza kukuta yameshachakachuliwa na usipate faida unazitarajia.

Asante.

#Tunza ngozi yako:

UBUYU.jpg
 
View attachment 2429711
naomba kuuliza,haya mafuta yanatengenezwaje?

yaani ubuyu unatoaje mafuta?
 
Mode acheni upumbavu,mnafuta comments za watu ili iweje?,mnapata nini?

jana nimeandika comment hapa kumuomba BIN NUN asiache kutoa elimu hii,nae mmefuta,kuna ubaya gani kwenye comments ile?,huu ni upumbavu na ujinga,mnadhani mitandao ni JF tu?,ipo siku mtakosa watu wajinga ninyi;

NIMECHOKA KUBEMBELEZA;

Kama ni ban pigeni;
Kuna tatizo gani mkuu?uliandika kitu gani ambacho Mods wamefuta?
 
Sintokasahau kale kabinti.Aliponiuzia sikuyachunguza nikiamini angekuwa muaminifu.Nilipoenda kuyaangalia upya ndipo nikakutana na kiroja hicho.Alinitwanga kofi la machoni.
Kama mimi siyajui nikiwa nanunua ntajuaje Kama haya ndo yenyewe au kanyanga
 
Back
Top Bottom