Mayu
JF-Expert Member
- May 11, 2010
- 6,699
- 10,795
Wakuu kwema?
Kuanzia mwaka 2012 nilikua nanunua mashamba nje ya mji kidogo kidogo kwa mzee mmoja huko mkoani kwa jumla ya Tsh M3.
Mwaka 2017 watu wote wenye maeneo huko tukaitwa kistaarabu kabisa na kanisa kupitia kwa mkuu wa mkoa na tukaombwa tuliuzie kanisa eneo hilo kwakuwa linataka kufanya uwekezaji mkubwa sana wa chuo kikuu na hospitali
Baada ya majadiliano marefu tukakubali, na kila mmoja akawa anakwenda ofisini kupatana bei na wachungaji/maaskofu na majoho yao.
Binafsi tulipatana sh M38
Tukapewa sh 1M kila kama kishika uchumba na tukaambiwa tusubiri ndani ya mwaka wafadhili watakua wametuma hela na tutamaliziwa hela zetu
Miaka mitatu ikapita kila siku sound tu
Mwaka wa 5 tukabana kwamba tunataka hela zetu na thamani ya viwanja imekua kubwa hivyo watulipe na fidia ya ongezeko la thamani
This time wakaja watu wa serikali, maafisa aridhi
Tukaambiwa itafanyika tathmini upya kupitia maafisa aridhi na wao ndio watatoa tathmini ya bei kulingana na uhalisia
Tukajipa moyo labda tathmini ya wataalamu itakua nzuri kuliko ya awali
Aisee wakanitathminia 12M tu kutoka M38 ya awali na hapo nimekwisha tafuna 1M
Tukakubaliana kugoma na tuka demand kuonana na wachungaji/Maaskofu tuliopatana nao..... utawaona wapi???? Hapo tuna deal na maafisa wa serikali tu sasa
Tukanyooka kwa RC akatusikiliza kisha akatuuliza mnayo mikataba kusapoti madai yenu? Tukatoa macho kama mjusi kabanwa na mlango
Akasema kama hatujaridhika tuende mahakamani
Njaa mbaya kuna wenzetu wakakubali wakaandikiwa mikataba ya tathmini mpya na kupokea malipo yao
Wabishi bado tunakomaa
Tulio komaa ni wale ambao tulinunua maeneo lakini wenyeji wengi wamekubali kupokea hela
kwakuwa hakuna maandishi ya makubaliano ya kuuziana maeneo hivyo tumeamua kwamba hatujakubaliana na kanisa chochote na hatuuzi maeneo yetu la sivyo wakae chini na sisi tupatane bei na sio kunipangia bei. HII IMEKAAJE KISHERIA?
Maana tunatishwa kwamba serikali inauwezo wa kutulazimisha ikiamua kama inavyofanya kwenye upanuzi wa barabara
Mind you that haya ni mashamba tu hayana hati zaidi ya hati za makubaliano ya mauziano za mtendaji wa kijiji
Majoho yametuponza