Msaada kwa tuta: GHARAMA ZA KUWEKA SOLAR POWER | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada kwa tuta: GHARAMA ZA KUWEKA SOLAR POWER

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kamarada, Mar 21, 2011.

 1. K

  Kamarada Senior Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hi wanafamily wa JF!!

  Plz, nataka kuweka Umeme wa jua kwa kibanda yangu, loc- Mbezi Temboni Dsm, iwe na uwezo wa kuwasha bulb za wts 40 or less idadi 8, kucharge simu, kutumia Laptop and if possible kuwasha ka-fridge kadogooo.

  Plz, wataalam Techn hii naomba mnipe estimate ya gharama ya kazi hiyo and may be wapi naweza pata mafundi wa kuifanya kazi hiyo.

  Thnx in advance vile najua JF ni kama ENCYLOPIDIA!!
   
 2. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kw kuwa upo DSM fika shekilango-Millenium Business Park jirani na duka(bata) la kuuza viatu kuna kampuni inauza hivyo vifaa unaweza kufika na kupata maelezo.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu kamarada mimi pia nimetoka kufanya research kuhusu hiyo kitu na bahati nzuri matumizi yako ni kama yangu tu ila mimi nilihitaji kuwasaha na TV.
  Gharama ya solar kwa mujibu wa mahitaji yako, ungeipata ile ya shilingi laki tano.
  Lakini wataalamu wameniambia solar power kwa bei nafuu na imara, zinapatikana Mbeya tena ukiweza kwenda Tunduma ndio utapata kwa bei nzuri na mashine nzuri zaidi. na hata hiyo ya bei niliyokutajia ni kwa huko Mbeya.
  Mimi nimeshaagiza ya kwangu.
  Kuwa makini na solar power feki.
   
 4. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Fridge unayotaka kutumia ni ipi? ni ya umeme wa kawaida au maalum kwa solar? kama ni ya kawaida basi unahitaji kujua hiyo fridge yako watts ngapi inakula. Watts za fridge kujumlisha na watts za taa/vifaa ambavyo kwa wakati mmoja vitatumika ndio utapata kujua solar panel(s) za watts ngapi unahitaji.
  Link hizi hapa chini wasiliana nao watakupa ushauri, kuna Zara solar power mitaa ya kkoo uhuru/msimbazi

  http://helveticsolar.com
  Rex Investment Limited - Tanzania's leading solar energy contractor - Home
  Na wengine hawa.....

  • Address: 3rd Floor, NSSF Building, Ubungo, Dar Es Salaam,
  • Telephone: +255 (0) 22 2450 468
  • FAX: +255 (0) 22 2450 468


  • Address: P. O. Box 3786, Uhuru Msimbazi Round about, Dar es Salaam, Tanzania
  • Telephone: +255 782325283/717930390


  • Address: P. O. BOX 26, Millenium Business Park, Morogoro/Shekilango Road near Ubungo. , Dar Es Salaam, Dar Es Salaam Tanzania
  • Telephone: +255 22 2401374/5
  • FAX: +255 22 2401376
   
 5. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,045
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa anataka makadirio ili labda ajipange vizuri badala ya kwenda hapo na kuanza ku-raise expectation za wauzaji. Anachotaka ni kama umeweka umeme huo ulitumia Tsh Ngapi kwa requirements zake? Nawasilisha
   
 6. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Aisee embu toeni estimationa bana msituambie tuende millenium,hapa tunataka data sio dar guide hii,watu wengi tunahitaji hii
   
 7. K

  Kamarada Senior Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkuu Ndibalema nimekusoma vema, ni vile tu nilisahau kuorodhesha na TV. Thanx kwa ushauri wako wa mwanzo. Kwa Mby/Tunduma hizi product si lazima zinatoka Dsm au wao wana-import toka South Via Zim/Zambia? But ngoja tuendelee kuwasikiliza waungwana humu jamvini, twaweza pata a proper Xpert!
   
 8. K

  Kamarada Senior Member

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkuu De Javu, thanx kwa links na Contact hizo, nazifanyia kazi. Wanafamily wengi humu ndani ni wahitaji wa hii kitu hasa during these Richmond Ngeleja's days, so plz endeleeni kutusaidi kupata a proper analysis ie. Items zinazohitajika, may be type and Quantity, Estimated price, ikiwezekana hata gharama za kiufudi kama kuna injinia wa hii kitu. Otherwise shop owners wanaishia kutupatia price list though technically bado hatujajua tunatakiwa kununua nini cha quqality and quantity ipi.
  Once again thanx Mkuu De Javu, sambamba na Wakuu: Mwamanyika, Ndibalema pamoja na wahanga wenzangu Nyati & Son of Peasant a.k.a Mtoto wa Mkulima/ PM? vile mmetuptia pahala pa kuanzia.
  Big up JF!!
   
 9. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ukifika hata Mafinga na Makambako wana solar nyingi sana wao wanasema wanazipata toka Malawi kwa bei nzuri ila kwa suala la ubora sijui. Kwahiyo inawezekana hao wa Tunduma wanazipata toka Zambia.
   
 10. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  NIMESIKIA KUNA JAMAA PALE EXTRENAL ANAUZA UMEME WA MAPANGA BOY NA PANGABOY LINAWEZA KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA MATUMIZI YOTE YA NDANI NA HATA UKAUZA UMEME KWA MAJIRANI YAANI UKAWA KATANESCO BINAFSI HII IKOJE KAMA KUNA MTU ANAFAHAMU ZAIDI TAFADHALI ATUJUZe
   
 11. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hi wasiliana na kampuni hii wako more reliable 0786 148148, wapo kariakoo msimbazi/makamba street opposite Akamba Bus Terminal
   
 12. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Jee unamaanisha umeme wa nishati ya upepo?
   
 13. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu Nyati hapa ilikuwa ni suala la kutoa msaada na msaada wa nyavu ni bora kuliko samaki. Au ni kama mtu anahitaji shilingi mia ukimsaidia hamsi ashukru na aitafute inayobakia kwingine.
   
 14. K

  Kamarada Senior Member

  #14
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Uko sawa Mkuu, pia nimeambiwa pale Mafinga kuna chuo VTC cha KKKT kinafundisha hii technologia na kinao mafundi pia. Thanx kwa muongozo mzuri!!
   
 15. K

  Kamarada Senior Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  Du Mkuu hii inaweza kuwa nzuri zaidi, but vp ile sheria ya u-monopoly wa TANESCO ilikwisha ondolewa? If kwisheney then yaje makampuni kama ilivyo fanyika kwa sekta ya mawasiliano. Freemarket Bongo haiwezi kuwa giza...
   
 16. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Solar power requirements:
  *Solar panel(S): Panel ya kufyonza nguvu za jua, huwekwa nje iweze kupokea mwanga wa jua ni lazima uiweke sehemu ambayo itapata muda mwingi wa jua bila kivuli (maximum sunlight). Kuna aina nne za solar panels.
  1-single crystalline au mono crystalline efficiency up to 12%
  2-poly crystalline au multi crystalline efficiency up to 10-11% moreless kama single (bora single)
  3-string ribbon efficiency 8-9% and last
  4-thin film or amorphous 5-7% efficiency
  Ukiangalia utaona type 1 and 2 hazipishani na ndio bora lakini 3 and 4 ni cheaper pia inadaiwa kua type 3 zina dumu au kuchakaa kwake ni polepole kulinganisha na type zingine. Solar panel zote zinaweza kudumu kufikia hadi miaka 20.
  Solar panel zipo ukubwa wa aina mbali mbali na uwezo(watts) tofauti kuna panel za watts 30w, 50w, 60w au zaidi, kulingana na mahitaji yako unaweza kutumia panel moja au hata zaidi; ni muhimu kupiga mahesabu ya mahitaji yako ya matumizi ie taa ngapi na kama unahitaji kutumia mashine za jikoni kama fridge/blender etc. Nyumba ya vyumba 4/6 bila mashine yeyote panel ya 60w inatosha, ukichukulia kua si wakati wote taa zote zitawaka. (energy saver bulbs za kileo sio zile za kizamani)
  Charge controller: kazi yake ni kudhibiti nguvu za jua kwenda kwenye battery
  *Inverter: kubadili nguvu za umeme toka 12volt kwenda 220/240v(kwa umeme wa Tz), ikiwa hutumii vitu vya 220/240v basi huhitaji kifaa hiki (kama vifaa vyako ni vya 12v)
  *Cables/wiring: kama ilivyo wiring ya kawaida ndani ya nyumba
  *Battery: Battery kama ya gari, hapa ni muhimu :- matumizi makubwa yanahitaji powerful battery, mfano kama vile ilivyo kwa gari dogo basi battery ni ndogo, gari kubwa/lorry/Bus battery yake lazima iwe kubwa; kadhalika kama matumizi yako ni makubwa ie... taa nyingi pamoja na vifaa vingine basi pia unahitaji battery kubwa.Hii ndio inakua ndio bank ya umeme wako.
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mkuu asante kwa ufafanuzi wako. Sasa naomba niulize ikiwa nina nyumba ambayo nahitaji kuwasha taa 16, tv, blender, fridge dogo na pasi ndogo yenye watts 500. nahitaji pannel ngapi na zenye watts rating ngapi, na pia inverter iwe ya watts ngapi?
  Na kwa soko hapa nchini gharama ya vifaa hivyo itakuwa shilingi ngapi?

  Naomba msaada hapo.
   
 18. K

  Kamarada Senior Member

  #18
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  Mkuu De Javu, kwanza pokea FIVE then nimekupa Bonge la M-thanx! All after hebu tutafunie ya hoja ya Kiongozi mwingine hapo chini juu ya gharama.
  Infact JF ni zaidi ya shule!!
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Itakugharimu milioni moja na elfu ishirini kwa aina ya mahitaji uliyoyataja boss hiyo nipamoja na kukufikishia saiti na kukufungia kwa maelezo zaidi fika ofisini Yecco (T) Ltd posta upanga street cont 0715865544/0755...0788...au yeccotltd@yahoo.com
   
 20. K

  Kamarada Senior Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwa kuwa wewe ndo mwenye ofisi, nadhani ingependeza zaidi ukaweka na mchanganuo wa hizo gharama other than tukupigie ama kuja kwa ofisi. Fahamu kuwa siyo wahitaji wote wapo Dsm/ Tz kwa sasa, but wanaweza fanya biashara na weye through ndg zao. Unge-outline bei za vifaa, tpt, gharama za ufundi na guarantee kama ipo.
  Thanx!
   
Loading...