Msaada:kozi ya computer

Msaada:kozi ya computer

GABOO

Senior Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
118
Reaction score
12
Salaam wanajf,mimi napenda sana macomputer,natamani sana kusomea na kufanya kazi kwenye macomputer,nishaurini kozi nzuri na chuo kizuri naweza somea.nipo Arusha.
 
Elimu yako ni level gani. Na unatakuanza kusoma level gani certificate, diploma, au degree. Interest yako ni ipi hardware maintanance, database na programming, graphics na multimedia etc. ukijibu hayo maswali itakuaa rahisi kukusaidia.
 
inabidi uanzie msingi ili ujue uende wapi.
 
Ukitamka neno "computer" katika teknolojia ya habari na mawasiliano ni kama kutamka neno "maisha" katika sayari hii ya dunia...they are very general terms kiasi kwamba ukishindwa kubainisha haswa nini unataka kusaidiwa mtu atashindwa kukusaidia, cha msingi we tuambie kiwango chako cha elimu cha sasa na eneo gani haswa la "computer" linalokukosha.....je ni computer maintainance, computer programming, computer networking yani sema ni field gani ya computer unayohisi kuihusudu ili wanajukwaa wajue pa kuanzia kukushauri!!
 
Ok,ni hivi mimi nimefika form 4 na kozi inayonikosha ni A+ na graphics and multimedia
 
Gaboo
Kwa Dar es Salaam waweza fika pale Technobase Training College ,Chang'ombe karibu na maduka mawili njia panda ya TCC sigara...kuna wataalam watakufanyia assessment ya career na background yako kabla ya kukushauri kozi inayokufaa....mdogo wangu nilimpeleka pale akiwa na nia ya kusoma computer engineering lakini kumbe Mobile engineering ndiyo iliyomfaa na sasa ndio inayomuweka mjini huku Tandika ...sasa anasomea Video production palepale.
 
nenda JRIIT sakina au UCC ngarenaro,pia ipo KITECH kijenge na Horizon town ila hivi viwili sijui ubora wao sana
 
Ahsanteni sana kwa mawazo yenu,ntayafanyia kazi
 
Back
Top Bottom