Ngoja nikuainishie aina za Mashina na kazi za Balozi wa nyumba kumi anayetokana na Ccm.
Aina za mashina:
1.Mashina yaliyo undwa ktk maeneo ya makazi maarufu kama Mashina ya nyumba kumi.
2.Mashina maalum yaliyo undwa katika Ofisi za Ccm,Jumuiya za wananchi zinazoongozwa na Ccm na Taasisi nyingine za Ccm.
3Mashina ya wakereketwa au Maskani kwa kule Zanzibar yaliyoundwa na wanachama wa Ccm katika maeneo husika baada ya kupata idhini ya Kamati ya Siasa ya Wilaya.
4Mashina ya nje ya nchi Mashina yaliyoundwa nje ya Nchi katika maeneo wanakoishi wanachama wa Ccm baada ya kupata idhini ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Kazi za Balozi wa shina (Balozi wa nyumba kumi) wa Ccm.l
1.Balozi au Mwenyekiti wa Shina atachaguliwa na Mkutano wa mwaka wa Ccm wa shina.
Atakua katika nfasi ya uongozi kwa muda wa miaka mitano.
Lakini anaweza kuchaguliwa tena baada ya muda huo kumalizika.
2. atakua na madaraka ya kuangalia mambo ya Ccm na utandaji kazi katika Shina.
3.Atakua kiungo cha wanachama wote katika Shina.
4.Atakua ndiye mwenezi na mhamasishaji mkuu wa siasa ya Ccm katika eneo lake.
5.Atakua na wajibu wa kuwaeleza wanachama maamuzi yote ya Ccm,kuwaongoza na kuwashirikisha katika utekelezaji wa maamuzi hayo na kufikisha mapendekezo ya wanachama katika vikao vya juu.
6.Atakuwa na wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa mambo yote ya siasa katika shina lake.
7.Atakuwa na wajibu wa kujenga uhusiano mwema wa wakazi wa shina lake kwa lengo la kuunda mazingira ya amani na utulivu.
8.Ataongoza Kamati ya Uongozi ya Shina pale panapohusika.
9.Atakua Mwenyekiti wa Mkutano wa Mwaka wa Ccm wa Shina na Mkutano wa Wanachama wote wa Shina.
10.Katika Mikutano atakayoongoza zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida atakua pia na kura ya uamuzi endapo kura zabwajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitalingana.
Isipokuwa kwamba kama kikao anachokiongoza ni kikao cha uchaguzi,Mwenyekiti atakua na kura yake ya kawaida tu.Hatakuwa na haki ya kutumia kura yake ya uamuzi endapo kura za wajumbe zimelingana.Wajumbe wa kikao wataendelea kupiga kura mpaka hapo mshindi atakapopatikana.
Hadi hapo hakuna sehemu palipo andikwa kwamba Balozi ni muajiriwa wa Serikali na pia hakuna sehemu iliyo andikwa kwamba Balozi anatoa kadi kwa wanachama wapya.
Katibu wa siasa na uenezi wa Tawi moja ya majukuku yake ni
Ibara ya 45 (a) Kusimamia kueneza na kufafanua masuala yote ya Itikadi,Siasa na Sera za Ccm katika Tawi.a
Moja ya majukumu ya Katibu wa Tawi ni.
Ibara ya 44 (4)Atashughulikia masuala yote ya Organaizesheni ya Ccm katika Tawi ambayoni
(a)Masuala yote ya wanachama.
Hapo nimekumegea kidogo tu ili upate picha ni wapi uanzie ila muhimu umjue Balozi wako kabla hujaenda Ofisi ya Tawi maana lazima utaulizwa eneo unaloishi na kikawaida Balozi nikama mdhamini wako.
;