Msaada: kwa anayeishi Arusha

Msaada: kwa anayeishi Arusha

EveningStar

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2018
Posts
262
Reaction score
162
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume (30), hivi karibuni nimepangiwa kazi Arusha maeneo ya Namanga, ila mimi ni mgeni sijawahi kufika Arusha kabla na ukizingatia nitaishi huko, hivyo naomba kwa wenyeji wa huko wanifahamishe kuhusu upatikanaji wa vyumba na gharama zake na hali ya usalama.

Mawasiliano zaidi PM.

Ahsanteni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa vyumba vya kawaida vile vya magetoni kwetu ukihamka unona kila kitu chako,umeme,maji,geti ndani kwa ndani,usiwaze ni 40000.
 
Ni mji wenye anasa nyingi na wajuaji wengi,hivyo umakini unahitajika sana kwa ugeni wako.
vinginevyo ni mahali salama pa kuishi.
 
Namanga ipo mkoa wa Arusha ila kilometer kadhaa kutoka mjini kwa umbali wa 60mins.

Maiha ya pale yamechangamana kutokana na kuwa karibu na mpaka wa nchi ya Kenya hivyo kupelekea kitongoji hicho kuwa changamfu wakati wote.

Kwa ujumla kama umeishi kitongoji chenye pirika pirika huwezi kushindYwa kuishi hapo, tatizo lake sehemu za mipakani kuwa makini kutokana na mazingira ya muingiliano.

Nimeishi mpakani na chumba nilikuwa nalipia 30,000 kizuri kukiwa na usalama, weekend nilikuwa najimwaga mitaa ya Koinange jijin Nairobi.
 
Ahsante sana mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namanga Ni mbali na Arusha, Kama Lisaa moja na nusu kutoka Arusha mjini, mpakani na Kenya. Maisha sio ya gharama Sana, usalama upo sababu ni mpakani. Ni kamji kadogo Sema mpaka ndo umepachangamsha

Ila wajuaji na matapeli wengi sababu hizo ndo kazi za mipakani kutapeli wasafiri wasioelewa kitu. So ukifika kuwa makini Hadi uzoee kabisa mazingira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom