Msaada kwa tuta: Gharama za kuweka solar power

Itakugharimu milioni moja na elfu ishirini kwa aina ya mahitaji uliyoyataja boss hiyo nipamoja na kukufikishia saiti na kukufungia kwa maelezo zaidi fika ofisini Yecco (T) Ltd posta upanga street cont 0715865544/0755...0788...au yeccotltd@yahoo.com

mkuu .... kuna thread ulianzisha inahusu kupatikana kwa internet bundles za bei rahisi .... lakini uliingia mitini

authenticity required
 
Solar power requirements:
*Solar panel(S): Panel ya kufyonza nguvu za jua, huwekwa nje iweze kupokea mwanga wa jua ni lazima uiweke sehemu ambayo itapata muda mwingi wa jua bila kivuli (maximum sunlight). Kuna aina nne za solar panels.
1-single crystalline au mono crystalline efficiency up to 12%
2-poly crystalline au multi crystalline efficiency up to 10-11% moreless kama single (bora single)
3-string ribbon efficiency 8-9% and last
4-thin film or amorphous 5-7% efficiency
Ukiangalia utaona type 1 and 2 hazipishani na ndio bora lakini 3 and 4 ni cheaper pia inadaiwa kua type 3 zina dumu au kuchakaa kwake ni polepole kulinganisha na type zingine. Solar panel zote zinaweza kudumu kufikia hadi miaka 20.
Solar panel zipo ukubwa wa aina mbali mbali na uwezo(watts) tofauti kuna panel za watts 30w, 50w, 60w au zaidi, kulingana na mahitaji yako unaweza kutumia panel moja au hata zaidi; ni muhimu kupiga mahesabu ya mahitaji yako ya matumizi ie taa ngapi na kama unahitaji kutumia mashine za jikoni kama fridge/blender etc. Nyumba ya vyumba 4/6 bila mashine yeyote panel ya 60w inatosha, ukichukulia kua si wakati wote taa zote zitawaka. (energy saver bulbs za kileo sio zile za kizamani)
Charge controller: kazi yake ni kudhibiti nguvu za jua kwenda kwenye battery
*Inverter: kubadili nguvu za umeme toka 12volt kwenda 220/240v(kwa umeme wa Tz), ikiwa hutumii vitu vya 220/240v basi huhitaji kifaa hiki (kama vifaa vyako ni vya 12v)
*Cables/wiring: kama ilivyo wiring ya kawaida ndani ya nyumba
*Battery: Battery kama ya gari, hapa ni muhimu :- matumizi makubwa yanahitaji powerful battery, mfano kama vile ilivyo kwa gari dogo basi battery ni ndogo, gari kubwa/lorry/Bus battery yake lazima iwe kubwa; kadhalika kama matumizi yako ni makubwa ie... taa nyingi pamoja na vifaa vingine basi pia unahitaji battery kubwa.Hii ndio inakua ndio bank ya umeme wako.

JF rocks!!! nime google hii kitu, vuup nikarudishwa JF. asante sana kwa maelezo mazuri mheshimiwa De Javu
 
Kwa kuwa wewe ndo mwenye ofisi, nadhani ingependeza zaidi ukaweka na mchanganuo wa hizo gharama other than tukupigie ama kuja kwa ofisi. Fahamu kuwa siyo wahitaji wote wapo Dsm/ Tz kwa sasa, but wanaweza fanya biashara na weye through ndg zao. Unge-outline bei za vifaa, tpt, gharama za ufundi na guarantee kama ipo.
Thanx!
Jamani mfumo wa solar wenye kuweza kusambazwa kwenye majengo matatu, kwaajili ya shule unagharimu kiasi gani?
 
Rex sijui whatever, utaambiwa a hel of expences. Fanya hivi. Nisomee vifaa vyako vina watt ngapi na vitawaka kwa muda gani katika masaa 24. Mfano taa10 za watt 8@ zinawaka masaa 8 hapo = 8*10*8=640watt., hivyo unatakiwa kujumlisha watt zote kwa kila kifaa na idadi utakayopata ongeza na 20% ya hiyo idadi ambayo ni autonomous hours. Ndo utadetermine ni plant ya ukubwa gani utahitaji. Ila kwa hataka tu unahitaji kama panel 5 za 100watt, na betry dry 2 N200@ 13amps regulator
 
Back
Top Bottom