Msaada: Kujiunga rasmi na CCM

Msaada: Kujiunga rasmi na CCM

Mimi kati ya vitu ninavyodhani sitakaa nifanye mpaka naondoka duniani ni kujiunga , kushabikia au kumpigia kura mtu yeyote mwenye unasaba na ccm. Mimi naamini pasipo shaka kuwa umasikini wa nchii hii, mateso ya watanzania , dhiki kuu tunayopitia kama raia chanzo chake ni ccm. Nchi hii hakuna na hakutakuwa na fisadi kama ccm. Hii ni imani yangu wala sikulazimishi uamini.
HIVI NI LINI CCM ILIJENGA VIWANJA VYOTE VYA MPIRA KILA MKOA NCHINI ? HUU NAO NI UFISADI WA KIHISTORIA
 
Maisha ya ajabu sana,kilichokushawishi kinaweza kuwa nini!? Huenda ukashawishi wengine.
 
watu kukosa utashi, kaomba msaada ajiunge na ccm, nyie mnaingiza chadema sijui mafisadi, utakuwa bashite wewe sio siri, ndio nyie mliofeli shule
 
Kwa Chadema sasa kila anayeachia ngazi hata kama ameyafanya maovu kiasi gani akiwa ccm kwao ni shujaa wao.Leo hii mnamwona kinana ni shujaa kweli? Mnamwona Mecky Sadik ni shujaa kweli Chadema mko serious mna nia ya dhati na mnaitakia mema nchi hii?
uzuri wa CCM ukiwa mwana chama wewe ni safi na mchapakazi kweli lakini ukijiuzuru hapo ndipo utaanza kusikia mpiga dili .mwizi.fisadi na kibwagizo cha mwisho huyu haitakii mema nchi yetu
 
Sina shaka na afya zenu
Wakuu nimeamua kwa dhati kabisa kujiunga na chama kikongwe nchini na chenye ushawishi mkubwa kwa wananchi wake ukiangalia falsafa, mtizamo na sera za chama. Hii haina maana nilikuwa upinzani no. mm nilikuwa neutral sikuwahi kumiliki kadi ya chama wala kushiriki kazi zozote za kichama. Leo baada ya kutafakari nikaona kama kijana nahitajika pia kujenga nchi yangu kupitia chama na hasa CCM.

Ombi langu kwenu wadau naomba mnipe mwongozo na taratibu za kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM)-[Revolutionary party]

Kidumu chama cha Mapinduzi
Asanteni
Nenda katika shina
Nenda na Picha Moja
Ada ni sh.300 kwa mwezi

Karibu chama kubwa Kiboko ya UKAWA.
 
Kabla ya kujiunga wakupe kwanza mkwanja kwa kuwa CCM ni Chama ambacho kimejengwa katika misingi ya ulaji.
 
Bora uwe mwanachama wa CCM kuliko kuwa chama cha wenye vurugu. Hata wakisimama majukwaani sera zao ni za chuki chuki tu. Na hapo ndipo ccm wanapowapiga gap.
Ukiona kiongozi mkubwa a anajiuzulu kipindi hiki cha baba Magu alikuwa mpiga deal
Acheni waondoke wengine watajiunga na chama

Na hii ndio inaowamaliza ccm..... yaani hamuamini kma mnakoseaga kabisa yaani meck sadick leo mpiga dili kisa kajiuzuru!! Ina maana magu alipomteua kuwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro hakujua ni mpiga dili?? Embu jifunzeni maana ya demokrasia na uhuru wa maoni hatuwezi wote kufanana kimtazamo.

Afu hicho chama cha vurugu ni kipi??? si mkifute kwa msajili au mkawafunge jela kma wanaleta vurugu!!!! Otherwise wao wakisimimamia serikali na kuikosoa ili ijirekebishe kwani ni nia mbaya??? Mbona kubana matumizi na kupunguza safari za nje lilipigiwa kelele sana kwenye M4C na nyie mmelishughulikia au hizo ndio chuki unazozisema
 
Kwa mwendo wa siasa za nchii zinavyokwenda hata mimi nafikiria hivyo kwani sioni mbadala wa ccm hasa kwa kipindi hiki cha Magufuli.
Mwendo gani mkuu!!! Huoni mbadala kwani hao wengine umewajaribu ukaona wameshindwa au kuonjeshwa sukari ndio unasema asali imekuwa chungu!!!!! Jifunze maana ya VYAMA VINGI ndio utaelewa kwanni marekani na maendeleo yote yale ila bado wana chama cha upinzani kikubwa tu na indeed wanabadilishana madaraka bila vurugu
 
Kwa Chadema sasa kila anayeachia ngazi hata kama ameyafanya maovu kiasi gani akiwa ccm kwao ni shujaa wao.Leo hii mnamwona kinana ni shujaa kweli? Mnamwona Mecky Sadik ni shujaa kweli Chadema mko serious mna nia ya dhati na mnaitakia mema nchi hii?
Kwani makene katoa official press release ya chama kuwaita hao mashujaa??? Au siku hizi jamii forums ndio ofisi za chadema zilipo!!! Kwanni maoni ya mtu mmoja mmoja tena anayetumia ID feki useme ni ya chama!! Hii tendency iishe mambo ya JF ni JF na chadema ni chadema
 
Sina shaka na afya zenu
Wakuu nimeamua kwa dhati kabisa kujiunga na chama kikongwe nchini na chenye ushawishi mkubwa kwa wananchi wake ukiangalia falsafa, mtizamo na sera za chama. Hii haina maana nilikuwa upinzani no. mm nilikuwa neutral sikuwahi kumiliki kadi ya chama wala kushiriki kazi zozote za kichama. Leo baada ya kutafakari nikaona kama kijana nahitajika pia kujenga nchi yangu kupitia chama na hasa CCM.

Ombi langu kwenu wadau naomba mnipe mwongozo na taratibu za kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM)-[Revolutionary party]

Kidumu chama cha Mapinduzi
Asanteni
Kama unawahi mgao wa hela ya rambirambi, Gumbo na mafisi wengine wameshazimaliza hivyo umechelewa. Itabidi usubiri tena maafa mengine yatokee tuchange rambirambi ndio na wewe ufaidike na mgao.
 
Bora uwe mwanachama wa CCM kuliko kuwa chama cha wenye vurugu. Hata wakisimama majukwaani sera zao ni za chuki chuki tu. Na hapo ndipo ccm wanapowapiga gap.
Ukiona kiongozi mkubwa a anajiuzulu kipindi hiki cha baba Magu alikuwa mpiga deal
Acheni waondoke wengine watajiunga na chama
Mkuu tupo pamoja tukijenge chama
 
Mimi kati ya vitu ninavyodhani sitakaa nifanye mpaka naondoka duniani ni kujiunga , kushabikia au kumpigia kura mtu yeyote mwenye unasaba na ccm. Mimi naamini pasipo shaka kuwa umasikini wa nchii hii, mateso ya watanzania , dhiki kuu tunayopitia kama raia chanzo chake ni ccm. Nchi hii hakuna na hakutakuwa na fisadi kama ccm. Hii ni imani yangu wala sikulazimishi uamini.
HIVI NI LINI CCM ILIJENGA VIWANJA VYOTE VYA MPIRA KILA MKOA NCHINI ? HUU NAO NI UFISADI WA KIHISTORIA
Umesema vizuri **kati ya vitu unavyozani**
 
Wajumbe wa nyumba kumi niwafanyakazi wa serikali sio chama mkuu..labda niulize ofisi zao hapa nilipo
Wajumbe wa nyumba 10 ni wafanyakazi wa CCM. Serikalini hakuna cheo hicho.
 
Sina shaka na afya zenu
Wakuu nimeamua kwa dhati kabisa kujiunga na chama kikongwe nchini na chenye ushawishi mkubwa kwa wananchi wake ukiangalia falsafa, mtizamo na sera za chama. Hii haina maana nilikuwa upinzani no. mm nilikuwa neutral sikuwahi kumiliki kadi ya chama wala kushiriki kazi zozote za kichama. Leo baada ya kutafakari nikaona kama kijana nahitajika pia kujenga nchi yangu kupitia chama na hasa CCM.

Ombi langu kwenu wadau naomba mnipe mwongozo na taratibu za kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM)-[Revolutionary party]

Kidumu chama cha Mapinduzi
Asanteni
mbona ni rahisi tu. nenda tawi la ccm lililoko karibu. kama wanawajibika vizuri watataka uhakika kama ni raia pengine maswali kadhaa. zamani kulikua na program ya maelekezo kuhusu sera na itikadi ya chama kabla ya kuingizwa rasmi. ccm ya magufuli huenda wamerudisha utaratibu huo.
 
Mwendo gani mkuu!!! Huoni mbadala kwani hao wengine umewajaribu ukaona wameshindwa au kuonjeshwa sukari ndio unasema asali imekuwa chungu!!!!! Jifunze maana ya VYAMA VINGI ndio utaelewa kwanni marekani na maendeleo yote yale ila bado wana chama cha upinzani kikubwa tu na indeed wanabadilishana madaraka bila vurugu
Siasa za marekani na Afrika hazishabihiani hata kidogo. Wenzetu kila chama kinajipambanua kwa sera zake hawayumbishwi namatukio. Sisi huku ni tofauti sana. Vyama vina sera ambazo havizisimamii, zimehifadhiwa kwenye makaratasi.viongozi na wanachama hawajui sera za vyama vyao. vinahangaika na matukio na matamko.
 
Sina shaka na afya zenu
Wakuu nimeamua kwa dhati kabisa kujiunga na chama kikongwe nchini na chenye ushawishi mkubwa kwa wananchi wake ukiangalia falsafa, mtizamo na sera za chama. Hii haina maana nilikuwa upinzani no. mm nilikuwa neutral sikuwahi kumiliki kadi ya chama wala kushiriki kazi zozote za kichama. Leo baada ya kutafakari nikaona kama kijana nahitajika pia kujenga nchi yangu kupitia chama na hasa CCM.

Ombi langu kwenu wadau naomba mnipe mwongozo na taratibu za kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM)-[Revolutionary party]

Kidumu chama cha Mapinduzi
Asanteni

Mtafute huyu atakusajili, Lizaboni.
CC Lizaboni.
 
Back
Top Bottom