Msaada: Kila nikipata pesa linafata tatizo

Msaada: Kila nikipata pesa linafata tatizo

Hiyo ni inshu ndogo inawezekana kuna roho ya kifungo inakufatilia pia roho ya kutokustawi,ushauri wangu ni kwmba kama hujaokoka tafuta kanisa la kiroho lililokaribu ukaongozwe sala ya toba uokoke na baada ya hapo ukishafunguliwa kila ukipata hela kwnye mapato yako katoe fungu la kumi (10%) ya mapato yako yote unayopataga,hiyo itasaidia pia kufungua baraka zako nyingi na pia kuiwekea ulinzi fedha yako iliyobakia na matatizo hayatakupata mara kwa mara
N.B usipookoka hata uwe unalala kanisani au unaombewa kila siku kamwe matatzo hayataisha kukuandama.

Sikubaliani Na hilo
 
Naomba kupingana na wote waliotoa ushauri kuwa aendw kwenye makanisa ya kilokole/kiroho.

1. Issue ya kiimani inahitaji imani hasa, iwapo akienda na hana imani ni kazi bure.

2. Kwa imani yake aliyonayo kwa Mungu iwe ni Mkristo au Mwislam, kwanza aanze kujitathimini mwenyewe je ana uhusiano mzuri na Mungu wake? Mf. Je anatoa sehemu ya kumi ya mapato yake katika dhehebu lake? (nina imani wakristo na waislamu huwa tuna hii ibada) iwapo hatoa basi asali na kuomba msamaha kwa kutotoa hiyo sadaka /zaka.

3. Kama kuna matendo mabaya aliwahi kuwafanyia watu kama vile kudhulumu au njia anayotumia kupata hizo pesa sio halali hakika hazitadumu ndio sababu zinaondoka kupitia matatizo.

4. Kama ulikuwa huwasaidii wahitaji anza leo, ila angalia kuna matapeli wengi katika hili

Mwisho sali/omba Mungu akuondolee hilo pepo la matatizo baada ya kujitathimini. Usiamini katika kwenda kuombewa kwani huko wanatoza fedha kwa ajili ya kufunguliwa n.k.

Ni mtazamo wangu CL...

Nakuunga mkono asilimia mia moja.
 
Makanisa ya kwenda ni Roman Catholic church au Anglican church (CPT) au KKKT, ya kiroho ni ya wahuni walioasi kwenye makanisa halali. Yaani usiende kwenye kanisa ambalo kiongozi wake ni mtu wa kawaida tu aliyemjasiriamali wa kupiga hela za watu na wake zao. Utakuta mchungaji/nabii/mtume hajasomea mahali popote ila atakuambia anafufua watu wakati hata kuku hajawahi kufufua.

Kwa imani yako mwenyewe muombe MUNGU kwani hata wewe anakusikia tena vizuri tu ukiwa chumbani kwako. Ila jumapili hudhuria kwenye ibada kwenye makanisa tajwa hapo juu.

Kweli mkuu!.
 
Nina bahati ya kupata hela,kila nikizipata linafata tatizo sijawahi fanya kitu cha maana.

Msaada tafadhali

Mkuu kuna wakati matatizo hayaongezeki, ila wewe binafsi unaongeza wajibu, ukidhani kila tatizo linalofika mbele yako waweza litatua. Mfano ukiwa huna pesa ukasikia ndugu fulani kashindwa kwenda shule kwa sababu ya kukosekana ada, inaweza isiwe tatizo. Lakini ukiwa na pesa, ukasikia hiyo taarifa unaweza ukapatwa na bwana huruma na kutaka kusaidia.
 
Nina bahati ya kupata hela,kila nikizipata linafata tatizo sijawahi fanya kitu cha maana.

Msaada tafadhali


Jaribu kuangalia mahusiano yako na Mungu, wazazi, familia, na Jamii yenye uhitaji....nisome kwenye mada za kiroho 'kuna vitu sio vyetu'
 
Habari wana jamvi hilo ni tatizo la watu wengi na wengi huwa hawajui tatizo ni nini hayo ni mambo ya kiroho kama wewe ni mkristo hakikisha sehemu ya kumi ya pato lako unapeleka kanisani kama ni mfanyakazi sehemu ya kumi ya gross salary yako peleka kanisani hapo mapato yako yatakuwa salama au hata kama ni muislamu hii ya zaka na kwenu ipo uliza mashehe watakuelekeza,kwa wakristo mistari y hilo agizo ni hii hapa:
Malaki 3:7-18
Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.
12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
13 Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani?
14 Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi?
15 Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.
16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake.
17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.
18 Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.

Pia kwanini hatufanikiwi katika biashara au kazi zetu?mistari hii inajibu hayo
Hagai 1:5-11

5 Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
6 Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka.
7 Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
8 Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana.
9 Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake.
10 Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake.
11 Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono.
 
Dawa ni kumchagua Lowassa ambaye amesema atafuta umasikini!
 
Pia angalia mwanamke unaetembea nae. Kuna wanawake wenye mikosi. sijui ni kwanini lakini hili halina ubishi. Palikua na mwanamke pale Forest bar Mbezi kwa Msuguri, hakika ukitembea nae siku inayofuata unafukuzwa kazi, kama ni mfanya biashara ujue biashara imekufa kwani nuksi utakayoipata hataingia mteja dukani kwako zaidi ya TRA kuja kukagua.

Ushahidi upo anaetaka kujaribu anakaribishwa.
 
Jibu langu kwa ufupi ni kwamba unaishi kwenye low/negative energy au frequency au vibration, ndio maana unavuta kwako mambo hasi inaweza ikawa sio hilo tu la pesa kukimbia kila unapozipata bali hata maisha yako yapo yapo tu. Nini cha kufanya?. Tune inn High frequency/vibration/energy. Utafanya nini ili uwe kwenye High frequency/energy? Hapa ndio msingi wa dini zote duniani upo. kwa ufupi badili maisha yako kama ifuatavyo si lazima uende kanisani.

  • Acha Pombe au kunywa kidogo sana
  • Punguza sana ufanyaji wa Ngono hasa ngono holela
  • Fanya Meditation angalau mara mbili kwa siku
  • Usiwe mlafi kwa maana ya kula mpaka unavimbiwa, na pia punguza Nyama, mafuta, Chumvi, Sukari katika mlo wako
  • Fanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki
  • Ongeza upendo katika maisha yako mpende kila mtu hata waliokukosea ni mhimu sana hili.
  • Badili jinsi unavyo fikiri badala ya kufikiri kila saa mambo mabaya anza kufikilia ushindi hata pale penye shida jipe moyo (IMANI/FAITH)
  • Punguza mda unao tumia kungalia TV,
  • Kama upo karibu na sehem ina msitu au miti Mingi jitahidi uwe unaenda kutembea huku ukiwa ume relax au kukaa tu na kutulia ni tiba nzuri. Miti haina negative energy kwa sababu haina mawazo. kwa hiyo utachota kutoka huko positive energy za kutosha
  • Nyumbani kwako hakikisha ni kusafi na huna takataka ndani (hii ni pamoja na nguo/vitu vya zamani ambavyo hutumii tupa vinakuletea negative energy nyingi sana bila wewe kujua.


Wenye kujua zaidi tafadhali mje hapa tusaidiane
 
1. Soma neno la Mungu (Biblia
)ili uujue wwajibuna haki zako kama
MMwanadamu
2.UWE na muda wa sala, maombi .
3. Upate muda wa kutafakari mambo
Yako yote na uyapange katika mfumo
Chanya.
4.samehe waliokukosea,tengeneza nia
Njema ndani yako,uwe na amani na
Furaha,uwe na moyo wa shukrani.
5.usiwe mtu wa maovu.
 
Nenda kwenye makanisa ya walokole yenye nguvu za Mungu wakuombee na upate ukombozi(deliverance)
 
Ni wengi....wenye shida kama hizo...hayo matatizo hujafafanua lakini binafs naona kama mm ilivokuwa inanitokea..cha muhimu weka plan...kama unategemea mshahara au pia pesa deal nje ya mshahara list down vitu unavotka kununua kwa maendeleo yako mfano kiwanja, vitu vya ndani, ada, msaada wa familia nk...mara ukishika pesa zako haraka work na list yako funga masikio na ishu za extended family au close family..nilkuwa bwana huruma sana ktk maisha na familia...nilkuja anguka kipind fulani wote nilkuwa nawasadia ktk matatizo kumbe sio wa msaada ni formula yao kuwa na matatizo ili yasovie....pia kama labda unataka kujenga au kununua kitu cha thamani tumia utaratibu...wa kubandika.au elewana a duka la vifaa vya ujenzi jiaminishe hapo then chukua kama ni sement kwa mali kauli ili ukipata pesa utakumbuka kulipa deni bila kujali matatizo yalijttokeza...pili acha mpango wa kushea ishu zzako za pesa....na watu pesa ni siri yako.....utafanya mengi...!! japo ujaweka wazi matatizo yako ni yepi lkn kwa kawaida nadhani ugonjwa ktk familia, ndugu kukamatwaa polisi...maafa km nyumba kuezuliwa na kimbunga...msiba nk..yote haya yakitokea yaache mfumo ufanye mambo yake.....km ni msiba usiwe ndio peke yako eti natoa gari, oooh ntakodi costa.....oooh ntasafirisha ndugu kuja kuzika....kumbuka mwisho wa siku utabaki peke yako na watoto wako au na mke wako....binafsi nimeona sana watu bahiri wagumu kuchangia au kushugulikia matatizo ya watu ndio wenye maendeleo makubwa sisi wengine mnaishia kuitwa mtu mwema........! wemaa hauna sifa kaka....mm nimejifunfza...
 
Nina bahati ya kupata hela,kila nikizipata linafata tatizo sijawahi fanya kitu cha maana.

Msaada tafadhali


Tatizo la mwanzo sio hilo unaloliona.Ila tatizo la Mwanzo ni wewe mwenyewe ndio tatizo.
Na kama pesa ingekuwa inasema basi Pesa yenyewe ingesema hivi
"Mie pesa Kila nikipatikana kwa huyu mtu anaeitwa washeby basi napata shida sana katika kutumiwa vibaya"

Hapo tatizo sio tatizo ila ila tatizo ndio limeoleta tatizo.

Binaadam yoyote alieumbwa na Mungu basi akipata pesa lazima tatizo litokee,haijalishi kwamba litakuwa kwenye kiwango hicho cha kipato au chini yake.Ila kila tatizo sio kwamba ni tatizo ambalo linahitaji pesa.na hapo ndio tunakwama wengi.
Matatizo mengine unayapeleka kimperampera na yanakaa yenyewe.We umeona mtu anaumwa homa hana pesa?sasa subiri upate pesa hata buku kumi tu,ndio utasikia vihoma vya ajabuu,vibaridi uchwara,balaa tupu,halafu mie kipindi hicho kwangu ilikuwa vihoma vikija vinataka chipss tuuuu,aisee.Na pesa ikiisha homa hiyoo inasepa naanza kurudia kwenye maharage yangu na Ugali.

Mie ningekushauri kwamba usitafute mchawi,ila tambua tatizo liko kwako.Kwa kuamini kwamba Pesa ndio kila kitu na pesa inatatua kila kitu.Mtu hafilisiki kwa kula,ila anafilisika kwa matumizi yasio ya lazima ambapo sie kama binaadam huwa tunayafanya kuwa ya Lazima na tumejizoesha hivyo.
Na kwa sie Vijana wengi ni kwamba tuna kauli ya pesa ya soda,au pesa yenyewe pesa mbuzi nitaifanyia nini.Unaweza kukuta mtu kapata Elfu 50,basi atakuambia hivi hii itafanya nini si niilambe tu.Sasa hayo yataku wamaisha yako hadi unakufa.We nenda kaone Mamalishe wanavyokuzuungushia mtaji wa Elfu 30 tu.Halafu wanasomesha watoto hadi Chuo kikuu
Zingatia haya:-
-Acha kuiga Maisha
-Heshim pesa hata kama mia
-Sio kila tatizo linatatuliwa kwa pesa
-Lazima uwe na malengo ya level yako kimaisha,sio kuwa na ndoto za milioni kumi wakati hata mia huna.Anza na ndoto yako ndogo na jaribu kujifunza kupitia wenzia walioanza na laki moja au mbili.Utajifunza mengi,hata huyo unaemuonaa ana nyingi alianza na moja,ila wewe umekuta nakuona kwamba aliibuka tu kamauyoga.
-Ukiamka nakuomba usianze Kuangalia JF Jukwaa la Siasa,utapotea,tuachie huku sie tuvurage,wewe anzia jukwaa la Wajasiriamali,kule kuna miradi ya kufa mtu,watu wanavichwa vya ajabu huko.Wewe na pesa yako tu,kuna Miradi ya kuanzi elf 50, mpaka Bilions.Na unaweza kushangaa kwamba kuna miradi ya pesa ndogo inaingiza Faida kubwa kuliko miradi ya pesa nyingi.
Sasa nakushauri tembelea Jukwaa la JF wajasiriamali,utajifunza mengi na utakutana na waliokatatamaa kuliko wewe,sasa hii itakufariji kuona kwamba haupo peke yako katika hali hii na utapata njia Zaidi huko.

Narejea,kwa hali uliyonayo,usiingie kwenye JF Kukwaa la Siasa,Nenda JF wajasiriamali Forum.
JF Wajasiramali kuna watu wamo huko na hawana muda kabisaa wa kupoteza kwene Jukwaa letu la habari za Siasa za kusubiria nchi ya kusadik,wao miradi na pesa kwenda mbele.Ni Jukwaa ambalo mie huanza kuingia kila siku then ndio naenda kenye Porojo zetu za siasa kuvuragana ila kwa Amani tu.Ila kama unaanza maisha Jukwaa la Siasa sio salama kwako(Ni mtizamo wangu tu)

Mwisho,tatizo lako wa kuliweza ni wewe mwenyewe kukubali mabadiliko na kuondoa fikra za zamani.La sivyo utaishia kwa Waganga wakati Mganga mkuu ni Mungu aliehai ambae husikiliza kila Anaemuomba na kumtekeleza kwa kuangalia uchamungu wake.

Dalili Njema kwako ambayo namuomba Mungu akufunue na akupe wepesi (Ameen):
Ni kwamba ukioona mtu amejitambua na kuwa muwazi namna hii,basi jua ndio njia ya mafanikio inakuja.Mungu akubariki sana kwa kujitambua nakujua tatizo lako.Endelea kumuomba sana Mungu,shetani siku zote huifuata pesa ilipo ili akupoteze.
 
Naomba kupingana na wote waliotoa ushauri kuwa aendw kwenye makanisa ya kilokole/kiroho.

1. Issue ya kiimani inahitaji imani hasa, iwapo akienda na hana imani ni kazi bure.

2. Kwa imani yake aliyonayo kwa Mungu iwe ni Mkristo au Mwislam, kwanza aanze kujitathimini mwenyewe je ana uhusiano mzuri na Mungu wake? Mf. Je anatoa sehemu ya kumi ya mapato yake katika dhehebu lake? (nina imani wakristo na waislamu huwa tuna hii ibada) iwapo hatoa basi asali na kuomba msamaha kwa kutotoa hiyo sadaka /zaka.

3. Kama kuna matendo mabaya aliwahi kuwafanyia watu kama vile kudhulumu au njia anayotumia kupata hizo pesa sio halali hakika hazitadumu ndio sababu zinaondoka kupitia matatizo.

4. Kama ulikuwa huwasaidii wahitaji anza leo, ila angalia kuna matapeli wengi katika hili

Mwisho sali/omba Mungu akuondolee hilo pepo la matatizo baada ya kujitathimini. Usiamini katika kwenda kuombewa kwani huko wanatoza fedha kwa ajili ya kufunguliwa n.k.

Ni mtazamo wangu CL...

Asante sana kwa mawazo. Naongezea pia umuhimu wa kuwa na "financial discipline" yaani nidhamu ya kipesa. Hili ni tatizo kubwa kwa watu wengi hata taasisi. Nidhamu hii ina maana kupnga mipango yako na kupanga bajeti utakayoitekeleza kutumia pesa unazo pata. Hili ni tatizo kubwa hata kwa serikali yetu.

Inabidi upange mipango na bajeti yake halafu uhakikishe unatumia kufuata bajeti hata kama unapata vishawishi vya kutoifata.
 
Umemaliza mama.
Ajiwekee hazina mbinguni.
Yaani atoe sadaka mara moja tu kwa nia aone matoke yake.
Naomba kupingana na wote waliotoa ushauri kuwa aendw kwenye makanisa ya kilokole/kiroho.

1. Issue ya kiimani inahitaji imani hasa, iwapo akienda na hana imani ni kazi bure.

2. Kwa imani yake aliyonayo kwa Mungu iwe ni Mkristo au Mwislam, kwanza aanze kujitathimini mwenyewe je ana uhusiano mzuri na Mungu wake? Mf. Je anatoa sehemu ya kumi ya mapato yake katika dhehebu lake? (nina imani wakristo na waislamu huwa tuna hii ibada) iwapo hatoa basi asali na kuomba msamaha kwa kutotoa hiyo sadaka /zaka.

3. Kama kuna matendo mabaya aliwahi kuwafanyia watu kama vile kudhulumu au njia anayotumia kupata hizo pesa sio halali hakika hazitadumu ndio sababu zinaondoka kupitia matatizo.

4. Kama ulikuwa huwasaidii wahitaji anza leo, ila angalia kuna matapeli wengi katika hili

Mwisho sali/omba Mungu akuondolee hilo pepo la matatizo baada ya kujitathimini. Usiamini katika kwenda kuombewa kwani huko wanatoza fedha kwa ajili ya kufunguliwa n.k.

Ni mtazamo wangu CL...
 
Nina bahati ya kupata hela,kila nikizipata linafata tatizo sijawahi fanya kitu cha maana.

Msaada tafadhali


Bora wewe Mi kila nikipata hela zinaishia kwenye pombe naweza malizia laki mbili baa kwa siku moja na kesho naamka sina hata hela ya supu...
 
Bora wewe Mi kila nikipata hela zinaishia kwenye pombe naweza malizia laki mbili baa kwa siku moja na kesho naamka sina hata hela ya supu...

Hahahaha,aisee nimecheka mpaka basi,maana kuna jamaa yangu yeye huuza hadi vitu vya ndani,siku akipata hela ananunua tena furniture mpya,akikosa pesa ya pombe anauza tena.Tunamuita Mobile show room

Sio ya kucheka ila Mungu akupe wepesi na akupe njia ya namna ya kuacha Pombe.

Na kinachoponza wengi kwenye pombe ni hizi Kampani hizi.Yaani unafanya kama mazoe yaani bila kwenda sehem fulani basi siku yako haijawa siku.Na unakuta sasa kuna wengine kipato chao ni kikubwa katika kampani yenu.Sasa wale wenye kipato kidogo ndio wanaumia sana kimaisha.Maana wanaishia maisha yao katika level hiyo hiyo huku umri ukiwa hausubirii wewe uache kupombeka,Umri unaenda tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom