Historia fupi ya ukadinari na wajibu wake ndani kanisa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Tangu karne za mwanzo wa kanisa, kumekuwa na historia nzuri sana ya kuelezea mwanzo na chimbuko la ukadinari ndani ya kanisa. Askofu wa Roma, ambaye ndiye askofu wa kwanza wa Roma, anachukuliwa kuwa mrithi wa Mtume Petro. Kila askofu wa Roma hukalia kiti cha Petro na kuendeleza uwakili wa Kristo hapa duniani.

Katika karne ya nne, hasa baada ya Edict of Milano mwaka 313, Mfalme Constantine alitangaza uhuru wa kanisa katika kuendesha ibada zake wazi wazi. Hii ilifuatia mateso ya Wakristo kwa karne tatu zilizopita. Mwaka 324, Ukristo ulitangazwa kuwa dini rasmi ya Dola ya Kirumi. Hii ndio mwanzo wa kuwa na muundo wa kanisa. Askofu Mkuu wa Roma akaanza kuwa na wasaidizi katika kuongoza kanisa la ulimwengu ndani ya Dola ya Kirumi.

Tunajua kwamba mwaka 325, Mtaguzo wa Kwanza wa Nisea ulipitisha Kanuni ya Imani na kusahihisha mafundisho potovu ya Arius na wafuasi wake. Washauri wa Askofu wa Roma walichaguliwa kutoka kati ya mapadri au makadinali wa Jimbo la Roma. Kundi la kwanza lilikuwa mashemasi saba, ambao kazi yao ilikuwa kuongoza shughuli za Askofu wa Roma kwa kugawa ruzuku kwa mapadri, kugawa chakula kwa maskini, na kuongoza ibada katika sehemu saba za Jiji la Roma (hawa waliitwa kardinali mashemasi). Idadi yao iliongezeka kadiri karne ya tisa ilivyokuwa ikiendelea, kulingana na mahitaji ya kanisa. Ingawa wanabaki kuitwa kardinali mashemasi, sasa wanawajibu wa kuongoza wizara mbalimbali za Holy See (Decastery). Pia, wanajulikana kama makardinali bora kutokana na kazi na ujuzi wao katika maeneo mbalimbali.

Makardinali Mapadri (kardinali kasisi), chimbuko lao linaanzia karne ya tatu. Ndani ya Jimbo la Roma, kulikuwa na parokia za hadhi ya titulus. Parokia hizi za hadhi zilikuwa na mapadri wao, ambao pia walikuwa sehemu ya baraza la ushauri la Askofu wa Roma. Wajibu wao ulikuwa kutoa sakramenti ya ubatizo katika parokia hizo. Leo hii, parokia hizi zina mapadri wao, lakini kila parokia ina kardinali wake, yaani, kardinali kasisi. Hawa ndio makardinali walioko majimboni, lakini bado ni sehemu ya Jimbo la Roma.

Makardinali Maaskofu, chimbuko lao linatokana na karne za mwanzo za kanisa. Jimbo la Roma linazungukwa na majimbo saba yanayojulikana kama jimbo za Kikatoliki (Suburbicarian Dioceses) kama vile Ostia, Albano, Frascati, Palestrina, Porto, Valletri, na Sabina. Maaskofu wa majimbo haya waliishi ndani ya Jiji la Roma na walimsaidia Askofu wa Roma kuongoza ibada katika kanisa lake la kikaskofu la Laterano kwa siku sita, na siku ya saba, yaani Dominica, Askofu wa Roma mwenyewe aliongoza ibada katika kanisa lake la kikaskofu. Mmoja wao aliongoza ibada ya Dominica ndani ya Kanisa la Mtakatifu Petro. Hawa maaskofu ni washauri wa karibu sana na Baba Mtakatifu, na askofu wa Ostia ndiye kiongozi wa baraza la makardinali. Hadi leo, majimbo haya saba yanabaki kuwa na hadhi yao.

Kwa nini makardinali wanapaswa kushiriki katika conclave? Tangu karne za mwanzo, askofu wa Roma alikuwa anachaguliwa na waamini na mapadri kupitia kura. Katika karne ya kumi ya kanisa, utaratibu huu ulionekana kuwa si mzuri kutokana na vurugu na maslahi binafsi katika uchaguzi, na hasa shida kubwa iliyotokea kati ya mwaka 882 na 1046. Wakati huo kulikuwa na mapapa watatu waliotangaza kila mmoja kuwa Papa halali. Mwaka 1046, katika Sinodi ya Sutri, Mfalme Henry III aliwafukuza mapapa wote na kumteua Papa mpya, na hapa ndipo ulipoanzia mchakato unaoitwa Gregorian Reform. Katika Sinodi ya Laterano mwaka 1059, kanisa rasmi lilianzisha sheria juu ya conclave, yaani uchaguzi wa Papa au Askofu wa Roma ungehusisha makardinali pekee, bila kuweka wajibu wa lazima wa kuwa mapadri wa jimbo la Roma. Hivyo, makardinali wote wanahudumu kama makleri wa Roma, kwa sababu mchakato wa uchaguzi unahusisha askofu wa jimbo la Roma na ukhalifa wa Mtume Petro.

Makardinali wanashiriki katika ushauri wa pamoja (collegiality) ndani ya Baraza la Makardinali, lakini bila kusahau kuwa maamuzi ya mwisho yapo kwa Papa mwenyewe. Wote wanasalia kuwa washauri.
 
Back
Top Bottom