Huyu mtoto ni wako.Habari,
Nina mtoto nimemlea kwa takriban miaka miwili hivi, nampenda sana uyu mtoto na ndo mtoto pekee nilienae kwa sasa ila njia ya mama yake na yangu zimeenda tofauti na kila mtu na maisha yake.
Kwa muda mrefu kidogo mtoto nlimpeleka kulelewa na bibi mzaa mama yake tena akiwa ananyonya baada ya mama yake kunitelekezea mtoto.
Nlimpa yule mama huduma zote za mtoto ikiwo bill ya maziwa na mahitaj mengine. Mtoto akaanza kusimama na kutembea akiwa kwa bibi nami nilimhudumia vizur tu.
Mama yake akaanza maneno kuwa mtoto sio wangu, akarudia na kurudia na kila nlipowashirikisha wazaz wake waliniambia nimblock kwakuwa ni hasira za kuwa mbali na mtoto kwakuwa japo alikutelekezea ila alipojua umemleta hapa nyumbani alimtaka mtoto ila tukamkatalia kwakuwa tumeshamwachisha nyonyo na kwamba mtoto aliletwa kwa maandishi kutoka serikal ya mtaa kwahiyo hawezi kutoka tena atakaa pale.
Basi nlipoambia ni hasira nkapuuza na kupuuza na kupuuza kila aliponitamkia hayo maneno.
Uvumilivu una kikomo, na ulikoma pale aliponitajia baba wa mtoto kwa jina kabisa na ni mwanaume ambae alishakuwa nae kimahusiano. Nikaacha kuhudumia vikaanza vikao visivyo na mwisho na visivyoeleweka na visivyo na suluhu. Nimesitisha huduma tangu mwez wa tisa.
Najiskia vibaya kutokumhudumia uyu mtoto hasa ikiwa ni wangu, ila ntajiskia vibaya kama ntahudumia mtoto sio wangu.
Naomba kwa anaejua gharama na taratibu za kupima DNA anijulishe mana hili swala ni gumu sana kwangu. Ikiwa gharama ni rafiki basi nikapime.
Asante
Hawapimi Hospital.....!Mkuu kama gharama ni 150k naweza kupambna kidogo kidogo nkaipata niko Moro mjini inamana wanapima hospital za kawaida au kuna hospital maalum nsaidie kwa hilo kama unajua pia.
Achaa kuongopa,Mungu hajamleta huyo mtoto kwa jamaa, ni mwanamke ndiyo kamleta huyo mtoto kwa jamaa! Tuwe wakweli, Jamaa ana haki ya kujua kama kweli huyo ni mtoto wake au laa, maana kuna Baba mwingine nae katajwa kwa huyo mtoto!!Gharama ya DNA ni Wastani wa 150,000.....!
All in all kila kinachotokea Kwa Binadamu kina sababu.
Ipo sababu Kwa Nini umeachana na huyo Mwanamke.....!
Pia ipo sababu Kwa Nini umeletewa huyo Mtoto na Mungu ili Umtunze...!
Yani nishatumia gharama kumlea ikiwa sio wangu huoni haja ya mimi kulipwa, mana ukiachilia mbali matumiz ya kila siku nlishlipa sh. Laki tatu ya makosa ya kumpa mimba binti yao yan kuna mambo mengi ata kuandika nakosa nguvuNaunga mkono. Yaani unapunguziwa mzigo unakataa
Umeongea poa sana yanHapana hii italeta mtafaruku mkubwa mbeleni..Vipi huyo jamaa anayetajwa ni baba wa mtoto akaja kumchukua mtoto wake na wewe umegharamia kila kitu.
Ni bora kuziba ufa mapema kuliko kuendelea kuumia na maumivu maana huyo mwanamke atamletea maumivu yasiyokoma.
Wanawake wapo wengi atampata atakayemfaa atamzalia. Wanawake wapuuzi sana.
NB; HAKUNA MWANAUME ANAYEPENDA DAMU YAKE ITESEKE, ILA WANAWAKE NDIO SABABISHI WANAUME KUONDOKA NA KUWAACHA.
Da nimekusoma mkuu ila nlishapigwaga na faini ya kumpa mimba binti yao sh laki tatu hiyo ni nje na matumiz ivi vitu vinaniumiza akili sana bas tu ndoivo maisha yenyew magumu tuHuwa naskia kuwa DNA inapimwa kwa amri ya mahakama..... Yani mnakubaliana mama na baba then mnaenda mahakamani hakimu anatoa vielelezo ambavyo dktr ndo anapata ruhusa ya kupima DNA ili kuondoa mgogoro apo hospitalin... Niliskiag Huu utaratb ila Sina hakika nao sana....
Nakushauri mkuu.. kam wanadai mtoto sio wako basi we kausha miaka miwili hesab kam umetoa sadaka tu, sitisha Huduma zote kaa tuliza akili tafuta mwanamk mwngine ila asiwe kutoka mjini ndo wale wale watakuumiza kichwa. Mi ni muhanga wa ishu kam yako ingawa ni tofaut kidg khus mtoto.

NAKAZIAMzee kwanini ujitese kama wamesema mtoto sio wako achana nao wamlee wenyewe ...damu nzito kuliko maji jipange upya utafute mwanamke upate mtoto
KiufupiHuyu mtoto ni wako.
1. Kama adingekuwa wako hangekuachia akaondoka.
2. Alijua utakwama lakini kwa mafanikio makubwa ulipata busara ukamlea kupitia mkweo na mtoto kawa mkubwa. Inamuuma.
3. Mkeo hana tofauti na muuaji, alitegemea mtoto angekushinda kumlea ili umpigie magoti.
4. Huko alikoenda amekwama kila kitu akaona amgeukie mtoto ili akuumize zaidi lakini ulifanya jambo zuri kumkabidhi mtoto kwa mujibu wa taratibu na sheria.
5. Kuna alichokitarajia kwako akaamua kuolewa sasa alikikosa akaamua kumrudia ex wake, hawa wawili lao moja.
6. Fanya ujasusi wa kumhusu ex wake. Fanya utafiti Je ana watoto? Kama anao wangapi? Ajiri mwanamke kijasusi hata ajifanye house girl akawapige picha watoto wake ufanye ulinganisho wa sura zao na huyu mwanao.
7. Ili ujue ni kweli ndiyo sababu ya yeye kukwambia mtoto ni wa ex wake.
8. 99% to 101% mtoto ni wako Kama sivyo mama yake angeliungana naye kwani tangu ujauzito wake wanawake hunong'ona na mama zao ila huyu hakuwai kufanya hivyo kwasababu hakuwa na sababu ya kufanya hivyo. Mtoto ni wako usijiumize nafsi yako.
9. Rudi nyuma kipindi cha mimba changa huyu mkeo alikuwaje? Je alikuwa mtu wa kutokatoka kabla ya kupata ujauzito? Je baada ya kujifungua sababu kuu ya kukuachia mtoto ilikuwa ni ipi. Na Kama ikiwezekana weka hapa chanzo cha mtafaruku hadi akamuacha mtoto sababu kubwa ilikuwa ni ipi.
10. Napenda kukusisitizia kuwa mtoto ni wako ila huyu mkeo anajua kuwa MAPENZI YAKO MAKUBWA NI KWA HUYU MTOTO SASA ILI AKUUMIZE AKAAMUA KUTAMKA HUO UJINGA. Huyu siyo wa kumrudia kamwe atakuua.
Mwisho type marejesho.
NashukuruHawapimi Hospital.....!
Kwa Dar es salaam, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ndo Huwa inapima....!
Office zao zipo jirani na Ocean road.
Kwel kakaAchaa kuongopa,Mungu hajamleta huyo mtoto kwa jamaa, ni mwanamke ndiyo kamleta huyo mtoto kwa jamaa! Tuwe wakweli, Jamaa ana haki ya kujua kama kweli huyo ni mtoto wake au laa, maana kuna Baba mwingine nae katajwa kwa huyo mtoto!!
Daah kwa Scenario Hii Umepigwa Nyumbani na Umepigwa Ugenini, Tena Cleansheet hiiKiufupi
Sikulea mimba ila aliniletea mtoto na kusema ni wangu.
Nlipomuuliza mimba umeleaje pekeako na hukunambia akasema aliolewa na mme mwingine ambae alikataa kuwa mtoto sio wake kwakuwa muda waliokaa inaonekana mimba ilitangulia kabla ya ndoa
Nkamuangalia mtoto nikaona ni kama nafanana nae na mtoto mchanga mi mwanaume siwez kufananisha sana ila nkaanza kumlea tangu hapo.
Nlipokubali kumlea wazaz wake ndo wakaniita kuwa nilipe fidia kwa yule alielea mimba nakuongeza kuwa yule mwanaume anawalaumu kumuozesha mke ambae alikuwa na mimba.
Sikuhoji kitu nkalipa sh laki tatu ambazo nlitakiwa kulipa huku nikiendelea kumlea mtoto.
Sasa mtoto alizaliwa akiwa mikonon mwa uyo mme wake na majina anayotumia clinic ni hayo hayo jina nlilompa linatumika tu kwenye kumuita. Sasa hata kubadili jina kwenye kadi kwa muda wote kuanzia mama yake na bibi yake wote hawakubadili wanasema kubadili jina ni ngumu ( binafsi sielewi)
Sasa badae ndo mapichapicha mara mtoto sio wako mara unajisumbua kulea mtoto sio wako mara mtoto ana kadi tatu uyo we jisumbue tu.
Sasa nikae kimya vip gharama zangu?
Au niache kulea vip ikiwa ni damu yangu afu akawa anateseka, hapo ndo naumia
Yalikoma siku hiyo hiyo ila kila kukicha ananitafuta kwa namba mpya na kero zipo constant. Nshablock namba zaid ya nane na bado atakutafuta tuMawasiliano na huyo Mwanamke yalitakiwa yakatike toka alipokutelekezea mtoto
Nashukuru angalau umefanya nitabasamu, ubaya ubwelaMadaktari wanaopima DNA wameruhusiwa kutoa majibu ya uongo ikiwa ataona inafaa!,hiyo ni kwaajili ya mtoto apate mahitaji yake nakueupusha watoto wa mitaani.
kama utahitaji majibu ya kweli kabisa nafikiri itakubidi utumie fedha zaidi,
Hivyo ndugu kaa ukijua dunia haipo kwaajili ya sisi wanaume, yani dunia kwetu ni ubaya ubwela...![]()
Endelea kupiga block huyo! Kakubambikia mtoto mpumbavu sana huyo mwanamke! Achana nae Dalili za mvua ni Mawingu Sasa kama unataka mvua ya mawe ikunyeshee endelea kuweka mazoea nae!Yalikoma siku hiyo hiyo ila kila kukicha ananitafuta kwa namba mpya na kero zipo constant. Nshablock namba zaid ya nane na bado atakutafuta tu
Du atarDa
Daah kwa Scenario Hii Umepigwa Nyumbani na Umepigwa Ugenini, Tena Cleansheet hii
Pole sana
