Msaada: Kila nikipata pesa linafata tatizo

Msaada: Kila nikipata pesa linafata tatizo

Unatoa fungu la kumi?Jitahidi uwe unatoa hilo kwani ni ulinzi mkubwa sana wa vitu vyako vyote,hata ktk bilble imeandikwa atamkemea yule alaye ikiwa unatoa hiyo 10%,mimi yalinikuta ila nilishauriwa na nilipofuata ushauri kwa kweli naona sasa hivi naishi kwa raha
 
Simple,usipate pesa sasa!!!!

Hahahaha,aisee JF kweli kuna watu wamepinda.

Hahahah,yaani kama upo makaburini kwenye kuzika halafu ukafungua JF ukasoma,basi unaweza kujikuta unacheka halafu wata wakaona kwama unafurahia marehem kufa.Kumbe wewe umeingia JF na kukuta kituko kama hiki.

Aisee Burudani ndani shida
 
Ongeza speed ya kutafuta pesa.
Inawezekana unapopata pesa akili ya kutatua tatizo ndo inakuja.
 
Tatizo hilo sio lako tu, hata mimi pia.
Kila nikipata hela za madini wanawake wananipapatikia nao ujue wanakuja na matatizo yao ya kufunguliwa salon, maduka ya nguo na Tigo pesa, pesa ikikatika wanapotea kidogo.
Nikizipata tena wananipapatikia tena warembo zaidi, kwa kweli nimewakanyaga sana ila hata kiwanja sina, sijui ni mkosi gani niliokua nao.
Najitahidi sana hata wakati mwingine kuweka hela benki lakini wanawake wa mjini wanajua jinsi ya kunilainisha, mpaka nakwenda kutoa. Pale Mwenge kuna salon tano zimetokea mikononi mwangu na sasa hivi tumebaki kusalimiana tu, sana sana naishia ofa ya konyagi.
Safari hii nikizifuma tu naoa na kununua kiwanja Mabwepande labda huko hakuna wanawake wenye ushawishi kama Sinza.
 
Hata mie nina hilo tatizo,ila cha kufanya hapo naona ni kumrudia Mungu na kutoa sadaka na zaka itakuwa suluhu la matatizo.
 
Nina bahati ya kupata hela,kila nikizipata linafata tatizo sijawahi fanya kitu cha maana.

Msaada tafadhali

Kitu cha maana gani zaidi ya kutatulia matatizo? Pesa kazi yake kutatulia matatizo! Afadhali yako matatizo yanasubiri uwe na uwezo wa kuyatatua ndio yanakuja, mimi yanakuja tu na hata kama sina hela. Mshukuru Mungu tu...
 
Mungu aweza yote
 
Ukweli uko hivi binadamu tunamatatizo mengi sana zaidi yabhaya ambayo tunayaona wewe leo hii ukipata hata milion 100 hazitoshi kwasababu matatizo uliyonayo nimengi sana kuliko hiyo pesa na mtu ukiwa na pesa matatizo ndio yanaanza kuonekana kuibiwa kufiwa na kwa life la kibongo kwenye familia yenu ukiwa na pesa wewe halafu famili yenu wote maskini mtu akifa wanajua ni wewe tu umemchukua jini

Na watu wengi hawajui kazi ya pesa ni nini kazi ta pesa inabidi ikusaidie kwenye matatizo inamaana ukiwa na hela harafu tatizo likakukuta ukalitatua kwa kutumia hela ujue hiyo ndio kazi ya pesa na matatizo hayana mwisho ila sema inabidi uwe na akili ya kujiongeza ili kipato chako kiongezeke na matatizo yanavyo kukuta hizo tunaita changamoto kwamba usilizike na kipato unacho kipata kwasabu umri unavyo zidi kwenda majukumu yanazidi kuongezeka kwahiyo inabidi na kipato chako kiongezeke hayo yote wanayo kushauri kuhusu makanisani ni uongo hao nao wanataka pesa.
Ukifika kanisani itabidi umtolee mchungaji sadaka ili akuombee inamaana hapo anakua amekuongezea tatizo.
 
Ni wengi....wenye shida kama hizo...hayo matatizo hujafafanua lakini binafs naona kama mm ilivokuwa inanitokea..cha muhimu weka plan...kama unategemea mshahara au pia pesa deal nje ya mshahara list down vitu unavotka kununua kwa maendeleo yako mfano kiwanja, vitu vya ndani, ada, msaada wa familia nk...mara ukishika pesa zako haraka work na list yako funga masikio na ishu za extended family au close family..nilkuwa bwana huruma sana ktk maisha na familia...nilkuja anguka kipind fulani wote nilkuwa nawasadia ktk matatizo kumbe sio wa msaada ni formula yao kuwa na matatizo ili yasovie....pia kama labda unataka kujenga au kununua kitu cha thamani tumia utaratibu...wa kubandika.au elewana a duka la vifaa vya ujenzi jiaminishe hapo then chukua kama ni sement kwa mali kauli ili ukipata pesa utakumbuka kulipa deni bila kujali matatizo yalijttokeza...pili acha mpango wa kushea ishu zzako za pesa....na watu pesa ni siri yako.....utafanya mengi...!! japo ujaweka wazi matatizo yako ni yepi lkn kwa kawaida nadhani ugonjwa ktk familia, ndugu kukamatwaa polisi...maafa km nyumba kuezuliwa na kimbunga...msiba nk..yote haya yakitokea yaache mfumo ufanye mambo yake.....km ni msiba usiwe ndio peke yako eti natoa gari, oooh ntakodi costa.....oooh ntasafirisha ndugu kuja kuzika....kumbuka mwisho wa siku utabaki peke yako na watoto wako au na mke wako....binafsi nimeona sana watu bahiri wagumu kuchangia au kushugulikia matatizo ya watu ndio wenye maendeleo makubwa sisi wengine mnaishia kuitwa mtu mwema........! wemaa hauna sifa kaka....mm nimejifunfza...

