Kuomba msaada wa kuchangiwa kupata chombo cha usafiri (bajaji)

Goodluck Mshana

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,271
1,119
*KUOMBA MSAADA WA KUCHANGIWA KUPATA CHOMBO CHA USAFIRI (BAJAJI)*

Habari zenu Ndugu, Jamaa na Marafiki

Naitwa *David Marsha*, Mtanzania mwenye changamoto ya ulemavu wa miguu.

*HISTORIA YA TATIZO*

Ndugu/Marafiki zangu sikuzaliwa na hii changamoto bali niliipata ukubwani wakati nafanya masomo yangu chuo cha wanyama Pori (Mweka), mwaka 2007.

Nilipata ajali ya gari na kunisababishia kupata tatizo la *"uti wa mgongo na kupooza viungo vyangu vya mwili kuanzia shingoni mpaka miguuni"*

Nililala kitandani kwa muda wa miaka 3 ndio nikaanza kupata nafuu ya mwili na kuanza kukaa na kutembea kwa msaada wa Wheelchair .

Ilipofika mwaka 2012 niliona ni vema kufanya jambo litakaloniweka bize kuliko kuendelea kukaa ndani tuu, hivyo niliamua kufungua biashara ya duka la nguo, lkn changamoto ilikuwa ni *usafiri* kwenda sokoni Ilala asubuhi kuchukua nguo kuja kuuza dukani kadhalika kuwafikia kwa karibu na kwa wakati wateja waliopo mbali.

Kutokana na hali yangu sikuweza kutembea Muda mrefu kwa kutumia Wheelchair mpaka kituo cha daladala pia na changamoto ya kugombania kupanda daladala, na pia sikuweza kubeba mzigo mzigo mkubwa na kulazimika kutumia/kukodi usafiri wa Taxi

Gharama ya usafiri wa taxi ilikuwa kubwa sana ukitegemea kukodi taxi (kufuata mzigo sokoni na kunirudisha dukani) ilikuwa Gharama kidogo ikilinganishwa na kiwango cha mtaji niliowekeza katika Biashara yangu!

Mwisho wa siku nilishindwa kuendesha biashara yangu, kutokana na gharama na changamoto kibiashara kuwa kubwa zikijumuisha Usafiri, Pando, Kuwafikia wateja waliopo mbali na eneo langu la biashara n.k

Kutokana na changamoto tajwa hapo juu, nililazimika kufunga biashara na kupata wazo la kurudi Chuo kuendelea na masomo kwa kuwa Elimu ni ufunguo wa maisha.

Mwaka 2013 niliomba nafasi chuo kikuu Dar es salamu (UDSM) na kufanikiwa kujiunga, japo changamoto zilikuwa nyingi lkn namshukuru mungu nilifanikiwa kumaliza degree yangu ya SOCIOLOGY mwaka 2016.

Kwasasa nipo mtaani japo sijafanikiwa kupata ajira, nimejaribu kujiajiri tena kwa kufungua biashara ya jiko la nyama choma lakini maeneo ya Mwananyamala nilipata changamoto lakini bado nilikabiliwa na changamoto zilezile za gharama ya usafiri kutoka ninapoishi (Kimara) mpaka Mwananyamala ilipo biashara, hivyo pesa yote ya faida mpaka mtaji ikawa inaishia kwenye usafiri.

Nashindwa kufanya mambo mengi binafsi ya kuyatengeneza maisha yangu kwasababu ya uzewezekano mdogo wa kufika na kushiriki biashara ambazo ninaamini ndizo sehemu ya maisha yangu. Naamini katika kujiajiri zaidi japo kazi za maofisini hutupatia sehemu ya uzoefu kiutendaji.

*OMBI KWENU NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI*

Baada ya kuwaeleza baadhi ya ndugu na marafiki changamoto hii ya usafiri wamenishauri nipate BAJAJ (pikipiki ya miguu 3) chombo ambacho kitanisaidia kutoka sehemu 1 kwenda sehemu nyingine kwa gharama nafuu ya mafuta, vilevile uwezo wake wa kubeba wheelchair yangu na mizigo ya biashara yangu.

Pamoja na mambo mengine kikubwa na cha muhimu zaidi ni *Kuweza kuhudhuria effective mazoezi ( physio therapy) muhimbili*, kwa sasa natakiwa kuhudhuria mara 4 kwa wiki ambapo imekuwa changamoto kubwa sana kwangu kufanya effective kwasababu ya gharama kubwa za usafiri (kukodi taxi)

Gharama ya kununua BAJAJ mpya ni *sh. milioni 6*, niseme ukweli kwamba binafsi *"uwezo"* wa kununua BAJAJ sina.

Nimefikiria ninao marafiki na ndugu ambao tunapendana ni vema nikawashirikisha hili jambo japo wakanichangia kiasi watakachoguswa kutoka moyoni niweze kukusanya hicho kiasi cha milioni 6 nikapate mkombozi wa Biashara zangu.

Nafahamu kuwa hali ya uchumi wa nchi ilivyo na pia nafahamu kutaja milioni 6 ni pesa nyingi ila naamini kwenu nyie marafiki na ndugu zangu tukishikamana mkinichangia kutoka moyoni ni pesa ndogo. Ninaamini mnaweza kunikwamu hapa nilipo na kuandika historia nyingine ndani ya maisha yangu.

Hivyo kama ndugu, rafiki, classmates wangu nikuombe mchango wako kiasi chochote mnitoe kwenye changamoto za gharama za usafiri wa Taxi angalau na mimi nipambane kuyajenga maisha yangu. Umri unaenda na mimi nahitaji kuacha alama katika maisha yangu!

*NAWASHUKURU SANA PIA NAWAPENDA*

*------------------*
NO. ya kutuma mchango wako ni:- *Tigo pesa 0715 016 464 - Idda Masha* au 0659458415 (David Mambea)

CRDB Bank Acc. *0112095628000* - David Mambea Mshana.
*------------------*
6638188b07a079a60dd82737c9b3d9ea.jpg
3cc2cfd4e35a712fc8a3fc124c030dc7.jpg
023e58ea93de6380ba88806e6ab82972.jpg
 
Haha..
Rubii uko kama Mimi... Ulivyofikiria sivyo ulivyomkuta.. Ulidhani atakuwa rough...
Anyway ndo hali halisi ya Mawazo yetu coz co ww tu bali mi pia
Hahaha wakuu mmejawa na vituko... Huyo ni my younger Bro...ameniomba nimsaidie kushare kwa wana JF kwa atakaye guswa basi amsapoti kwa chochote!
 
Ukitaka jambo hili jema lifanikiwe na watu wawe na amani wasiliana kwanza na Moderator wakuhakiki na wakuthibitishe kwanza.... na watawathibitishia wana Jf kuwa wamesha kuthibitisha....
Ok..
Wazo zuri.... Naomba moderator aje kwa mahojiano na kujiridhisha juu ya taarifa hizi...
 
Ukitaka jambo hili jema lifanikiwe na watu wawe na amani wasiliana kwanza na Moderator wakuhakiki na wakuthibitishe kwanza.... na watawathibitishia wana Jf kuwa wamesha kuthibitisha....
Ok..
Kwel kabsa ikawa ni kwel kabsa,kiukwel nami nitakuchangia cchote ambacho nitaweza,kiroho saf kabsa bila kinying tena nitatoa huku natabasam na sitaacha kuja kukuunga mkono kwenye biashara yako ili iendelee zaid.. Pole sana bro
 
Ila familia yenu inaonekana ya kishua kiaina pole sana mkuu hujafa hujaumbika kila la kheri tutashirikiana katika maombi jambo ili lifanikiwe
 
Pamoja na ushauri mzuri wa kupitisha maombi kwa moderator, Goodluck Mshana ni mwanachama mwaminifu wa JF kwa jina, kwa picha na kwa "reputation". Hajifichi kama sisi wengine hivyo walau anaaminika.
 
Back
Top Bottom