Msaada kwa hili

isack raphael

Senior Member
Oct 26, 2013
131
195
Habari..
Naomba ushauri, nifanyeje ili kiingereza nikizoee na kukitumia kama navyokitumia kiswahili (naweza cha kuombea maji)
 

Kifyatu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,385
2,000
Habari..
Naomba ushauri, nifanyeje ili kiingereza nikizoee na kukitumia kama navyokitumia kiswahili (naweza cha kuombea maji)

Soma vitabu (novels) vya kiingereza kwa wingi. Hii itakuongezea msamiati wako na pia utaona maneno yanavyotumika. Mimi mwenzio ndio kilichonisaidia.
 

Fadhili Paulo

Verified Member
Sep 1, 2011
3,220
2,000
Soma vitabu vya kiingereza hasa vile vyenye habari/hadithi unazozipenda zaidi, sikiliza radio zinazotangaza kwa kiingereza kwa sehemu kubwa kama vile choice fm, kiss fm, tbc international etc, soma magazeti ya kiingereza, sikiliza muziki wa kiingereza ukiwa na mashairi yake, waza mambo kichwani kwa kutumia kiingereza, mwisho tafuta marafiki facebook wanaongeza kiingereza na uchat nao kwa kiingereza muda wote. Mwisho kabisa usikate tamaa.
 

isack raphael

Senior Member
Oct 26, 2013
131
195
Soma vitabu vya kiingereza hasa vile vyenye habari/hadithi unazozipenda zaidi, sikiliza radio zinazotangaza kwa kiingereza kwa sehemu kubwa kama vile choice fm, kiss fm, tbc international etc, soma magazeti ya kiingereza, sikiliza muziki wa kiingereza ukiwa na mashairi yake, waza mambo kichwani kwa kutumia kiingereza, mwisho tafuta marafiki facebook wanaongeza kiingereza na uchat nao kwa kiingereza muda wote. Mwisho kabisa usikate tamaa.

Nashukuru mkuu,nishaanza kufanyia kazi
 

Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,329
1,500
Kama ukiwa unaweza kujiunga kwenye mitandao ya kijamii ambayo wanatumia lugha tofauti itakusaidia. Nenda icq. com then tafuta jukwaa ambalo ni la kingereza ujumuike nao
 

mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Sijui kama unapenda / unaweza kutumia internet kujifunza Kingereza, lakini kama ni hivyo, websites ifuatayo ni bora na labda zinaweza kukusaidia pia:
---------------------
Kusoma na kusikiliza Kingereza (at the same time) BBC Worldservice Learning English ni bora.
Learning English - General & Business English (Bonyeza)
Chini ya General & Business English menu, "6 Minute English" na "English at Work" hasa inafaa.

Learning English - Grammar, Vocabulary & Pronunciation (Bonyeza)
Chini ya "Grammar, Vocabulary & Pronunciation" menu, "The English we speak" hasa inafaa.

Website ya BBC infaa sana kwa sababu yapo mazungumzo (conversations) mengi ya Kiingereza ya kila siku na zaidi ya hayo unaweza kusoma na kusikiliza at the same time. Pia, kulia na juu ya webpage nyingi unaweza kufungua audio file na text file, au kudownload yote kwenye computer yako (ukiwa na computer!)! Lakini kama ukitaka kusoma na kusikiliza at the same time kwenye internet, lazima to right-click on the audio au text file and then to choose the option "open link in new window". Ndipo utafungua files mbili separately ili kusoma na sikiliza pamoja.
---------------------
Kwa English grammar hii inafaa kuliko nyingine kadiri nilivyoona:
ENGLISH PAGE - Online English Grammar Book Hapa ni index. (Bonyeza)
Hii ni Homepage: Advanced English lessons (Bonyeza)
-----------------------------------------------
Mimi ni mwalimu wa Kiingereza hapo Uingereza katika shule ya kimataifa. Mimi ninajitahidi kujifunza Kiswahili. Naweza kusema kujifunza lugha nyingine ni kazi kubwa. Unahitaji motivation na kujitoa kwa muda mrefu kama ukitaka kuboresha level yako. Nashauri usome Kiingereza ya kwa kawaida sawasawa na level yako na endelea hatua kwa hatua. Usisome masomo au nakala ngumu kwako – itakuchanganyika na hutajifunza vizuri! Mimi nilipata faida kubwa sana katika kujifunza Kiswahili cha kila siku niliponunua na kusoma vitabu vya shule, "Tujifunze Lugha Yetu"! Kwa hiyo nashauri BBC hapo juu kama ni sawawa na level (kipimo?) yako. Wengine tayari walikushauri vizuri ila nilitaka kuzidisha kidogo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom