Msaada kisima changu kimejaa chura

Tumbukiza samaki uwafuge watakusaidia kula mayai ya vyura hivyo kuwapunguza.
 
Mkuu, huenda hilo shimo/kisima chako umekijenga bila kufuata kanuni zake. Kisima/shimo la maji safi ni muhimu kulifunika ili wadudu wasiingie, ni muhimu pia kuhakikisha mwanga wa jua haupenyezi ili maji yasiharibike haraka(pamoja na kwamba unaweza kuweka dawa).

Hakikisha umefunika hilo shimo/kisima, hakikisha halipitishi mwanga wa jua lakini pia hakikisha unatumia dawa kwa ajili ya kuyatibu maji. Hutapata shida, utayatumia maji yako kwa matumizi yoyote, hata kama ni maji ya mvua.
 
Kabla ya hayo yote atafute vijana watoe maji yote, wamsafishie kisima.
Kama hajakijengea wakijenge kabisa.
 
Huku niliko mvua ikinyesha vyura huwa ni kero kulia Sasa hapo kwako nakuonea huruma aisee.
 
Utaweka kambale wangapi? Naona umeshapata fursa ya kufunga kambale.
Natafuta madume mawili, sichanganyi jinsi maana unaweza solve tatizo la chura ukaweka tatizo la kambale
 
Mtafute mshabiki wa Yanga umuuzie utapata faida kubwa wao sijui wanawapeleka wapi
 
Halafu anawatoa tena au anawaacha?
Yeye mwenyewe ila nao wana kunya na kukojoa pia maji yatakuwa na uchafu maana watahitaji chakula! Kwaiyo njia hii sio Sahihi!
Amwage maji akijengeye! azibe kabisa
 

Mtafute Mchezaji Mmoja au hata Shabiki kama siyo Mwanachama Mmoja Mwandamizi wa Yanga SC watawatoa, kwani wana Uzoefu nao mkubwa.
 
waite yanga/ utopolo waje wawasajili wawapeleke pale jangwani
 
da mkuu utakuwa mtu wa ajabu sana wewe sikuhizi watu hawapendi samaki wanataka chura weweunawaogopa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…