Msaada kuhusu picha hizi.

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,390
Habari zenu wanaJF, pia napenda kuwakumbusha tuendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki cha majonzi. Mbele yenu nauliza matumizi, umuhimu, na faida za picha za viongozi katika ofisi za kiserikali. Nimekuwa nikiziona picha hizi mara nyingi sana sana ya raisi. Natanguliza shukurani za dhati kwenu.
 
mimi ninavyojua picha za viongozi zinawakilisha ufalme/utawala wao. hivyo unapokuwa ofisini kwako, picha hizo hubandikwa kwenye ukuta nyuma ya kiti unachokalia which means kazi zako zote unazozifanya, unizifanya kwa niaba ya huyo kiongozi ambaye picha yake iko ukutani nyuma ya kiti chako ofisini. na kwa nadharia hii, iwapo utaharibu kazi, means kaharibu kiongozi labda hajakupa maelekezo vizuri na ikigundulika umeharibu wewe kwa ujinga wako, kiongozi huyo lazima atakuwajibisha ili kusafisha jina na utumishi wake.
 
Ziko wapi?

inaonesha nyie bado wanafunzi wa chekechea, ndo maana mnashindwa kulijibu swali lake mtoa mada. fanya hivi, nenda kwenye ofisi yoyote ya ngazi ya wilaya, mkoa, hata kwa baadhi ya headmasters, angalia usawa wa kiti chake ukutani juu, utaona picha ya raisi wa jamuhuri.

au nenda kituo cha polisi chochote kilicho karibu na wewe, sema nina shida na OCD, angalia kwenye usawa wa kiti chake ukutani utaiona picha ya J.K.
Fanya hivyo kwenye kila ofisi ya serikali, lazima utaiona picha hiyo. na wengine huwa wanaweka na za maraisi waliotangulia kwa pembeni ya picha ya raisi anyetawala kwa wakati huu.

labda cha kufahamu hapa, zile picha huwa zinauzwa tena bei yake siyo ya kitoto. inaweza kutengawewa hadi 500,000/tsh kwa picha moja tu.

imekuwa ni migongo ya wao kupata pesa za walipakodi.
 
labda cha kufahamu hapa, zile picha huwa zinauzwa tena bei yake siyo ya kitoto. inaweza kutengawewa hadi 500,000/tsh kwa picha moja tu.
Ndo bei mkuu kwa JK zimebadilishwa mara mbili so watu wametoa 1,000,000.00 mpaka sasa
 
Habari zenu wanaJF, pia napenda kuwakumbusha tuendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki cha majonzi. Mbele yenu nauliza matumizi, umuhimu, na faida za picha za viongozi katika ofisi za kiserikali. Nimekuwa nikiziona picha hizi mara nyingi sana sana ya raisi. Natanguliza shukurani za dhati kwenu.
<br />
<br />
Unaongelea picha gani? Mbona sijaona picha yoyote sasa halafu unaomba msaada kuhusu picha!! Picha gani sasa? Aaarrrrghhhhhh
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom