Msaada Kisheria: Nimeibiwa fedha mtandaoni

masalapa

Senior Member
Oct 29, 2012
137
66
Nimekuwa mteja wa mtandao mmoja wa simu hapa nchini kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Licha ya kupata huduma bora katika kipindi chote hicho, hata hivyo hivi karibuni nimekuwa Nikishuhudia wizi wa fedha nilizokuwa nikitunza kama akiba kwenye account yangu ya simu. Yaani unaamka tu asubuhi unataka kutumia sehemu ya fedha hizo unakuta hela takribani yote ilishapigwa!

Ukifuatilia sana unaishia kuombwa tu msamaha na hela kurejeshewa kwa maelezo kuwa wizi huo unasababishwa na wafanyakazi wasio waaminifu! Imefika mahali Nimekosa kabisa imani na huduma zao kwani hii ni ishara kuwa huenda hata taarifa za mawasiliano yangu zikawa hatarini kutokana na uwepo wa wafanyakazi hao wasio waaminifu.

Nawezaje kupata msaada wa kisheria ili hatua stahiki dhidi ya uhuni huu ziweze kuchukuliwa kwa lengo la kukomesha kabisa tatizo hili?

Nitashukuru kwa msaada wenu.
 
Ungewataja kabisa kwa majina hayo Makampuni, Mimi hadi Leo Tigo wananielewa vizuri tu. Tulipekana mwaka mzima hapo TCRA
Tigo sihami ,pale shekilango hawana hamu na mm ,,aisee niliwasha moto wa kutosha ,,
Halfu pia kuna no yangu hiyo ya tgo walikuwa wanaitaka kinguvu sijui kuna tajiri gani alitangaza dau

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
Nikashinda kesi japo kimagumashi hivyo hivuo, I am convinced watu wa TCRA sana Yale "mahusiano mema" na makampuni ya simu hivyo kwa mtu wa kawaaida kushinda kesi ukapata stahiki zako ni ngumu sana. Niliweka evidence zote but nikipata ushindi kiduchu sana.
 
masalapa, Pa kuanzia ni kupiga kimya uwasubiri wajichanganye tena waibe, wakishaiba tu usiwashtue ili warudishe, tafuta wakili kwani ushahidi utakuwepo ili muwashughulikie vizuri, kesi yenye ushahidi dhidi ya mtu au taasisi yenye fedha ni ujasiriamali mzuri tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tigo sihami ,pale shekilango hawana hamu na mm ,,aisee niliwasha moto wa kutosha ,,
Halfu pia kuna no yangu hiyo ya tgo walikuwa wanaitaka kinguvu sijui kuna tajiri gani alitangaza dau

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
Unaweza kuja inbox ili unipe uzoefu Nami Niuwashe huo moto?
 
Back
Top Bottom