sundoka
JF-Expert Member
- Oct 9, 2011
- 2,067
- 2,753
Habari wanajamvi?
Mke wangu amekuwa anasumbuliwa sana na kuwashwa sehem zake za siri, na kuna kipindi ilifikia akawa anatoa uchafu mweupe una harufu mbaya. Baada ya kufatilia ikaonekana ni fangasi.
Nikamtafutia dawa za asili akawa amepona. Ila kila akipona akikutana na mimi kimwili basi anaanza tena kuwashwa. Yaani ule ugonjwa unamrudia tena.
Wiki mbili zilizopita nilimpeleka hospital ambapo walimpatia dawa za vidonge za kupachika ndani kwenye uke. Baada ya kutumia zile dawa kwa siku 6 akawa amepona. Tumepitisha kama siku 4 hatujakutana kimwili baada ya kumaliza dawa na alikuwa sawa. Ila baada ya juzi kukutana nae kimwili ameanza tena kuwashwa vile vile kama mwanzo.
Mimi nilipima Ghono, sina na sina mahusiano mengine nje ya ndoa yangu. UTI sikupima.
Sasa wakuu naomba msaada hapa, naweza miki kuwa na fangasi kwamba namuambukiza? Au fangasi zinaweza kuwa ndani kwenye mbegu za kiume? Maana kwa nje sina dalili zozote za fangasi.
Na je tiba yake itakuwa nini?
Nisaidieni ndugu maana ameniambia anachoka kumeza madawa alafu tukikutana anaumwa tena. Ametishia akitumia dawa tena bila mimi kupata matibabu, hakutani na mimi kimwili.
Natanguliza shukrani.