mkuu umeeleweka sana..hii haina haja hata ya kwenda huko makanisani!! Huruma ikizidi ni tatizo, kila kitu unaangushiwa wewe!!
 
Tatizo hilo sio lako tu, hata mimi pia.
Kila nikipata hela za madini wanawake wananipapatikia nao ujue wanakuja na matatizo yao ya kufunguliwa salon, maduka ya nguo na Tigo pesa, pesa ikikatika wanapotea kidogo.
Nikizipata tena wananipapatikia tena warembo zaidi, kwa kweli nimewakanyaga sana ila hata kiwanja sina, sijui ni mkosi gani niliokua nao.
Najitahidi sana hata wakati mwingine kuweka hela benki lakini wanawake wa mjini wanajua jinsi ya kunilainisha, mpaka nakwenda kutoa. Pale Mwenge kuna salon tano zimetokea mikononi mwangu na sasa hivi tumebaki kusalimiana tu, sana sana naishia ofa ya konyagi.
Safari hii nikizifuma tu naoa na kununua kiwanja Mabwepande labda huko hakuna wanawake wenye ushawishi kama Sinza.

Duh!!!!!!!
 
nenda kwa walokole ukaombewe tatizo litaisha, hiyo ni roho ya ufukara inakufuatilia.

Mbona hayo maisha ya kilokole ndo yanaongoza kwa kuwa na waumini wengi wa hali ya chini na walojaa stress mpaka akili zao zimejifunga???
Bro ushaur wangu jiombee mwnywe na kusudia kuacha maaasi
 
Hahahaha,aisee JF kweli kuna watu wamepinda.
Y
Hahahah,yaani kama upo makaburini kwenye pkuzika halafu ukafungua JF ukasoma,basi unaweza kujikuta unacheka halafu wata wakaona kwama unafurahia marehem kufa.Kumbe wewe umeingia JF na kukuta kituko kama hiki.
Aisee Burudani ndani shida

Marehem kufa?
 
ehh Mungu nirehemu... fedha sina na matatizo yananiandama. Ebenezer nyoosha mkono wako baba ukaninusuru na tatizo hili lilipo mbele yangu.
Baba umesema Tazama Mimi ni Mungu mwenye nguvu Je kuna jambo lolote nisilo liweza? Mungu wangu wewe ni mkubwa Sana kuliko tatizo langu, ehh baba Naomba ukaniokoe kwa mkono wako ulio hodari. Ukaniokoe Kama ulivyo waokoa wana wa Israel kutoka Egypt hadi nchi ya ahadi. Ukaniokoe Kama ulivyowaokoa Abednego, Shadrach na Meshach.
Mungu Asante kwa Wema wako, na Jua hutoniacha wala kunipungukia. Amen
 
Nina bahati ya kupata hela,kila nikizipata linafata tatizo sijawahi fanya kitu cha maana.

Msaada tafadhali

mkuu, sio wewe tu, hata mm hilo tatizo linanisumbua sana. ngoja wataalamu waje watuambie inakuwaje maana hata mimi nimeshindwa kuendelea kwa sababu hiyo.
 
Nina bahati ya kupata hela,kila nikizipata linafata tatizo sijawahi fanya kitu cha maana.

Msaada tafadhali

Hivi kwako pesa ni ya nini? Pesa kwa ajiki ya kukutatulia matatizo ndiyo matumizi haswa ya pesa! Imagine unapatwa na matatizo afu huna hiyo pesa utafanyaje...? Kikubwa usiendekeze matatizo uwe mvumilivu siyo kila ndugu anakusanya matatizo yao au ata kama ni matatizo yako mengine yapuuze uendelee na programs zako.
 
Nina bahati ya kupata hela,kila nikizipata linafata tatizo sijawahi fanya kitu cha maana.

Msaada tafadhali

Shukuru Mungu una Bahati ya kupata pesa, matatizo ni sehemu ya ubinadamu; cha msingi muombe Mungu zaidi akuongezee pesa na akupunguzie matatizo!
 
Dini imeharibu sana sisi waafrica hatufikiri tena kila kitu sasa kujipa majibu rahisi rahisi tuu na kujifariji kwa kusema ahhh ni mipango ya mungu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom