Msaada kunusuru suala hili

BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
573
wanajamvi

nimekutana na mkasa huu nikaombwa ushauri nikaona nililete jamvini kupata mawazo zaidi..

Jamaa analalamika kuhusu mabadiliko ya tabia ya mkewe hasa makundi na ulevi . wameishi kwa kipindi cha miaka miwili tangu waoane ndoa ya kimila, mwanzo walikuwa na maelewano mazuri na hata mambo mengi walikuwa wanashirikiana katika kufanya na kuamua..
kama miezi 6 iliyopita jamaa alipata matatizo kazini yakapelekea yeye kuamua kuacha kazi ili kujinusuru na maswaiba mengineyo.. sasa mke amekuwa na makundi ya kike na kiume na kila mtu anasema n mfayakazi mwenzake , sometime anamwita jamaa awajoin kwenye kinywaji (pombe) but inakuwa in last minute.

Mke anaweza kukaa kwenye ulevi hadi saa sita usiku au nane usiku ndo anarudi nyumbani.
jamaa mwanzo alikuwa anapenda kumuuliza labda alipo anaishia kuambia yupo point A kumbe hayupo au akaambia niko njiani nakuja kuanzia saa 4 hadi 7 usiku ndo anaingia .. kwa sasa hawana maelewano mazuri ndani ya nyumba kwani jamaa ameshakuta msg hata za mapenzi kwenye simu ya mkewe na mkewe akashindwa kumshawishi jamaa na jamaa anaamua kukaa kimya maana alishawahi kutoa vipigo ila anaona kama dharau inazidi..

Ksasa hawaongei ni kama week ya tatu, mke anaweza kutoka hata kuaga hakuna na hata akirudi sometime hamsalimii jamaa na jamaa ameamua kusitisha hata huduma ya chakula cha usiku ..

Jamaa anafikiria kuachana nae ila anaumia kwani wana mtoto mchanga ana miezi 5 na mke alimwachisha ziwa mtoto akiwa na miezi 2..

Wana jamvi hili mwalionaje??
 
mmmmh! sio kila sketi/gauni uionayo barabarani ukahisi ni mwanamke wengine ni majini ya kike sasa uyo rafiki ako alikutana na jini la kike
 
hivi kusitisha chakula cha usiku ni kumuadhibu mwanamke? najiuliza kama na mwanamke anayekerwa na mumewe anapositisha huduma ya mama n'gawie anakua ameadhibu ama ni kwamba hajisikii tu.
 
jamaa kasitisha kwa vile anadai mara kadhaa anahisi anavamia chakula kilicholiwa (kina tope) maana anaweza kurudi amelewa akifika analala sometime anasikia harufu ya sabuni isiyotumika kwake
 
Arghhhh...i can smell another divorce and new street kid is born...

Another one's dream put on vain soon or later is gonna die....

Ni bora kungoa kiungo chako kinachokukwaza kuingia peponi kuliko kuingia motoni jehanam na viungo vyako vyoote...

Maamuzi magumu ni hatua mojawapo ya muhimu katika kuleta maendeleo ya kweli ya mwanadamu...

A man was born to die continuously and to start afresh....
 
wanajamvi

nimekutana na mkasa huu nikaombwa ushauri nikaona nililete jamvini kupata mawazo zaidi..

Jamaa analalamika kuhusu mabadiliko ya tabia ya mkewe hasa makundi na ulevi . wameishi kwa kipindi cha miaka miwili tangu waoane ndoa ya kimila, mwanzo walikuwa na maelewano mazuri na hata mambo mengi walikuwa wanashirikiana katika kufanya na kuamua..
kama miezi 6 iliyopita jamaa alipata matatizo kazini yakapelekea yeye kuamua kuacha kazi ili kujinusuru na maswaiba mengineyo.. sasa mke amekuwa na makundi ya kike na kiume na kila mtu anasema n mfayakazi mwenzake , sometime anamwita jamaa awajoin kwenye kinywaji (pombe) but inakuwa in last minute.

Mke anaweza kukaa kwenye ulevi hadi saa sita usiku au nane usiku ndo anarudi nyumbani.
jamaa mwanzo alikuwa anapenda kumuuliza labda alipo anaishia kuambia yupo point A kumbe hayupo au akaambia niko njiani nakuja kuanzia saa 4 hadi 7 usiku ndo anaingia .. kwa sasa hawana maelewano mazuri ndani ya nyumba kwani jamaa ameshakuta msg hata za mapenzi kwenye simu ya mkewe na mkewe akashindwa kumshawishi jamaa na jamaa anaamua kukaa kimya maana alishawahi kutoa vipigo ila anaona kama dharau inazidi..

Ksasa hawaongei ni kama week ya tatu, mke anaweza kutoka hata kuaga hakuna na hata akirudi sometime hamsalimii jamaa na jamaa ameamua kusitisha hata huduma ya chakula cha usiku ..

Jamaa anafikiria kuachana nae ila anaumia kwani wana mtoto mchanga ana miezi 5 na mke alimwachisha ziwa mtoto akiwa na miezi 2..

Wana jamvi hili mwalionaje??

Ama kweli ndoa ndoano,...na kweli huu ni mkasa.

Kwa upande wangu habari ya mwanaume kuanza kudharauliwa na mke/mpnz wake inategemeana sana na mwanaume mwenyewe alivyo na mambo yake(haiingii kabisa eti mke wangu aje saa 6 uck half amelewa,mara sms za mapenzi kisa sina kazi mmmmh),jabari ya kuachana naye alaf eti unaogopa mtoto tena mmoja nayo mm naona kama ni kioja(kwani yy huyo mwanamke hajui kwamba ana mtt mpaka afanye upuuzi kama huo)
Anyway_mm ni mfuasi mzuri wa modern mfumo dume(kamwe sio mnyanyasaji ila naitambua na kuifanyia kazi nafasi yangu kama baba),...ushauri wangu aachane naye no matter what
 
lol! wivu utamuua! hapo sasa si ndo utakuta anampa huyo mwanamke sababu kabisa ya kuendelea kwa raha zake manake akija anajua hakuna usumbufu? muambie aache wivu banaa,dada wa watu anaongea dili za hela tu huko,si unajua dili za hela zinafanyika kwenye kilauri? ama kweli mkuki kwa nguruwe!
jamaa kasitisha kwa vile anadai mara kadhaa anahisi anavamia chakula kilicholiwa (kina tope) maana anaweza kurudi amelewa akifika analala sometime anasikia harufu ya sabuni isiyotumika kwake
 
Arghhhh...i can smell another divorce and new street kid is born...

Another one's dream put on vain soon or later is gonna die....

Ni bora kungoa kiungo chako kinachokukwaza kuingia peponi kuliko kuingia motoni jehanam na viungo vyako vyoote...

Maamuzi magumu ni hatua mojawapo ya muhimu katika kuleta maendeleo ya kweli ya mwanadamu...

A man was born to die continuously and to start afresh....

Well said mkuu..
 
Mwambie asione taabu kumwaga mkewe maana muda si mrefu atamuua yeye na maradhi...kwa hiyo ni bora abaki yeye alee mwanae wa miezi mi5 kuliko kuendelea naye wafe yeye na mkewe mtoto wao abaki yatima
 
Mpe pole jamaa! Kiukweli naamin maridhiano ya wawili walioko ndoani ni jambo la msingi zaid lakin kama hata hayo hayafikiwi jamaa anatakiwa kuchukua maamuzi magumu na ahiari kulea kiumbe chake ktk mazingira yeyote kwan ndoa ishaingia doa.

Najiuliza huyo mtoto kaachishwa kunyonya na kama bado ananyonya ni kwa namna gan na ni muda gan mtoto anapata haki yake na kama sio kulishwa uchafu? Jamaa afanye maamuzi magumu, ujue uvumilivu humshinda hata mwenye imani.

Mpende akupendaye, asiyekupenda pia usimchukie!
 
lol! wivu utamuua! hapo sasa si ndo utakuta anampa huyo mwanamke sababu kabisa ya kuendelea kwa raha zake manake akija anajua hakuna usumbufu? muambie aache wivu banaa,dada wa watu anaongea dili za hela tu huko,si unajua dili za hela zinafanyika kwenye kilauri? ama kweli mkuki kwa nguruwe!

kama dili ya pesa mbona akiulizwa alipo anaweza kusema yuko kazini au kuna mtu amepita kumuona kumbe yuko kwenye kilaji ??? kwa nini anaficha uwepo wake wa sehemu???
 
Mpe pole jamaa! Kiukweli naamin maridhiano ya wawili walioko ndoani ni jambo la msingi zaid lakin kama hata hayo hayafikiwi jamaa anatakiwa kuchukua maamuzi magumu na ahiari kulea kiumbe chake ktk mazingira yeyote kwan ndoa ishaingia doa.

Najiuliza huyo mtoto kaachishwa kunyonya na kama bado ananyonya ni kwa namna gan na ni muda gan mtoto anapata haki yake na kama sio kulishwa uchafu? Jamaa afanye maamuzi magumu, ujue uvumilivu humshinda hata mwenye imani.

Mpende akupendaye, asiyekupenda pia usimchukie!

mtoto kaachishwa ziwa na mama yake akiwa na miezi miwili tu na anatumia maziwa ya kopo
 
Mwambie asione taabu kumwaga mkewe maana muda si mrefu atamuua yeye na maradhi...kwa hiyo ni bora abaki yeye alee mwanae wa miezi mi5 kuliko kuendelea naye wafe yeye na mkewe mtoto wao abaki yatima

nashukuru mkuu
 
labda ndo utaratibu wao wa maisha kaka. muulize rafiki yako wakati akia kwenye enzi yake ilikuwaje? kuna mwanaume akiulizwa na mkewe uko wapi,anasema rose garden.ukimuambia niko hapa sayansi nakuja mume wangu, anakuambia niko salender bridge! labda hawaambianagi ukweli,kila mtu ana mapenzi yake,na wanakua na sababu nzuri tu.
kama dili ya pesa mbona akiulizwa alipo anaweza kusema yuko kazini au kuna mtu amepita kumuona kumbe yuko kwenye kilaji ??? kwa nini anaficha uwepo wake wa sehemu???
 
kama wife anamtelekeza mtoto hivyo,je mume?........hapo hamna ndoa tena,jamaa amtimue tu ila atafute namana ya kulea mtoto wake mwenyewe
 
labda ndo utaratibu wao wa maisha kaka. muulize rafiki yako wakati akia kwenye enzi yake ilikuwaje? kuna mwanaume akiulizwa na mkewe uko wapi,anasema rose garden.ukimuambia niko hapa sayansi nakuja mume wangu, anakuambia niko salender bridge! labda hawaambianagi ukweli,kila mtu ana mapenzi yake,na wanakua na sababu nzuri tu.

ila mwanaume akitoka kwenda kwenye kilaji mwanamke alikuwa anafuatilia kila baada ya dk kadhaa mara umekaa na nani unatoka saa ngapi na mwanaume asiposema muda halisi wa kurudi atashangaa mwanamke amefika anamjoin hata kama alikuwa na wenzake wanaongea
 
Well said mdau - hata mimi maoni yangu yanalenga huku huku - maana bi dada hana mapenzi sio kwako tu bali hat kwa mwanae mchanga hata ufanyaje hawezi badili tabia. Mtoto peleka kwa bibi
 
Back
Top Bottom