Msaada kupata uzoefu kuendesha Semi, semitrella n.k

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,680
12,254
Ndugu zangu kama kichwa Cha habari kinavyo jieleza, kijana wenu nimerudi tena najua hapa jamiiforums ni junguu kuu lisiloisha ukoko, ambamo ndani yake Kuna watu wa Kariba na hali tofauti tofauti. Nipo mkoani Dar es salaam kwasasa.

Nilipambana nikasoma udereva wa awali hivyo kuendesha gari najua, hivi sasa ndoto zangu ni kuendesha magari makubwa ya mizigo, iwe semi, na gari nyinginezo zinazo fanana na hizo.
1695871904470.png

Kikubwa ninacho omba kama Kuna mtu anaendesha gari hizo, ama anazo naomba anisaidie tusafiri wote walau wiki Moja TU au hata mwezi ikiwezekana. Ili nipate nafasi ya kuizoea hiyo gari.

Kwenye swala la chakula na mahitaji yangu mengine ya kibinaadam nitajitegemea.

Nimatumaini yangu maombi haya yatamfikia mtu sahihi na atanisaidia Kwa kadri ya anavyoona inafaa.

Nb.

Sijawahi kuomba msaada humu Jf nikapata 😭😭😭😭😭😭😭😭😭 eh Mungu fanya miujiza nilitukuze Jina lako...🙏🙏​
 
Upo wapi? Taja eneo ulipo uelekezwe kwa kwenda kujichanganya na wenye hayo magari alafu ni watu peace sana Ila tu wanakuaga na sheria zao si unataka kua Tandiboi au Utingo anaejifunza hayo magari
Nipo dar es salaam ndugu yangu. Nitafurahi sana kama utanisaidia
 
Hao jamaa kuna maeneo yao hua wanapaki ndio inabidi uwafuate wanapopaki ukaongee nao physically km upo Dar chukua Gari shuka Mwananchi mbele ya Mwananchi km unaelekea Ubungo pale kuna sehemu wanapaki yapo mengi tu ni km parking yao wakitoka mikoani wanapak pale ingia mule ndani ongea nao hawatokutosa watakusaidia nimeshakupa njia, ninachomaanisha hawa jamaa ili wakusaidie inabidi uwafuate physically wakuone wakuelewe ndio wakukubarie
 
Shukrani sana. Nitafanyia kazi maoni yako
 
O kama sijakosea😭😭😭
Jibu ni sawa.

Dunia hii inaongozwa na siri na ukiijua siri itakuweka huru. Kuna kitu kinaitwa Laws of attraction. +1(Unaomba msaada) halafu hapo hapo unasema (sijawahi kupata humu msaada) –1. Matokeo ya jibu lako lazima yawe ziro kutokana na hayo maneno wewe mwenyewe umeyatamka au yaandika.

Ulishawahi kujiuliza hivi kwanini wanasema unapata unachostahili na sio unachokitaka?

Tafuta muda wako kisha kaisome hiyo law
 
IPO kwenye kitabu Gani hiyo...?
 
We jamaa bhana...
Unataka ufwate DM kwamba njoo kwenye hii Actros nyeupe hapa ubungo?
Maisha hayapo hivo, nenda yanakoshinda magari husika, wapo watu wengi tu utakutana nao na utajua kama kweli utaweza au uendelee na haraki zingine.

Nla
 
Jibu ni sawa.

Dunia hii inaongozwa na siri na ukiijua siri itakuweka huru. Kuna kitu kinaitwa Laws of attraction. +1(Unaomba msaada) halafu hapo hapo unasema (sijawahi kupata humu msaada) –1. Matokeo ya jibu lako lazima yawe ziro kutokana na hayo maneno wewe mwenyewe umeyatamka au yaandika.

Ulishawahi kujiuliza hivi kwanini wanasema unapata unachostahili na sio unachokitaka?

IPO kwenye kitabu Gani hiyo...?
Uko Google utapata articles tofauti ila theme ni moja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom