Msaada kuhusu masuala ya kodi

Democrasia

Member
Feb 1, 2008
79
3
Jamani naomba msaada nina kampuni yangu na nilitakiwa kulipa VAT, Provisional Tax
Mimi likikuwa nimesafiri nikakuta kijana wangu amelipa vyote kwa paoja kwa kutumia cheki moja.
sasa naomba msaada wa yafuatayo:-J
*Kuna kosa lolote kisheria
*Je ukilipa VAT kwa commisioner of demestic revenue kuna kosa
*Na je unapochanganya mahala pamoja kuna kosa?
 
Pole kwa yaliyokutokea, lakini usijali, Kisheria si kosa, isipokuwa unatakiwa kuwaandikia TRA (Regional office yako ukiwajulisha kwamba katika 'cheque' namba fulani kulifanyika makosa ya kutotofautisha kati ya VAT na Provissional Tax, bila kuwapa taarifa 'Tax Account' yako na TRA itaonyesha kodi fulani umelipa zaidi na aina fulani ya kodi unadaiwa. Kwa namna nyingine unaweza kufuatilia TRA kujua kama cheque yako uliyolipa imewekwa fungu gani, kwa mfano kama imeingizwa katika 'Provissional Tax' 3rd Instalments na amount ni zaidi ya ulichotakiwa kulipa kama instalments, basi 4th Instalments utaipunguza ili katika mwaka usiwe umelipa zaidi ya kodi uliyokadiriwa ya 'Provissional tax'. Huu ndiyo ushauri wangu kwako juu ya masuala ya kodi.
 
ushauri sahihi kabisa kwakuongezea hutarudishiwa hela kama imelipwa Vat jua itabaki huko huko hadi mwezi unaofata utaclaim kama ni provisional itakua hivyo pia, na kama cheki imeenda Vat itabidi uandae nyingine ya incometax pia tafuta tax consultant wa kampuni yako
vinginevyo utajikuta kila siku unapigwa penati kwa kutokujua kwako, hao jamaa wanatabia ya kutafutaga makosa yaliyofanywa na taxpayer
 
Kwani hiyo VAT na provisional tax unatakiwa kulipa shemu/office tofauti? Zimelipwa kwa office inayostahili? Zimelipwa kwa wakati muafaka? Zote zinahusiana na kampuni moja?

Kama ritani ya VAT ilipelekwa kama inavyopaswa na hiyo provisional tax inaendana na ritani iliyokwisha wasilishwa...sioni tatizo hasa la kisheria. Unaweza kumwandikia kamishina au meneja wa mkoa wa kikodi unaohusika ukiambatanisha nakala ya ritani zote mbili kuonesha mchanganuo wa hiyo cheque uliyolipa (by the way, TRA wanakubali kulipwa kwa cheque?- I really doubt!).
 
Yote hiyo kwa ajili ya kutaka "cheap labor".

Ni kosa kumuachia mtu asiyejuwa mambo ya Taxation kukufanyia kazi zako za TRA, Mara nyingine uwawachie Auditors wako wakufanyie kama hauna mtu mwenye uzoefu.
 
Back
Top Bottom