Msaada kuezeka nyumba

babuwaloliondo

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
378
174
Wadau,
Ninakibanda changu cha vyumba 4 kimara mwisho, ningependa kujua makadirio ya kuezeka.
 
Kaka humu kuna wataalam utajuzwa tuu.. Ila ni kama M.4 hivi kwa kadilio la chini pia inategemea ni bati gani unatumia mkuu.
 
kuna tofauti kubwa ya bei kutegemea na aina ya unayotaka ie tiles, IT etc. mbao ni kama sawa
 
Wakumwitu;1826073]Kaka humu kuna wataalam utajuzwa tuu..Ila ni kama M.4 hivi kwa kadilio la chini pia inategemea ni bati gani unatumia mkuu.

Mkuu vyumba vinne hicho siyo kibanda ni nyumba kubwa na kuezeka pia kunategea anatumia mbao gani si maswala ya bati tu hapo. Mbao zenye dawa ni gharama zaidi. Na hapo pia inategemea na mchoro wa nyumba /design ya paa ikoje pia. Bila kusahau aina ya fundi unayetaka kumtumia, kama ni watu wenye fani zao au wa mtaani tu wa kuzeka banda. Inaweza kufika hata 20m kutegemea na variables hizo hapo juu.
 
Wadau,
Ninakibanda changu cha vyumba 4 kimara mwisho, ningependa kujua makadirio ya kuezeka.

Umekosa mafundi wa kukufanyia estimate? Sio bure inabidi uwalipe hiyo ni taaluma watafute wataku-charge kama kawaida lakini kama unaamua kwenda solo ni poa vile vile.
 
Umekosa mafundi wa kukufanyia estimate? Sio bure inabidi uwalipe hiyo ni taaluma watafute wataku-charge kama kawaida lakini kama unaamua kwenda solo ni poa vile vile.
nashukuru kwa mchango wako mkuu
Ningependa kujua Basis yakuweza kunegotiate nao, unajua hapa mjini watu wanakula kwa kiasi chao, anaweza kusema kiasi fulani nikakubali, baada ya muda nikakuta nimeliwa, hivyo nauliza ili niweza kujua base ya kunegotiate nae.
 
NA MIMI NAOMBA KUONGEZA SWALI:
nina kibanda au nyumba ina sitting,dining,2 bedrooms.,1 master bed room,garage,kitchen,veranda ya mbele na nyuma.Nataka kuezeka.
Ntatumia bati za kawaida (corrugated iron sheets,za gauge 30).Mbao za kawaida (ntazipaka dawa mwenyewe).Paa nataka yale ya kuchomeka.Naomba kujua estimates za Gharama ya fundi (wa mtaani,mzuri) na idadi ya material needed if possible na bei yake kwa sasa sokoni,ili niweze kujipanga. Nimeatach picha ya paa ninalotaka.fLoor plan pia nimetua hii hii,ila nimeshindwa kui-upload.Natanguliza shukrani.
ROOF PICTURE.jpg
 
nakushauri utumie miti kujenga na kuezeka,mimi niitumia miti ya mirunda,ipo kila mahali in Dar,na huwa ipo treted vizuri sana.
gharama huwa ni chini kuliko mbao zilizokuwa treated.
bati nenda kiwandani ukanunue,
kimsingi andaa around mili 2.5 hadi 3 kukamilisha zoezi
 
Mkuu NM,
Are mirunda aplicable on roofing? Inamaana inatumika badala ya mbao? Haiozi? Uimara wake je?
 
Mkuu NM,
Are mirunda aplicable on roofing? Inamaana inatumika badala ya mbao? Haiozi? Uimara wake je?

Kabla ya kuja usasa wa matumizi ya mbao wengi walikuwa (na wanaendelea) wanatumia miti. Mafundi wazuri wa kuezeka kwa miti huwa wanainyoosha na inakaa sawasawa. Hivi hii mirunda ni ile miti ya pwani kwa jina jengine mikandaa au mikoko? Kama ndiyo basi ni imara sana, haiozi, inadumu zaidi ya miaka 50.
- Wasiwasi wangu ni hiyo quote ya milioni 2 hadi 3. Bati zimepanda bei sana. Usishangae zote ninaishia kwenye bati hata kabla ya kununua miti.
- Wakati wa kununua bati kuwa makini. Rahisi mwishi huwa ghali, nikiwa na maana ya kuwa ununue bati madhubuti (ya geji 28 au 30) ambazo ni ghali lakini ni imara zaidi ya 34 au 36 ambazo ni nyembamba sana lakini rahisi.
- Tafuta ushauri zaidi kwa mtu ambaye ameezeka kwa bati ya kawaida na miti.
 
Kwa huyo anayetaka kuezeka kwa bati za kawaida bei ya fundi haizidi laki tano mpaka sita'nakumbuka nilisimamia ujenzi wa bibi mkubwa vyumba vitano'alipiga mambo za tinted kwa sh laki 9'mabati alinunua 70 haya ya kawaida na mengne kama kumi yalibaki ni pm'nikupe mchakato wote hata ww wa kimara nikutafute mafundi wazuri kwa bei nzuri naish stop ova
 
sisi wengine huwa tunabaki kushangaa kwenye gharama za hawa watu wenye fani zao.
Jamani hivi inakuwaje kwa mfano gharama za vifaa ni X na ufundi unakuwa unakuwa 50% of X.?
Linalonishangaza zaidi ni hawa mafundi wa mitaani ambao wengi wao ni std 7 au max. form 4,hivi kuna ulakini gani ukiwatumia hawa,maana nyumba ya baba yangu alitumia contractors,mimi nimewatumia hawa wa mitaani kuezeka bati za SA,na wametoa kama nilivyotaka,je kuna hatari inanisubiri kama paa kuanguka etc?
Maana wakati wa mabomu nyumba zilizokuwa zikilegea na kuanguka ni za watu wenye certification ya CRB au kuna uchakachuaji?Naomba msamaha kama nimekwaza mtu.
 
Mkuu, nilichogundua ni kwamba hata hawa wenye kampuni zao wanawatumia haohao mafundi wa mitaani. Kazi yao ni kuelekeza tu na wakati mwingine hata hawaelekezi chochote wanachukua tu mafundi na kuwapa michoro na mafundi kama ni wazoefu wanaanza kazi. Wanawalipa ujira kidogo na wao wanabaki na asilimia kubwa ya gharama za ujenzi ndo maana utakuwa wanakupigia hayo mahesabu ya asilimia ya gharama ya material ambayo naona ni wizi kwani muda wa kujenga au ugumu wa kazi hautegemei aina ya material. Labda kwenye paa kuna utofauti wa kuezeka kwa bati na vigae.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom