Tatizo hilo sio lako tu, hata mimi pia.
Kila nikipata hela za madini wanawake wananipapatikia nao ujue wanakuja na matatizo yao ya kufunguliwa salon, maduka ya nguo na Tigo pesa, pesa ikikatika wanapotea kidogo.
Nikizipata tena wananipapatikia tena warembo zaidi, kwa kweli nimewakanyaga sana ila hata kiwanja sina, sijui ni mkosi gani niliokua nao.
Najitahidi sana hata wakati mwingine kuweka hela benki lakini wanawake wa mjini wanajua jinsi ya kunilainisha, mpaka nakwenda kutoa. Pale Mwenge kuna salon tano zimetokea mikononi mwangu na sasa hivi tumebaki kusalimiana tu, sana sana naishia ofa ya konyagi.
Safari hii nikizifuma tu naoa na kununua kiwanja Mabwepande labda huko hakuna wanawake wenye ushawishi kama Sinza.