Msaada kunusuru suala hili

sasa na yeye kinachomfanya asuse kumfuatilia mkewe ni nini? ndo amesusa hadi mlo kabisa?! muambie asijivunge bana, amuulize maswali na kumfuata. inawezekana huyo mkewe nae si kama alikuwaga anafurahia kumfukuzia mumewe kila siku,ila basi sasa afanyeje inabidi alale mlango wazi!
ila mwanaume akitoka kwenda kwenye kilaji mwanamke alikuwa anafuatilia kila baada ya dk kadhaa mara umekaa na nani unatoka saa ngapi na mwanaume asiposema muda halisi wa kurudi atashangaa mwanamke amefika anamjoin hata kama alikuwa na wenzake wanaongea
 
Hilo limwanamke lake la rafiki yako lzm litakuwa na mapepo ya kutosha yaan jamaa kuacha kazi iwe nongwa,km vp ampige chini tu mwanamke gani hana hata huruma na mwanae mchanga hivyo?kiukweli amenitia hasira sana huyo sijui mwanamke au shetan.
 
Kesi za ndoa haziishi!

ndo mana twasema mmu ni bwagamoyo,kisima cha utulivu,pumziko la wenye msongo wa mawazo,ukumbi wa maliwazo,mashine ya kushusha mastress,Husninyo ukiona manyoya ujue kuku ameliwa,ukiona mtu kajifunua mmu jua yamemkuta,we msaidie mawazo mtoa mada,he must be in dire straits kama sio yeye basi mtu wake wa karibu.
 
kuna msemo...wen poverty enters thru the door love escaes thru the window...na hilo ndio lilimtokea jamaa yako hapa...akubali imekula kwake tuu hapa
 
Huwa wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...................kaka hapa anavuna alichokipanda unakuta wakati alivyokuwa na Kazi alikuwa ni wa kumtoa wife out na pombe kwa sana kama vile wapo kwenye uboyfriend na Ugirlfriend wakati wao tayari ni wanandoa............Mama kaamua kubaki kwenye starehe....Jamaa atafute kazi na apeleke mtoto kwa Bibi yake akalelewe huko na arudi aendeleze ligi na mke wake wote ni watu wa Sterehe.Miaka miwili ya ndoa mnakunywa na kustarehe mpaka usiku ndoa gani hiyo.
 
....kuna ndoa zinahitajika kuwekewa mabango kama haya...
Slow-Down-For-Monkeys.png
 
labda ndo utaratibu wao wa maisha kaka. muulize rafiki yako wakati akia kwenye enzi yake ilikuwaje? kuna mwanaume akiulizwa na mkewe uko wapi,anasema rose garden.ukimuambia niko hapa sayansi nakuja mume wangu, anakuambia niko salender bridge! labda hawaambianagi ukweli,kila mtu ana mapenzi yake,na wanakua na sababu nzuri tu.

Lakini hata hivyo king'asti huyu dada hapa anamkomoa nani? mumewe au mtoto? mbona mtoto ni mdogo mno kuadhibiwa kisa eti baba alikua anapitiaga rose garden au sijui wapi wapi. Wakiachana halafu mtoto akalelewa na mama wa kambo huyo mama akianza kumtesa mnalaumu mama wa kambo. Wanawake na sisi bwana wakati mwingine
 
wanajamvi

nimekutana na mkasa huu nikaombwa ushauri nikaona nililete jamvini kupata mawazo zaidi..

Jamaa analalamika kuhusu mabadiliko ya tabia ya mkewe hasa makundi na ulevi . wameishi kwa kipindi cha miaka miwili tangu waoane ndoa ya kimila, mwanzo walikuwa na maelewano mazuri na hata mambo mengi walikuwa wanashirikiana katika kufanya na kuamua..
kama miezi 6 iliyopita jamaa alipata matatizo kazini yakapelekea yeye kuamua kuacha kazi ili kujinusuru na maswaiba mengineyo.. sasa mke amekuwa na makundi ya kike na kiume na kila mtu anasema n mfayakazi mwenzake , sometime anamwita jamaa awajoin kwenye kinywaji (pombe) but inakuwa in last minute.

Mke anaweza kukaa kwenye ulevi hadi saa sita usiku au nane usiku ndo anarudi nyumbani.
jamaa mwanzo alikuwa anapenda kumuuliza labda alipo anaishia kuambia yupo point A kumbe hayupo au akaambia niko njiani nakuja kuanzia saa 4 hadi 7 usiku ndo anaingia .. kwa sasa hawana maelewano mazuri ndani ya nyumba kwani jamaa ameshakuta msg hata za mapenzi kwenye simu ya mkewe na mkewe akashindwa kumshawishi jamaa na jamaa anaamua kukaa kimya maana alishawahi kutoa vipigo ila anaona kama dharau inazidi..

Ksasa hawaongei ni kama week ya tatu, mke anaweza kutoka hata kuaga hakuna na hata akirudi sometime hamsalimii jamaa na jamaa ameamua kusitisha hata huduma ya chakula cha usiku ..

Jamaa anafikiria kuachana nae ila anaumia kwani wana mtoto mchanga ana miezi 5 na mke alimwachisha ziwa mtoto akiwa na miezi 2..

Wana jamvi hili mwalionaje??

Anamuonea huruma mtoto sasa huyo mtoto anapata raha gani hapo kutoka kwa mama yake? Mmama anaeweza kuacha mtoto wa miezi mitano hm na yeye kwenda bar kila siku huyo mtoto akifikisha umri wa mwaka na kuanza kutembea si ndio atakua anatelekezwa hata wiki?
 
maty, ukiskiza kesi ya ndoa upande mmoja utaona jinsi hawa watu wako biased. ukiona simba amekimbia ameacha mtoto ujue ngoma imebamba. hapa anaonekana mbaya huyo mwanamke tu,unajua ukimpewa huyo baba unaweza ukamuua ukasahau kumrudisha kwa mkewe! siamini kaka mwanamke ana pumzi ya kunywa pombe kila siku na kurudi saa nane za usiku.manake hata hawa wanaume wanaojidai wanakunywa hadi saa nane usiku tunajua kabisa kuna mahali anapita kunyoosha mgongo na kupunguza usingizi ila kwa vile mkewe ana ushahidi basi tena kesi inapotelea hewani! huyo wivu tu unamsumbua,kwa vile hana kazi mkewe akirudi home kapita mahali mara mojamoja na washkaji akanywa bia 2 roho inamtoka. same as mwanamke ambae ni mama wa nyumbani,mume akirudi saa nne usiku kanywa bia 4 unajiskia kama analala nje manake toka atoke asubuhi unamsubiria aje upige nae michapo mpenzi wako. nimetaka kumpa mtoa mada majibu calm,ambayo huwa wanatupa sie tukilalamika na tukakasirika wanatuona wa ajabu. hahaha,nadhani umenielewa,lol
Lakini hata hivyo king'asti huyu dada hapa anamkomoa nani? mumewe au mtoto? mbona mtoto ni mdogo mno kuadhibiwa kisa eti baba alikua anapitiaga rose garden au sijui wapi wapi. Wakiachana halafu mtoto akalelewa na mama wa kambo huyo mama akianza kumtesa mnalaumu mama wa kambo. Wanawake na sisi bwana wakati mwingine
 
Asante Kingast hawa watu bwana .......................kama ulivosema mwanzo mkuki kwa nguruwe kwao huwa ni mchungu kuliko shubiri

maty, ukiskiza kesi ya ndoa upande mmoja utaona jinsi hawa watu wako biased. ukiona simba amekimbia ameacha mtoto ujue ngoma imebamba. hapa anaonekana mbaya huyo mwanamke tu,unajua ukimpewa huyo baba unaweza ukamuua ukasahau kumrudisha kwa mkewe! siamini kaka mwanamke ana pumzi ya kunywa pombe kila siku na kurudi saa nane za usiku.manake hata hawa wanaume wanaojidai wanakunywa hadi saa nane usiku tunajua kabisa kuna mahali anapita kunyoosha mgongo na kupunguza usingizi ila kwa vile mkewe ana ushahidi basi tena kesi inapotelea hewani! huyo wivu tu unamsumbua,kwa vile hana kazi mkewe akirudi home kapita mahali mara mojamoja na washkaji akanywa bia 2 roho inamtoka. same as mwanamke ambae ni mama wa nyumbani,mume akirudi saa nne usiku kanywa bia 4 unajiskia kama analala nje manake toka atoke asubuhi unamsubiria aje upige nae michapo mpenzi wako. nimetaka kumpa mtoa mada majibu calm,ambayo huwa wanatupa sie tukilalamika na tukakasirika wanatuona wa ajabu. hahaha,nadhani umenielewa,lol
 
ndo matatizo ya kuoa wanawake wasiojitambua. Mwambia ahangaikie maisha yake huyo mwanamke atamuua.
 
jamani, inafikia sehem maisha yanakuwa ni magumu sana, sio tu ache wivu kama wadau walivyo sema, lakini ifikie kipindi asimame kama mwaume tena baba wa nyumba, ATOE MAAMUZI MAGUMU asiwe mdhaifu kiasi hicho. kama anuwakika kuwa anatembea nje ya ndoa amwache.

MALTIN LUTHER KING alisema :- "its better to die free, than to live as a slave "
 
huyo mke au balaa la mke, haya mume humpendi , hata huyo mtoto jamani, mtoto wa miezi mitano kweli hata nguvu anazitoa wapi za kukaa baa, aaarrrgghhh, shame
 
hizi maada zingine zinatutia hofu ambao hatujaingia kwenye ndoa,kama ni hvi bora niendelee kuwepokuwepo kwanza ila kwakuwa nilishweka post moja ya kuhitaji mwenzi ngoja niendelee kumsubiri huyo ambaye atakuwa anakuja asubuhi kubadilisha nguo ili aende kazini
pole sana mkuu ila naona hakuna ndoa hapo,ndoa pesa
 
kwani pumzi hiyo achana naye!,unaogopa mwanao atapata tabu mkiachana mbona hapo mlipo ni kama anapata taabu tayari mwanamke anayekuja saa nane usiku ameplay part gani kama mama?,huyo ulikosea tangia mwanzo kumuoa wanawake sio wa kushinda kwenye mabaa especially kama una mtoto mchanga....whether mumeo naye ni mlevi or not si staha mwanamke kushinda baa...kaka anza moja hio ndoa ishakfa tayari hamna maelewano hamna tendo la ndoa unasubiri nini??mbona unazubaa mtoto peleka kwa bibi yake for the time being huku ukitafuta kazi nyingine kwa bidii ukipata oa mwingine this time kuwa careful.
 
Hilo limwanamke lake la rafiki yako lzm litakuwa na mapepo ya kutosha yaan jamaa kuacha kazi iwe nongwa,km vp ampige chini tu mwanamke gani hana hata huruma na mwanae mchanga hivyo?kiukweli amenitia hasira sana huyo sijui mwanamke au shetan.

mimi kwa kweli alipogusia swala la mtoto ndipo hasira ilipanda kwa jinsia ninavyofeel suala la watotot halafu mtu hajui mwane ana hali gani toka asubuhi roho inaniuma hata kama anapata taarifa kwa simu haitoshi kama kumuona kwa uhalisia
 
Back
Top Bottom