Msaada: Kila nikikutana na mke wangu anapata fangas

sundoka

JF-Expert Member
Oct 9, 2011
2,067
2,751
Habari wanajamvi?

Mke wangu amekuwa anasumbuliwa sana na kuwashwa sehem zake za siri, na kuna kipindi ilifikia akawa anatoa uchafu mweupe una harufu mbaya. Baada ya kufatilia ikaonekana ni fangasi.

Nikamtafutia dawa za asili akawa amepona. Ila kila akipona akikutana na mimi kimwili basi anaanza tena kuwashwa. Yaani ule ugonjwa unamrudia tena.

Wiki mbili zilizopita nilimpeleka hospital ambapo walimpatia dawa za vidonge za kupachika ndani kwenye uke. Baada ya kutumia zile dawa kwa siku 6 akawa amepona. Tumepitisha kama siku 4 hatujakutana kimwili baada ya kumaliza dawa na alikuwa sawa. Ila baada ya juzi kukutana nae kimwili ameanza tena kuwashwa vile vile kama mwanzo.

Mimi nilipima Ghono, sina na sina mahusiano mengine nje ya ndoa yangu. UTI sikupima.

Sasa wakuu naomba msaada hapa, naweza miki kuwa na fangasi kwamba namuambukiza? Au fangasi zinaweza kuwa ndani kwenye mbegu za kiume? Maana kwa nje sina dalili zozote za fangasi.

Na je tiba yake itakuwa nini?

Nisaidieni ndugu maana ameniambia anachoka kumeza madawa alafu tukikutana anaumwa tena. Ametishia akitumia dawa tena bila mimi kupata matibabu, hakutani na mimi kimwili.

Natanguliza shukrani.
 
Wewe ndio una muambukiza mwenzako na wewe meza dawa maana ka anajitibu na kupona then alikutana it seems unamuambukiza.

pia mwambie awe ana vaa chupi za cotton, na awe anazianika juani na kuzipas kuua bacteria, pia chupi alizokuwa anatumia akiwa anaumwa azitupe au azifue kwa kuloweka na maji Dettol.

Poa gynozol ni kiboko ya hyo kitu pia na wewe jitibu kwanza loh
 
Ebu fanya jaribio hili kama mke wako akipona siku ya kukutana kimwili tumia kinga kwa umakini kabisa (siku 3) alafu uone je bado hilo tatizo analipata kama litatokea bas yeye ndo atakuwa anatatizo kama halitatokea wewe ndo unamatatizo [ila ningependa kujibiwa ili swali akipona huwa mkikutana mara ngap anaanza Kuona izo dalili?]
Siku mbili tu inaanza
 
Wewe ndio una muambukiza mwenzako na wewe meza dawa maana ka anajitibu na kupona then alikutana it seems unamuambukiza, pia mwambie awe ana vaa chupi za cotton, na awe anazianika juani na kuzipas kuua bacteria, pia chupi alizokuwa anatumia akiwa anaumwa azitupe au azifue kwa kuloweka na maji Dettol.
Poa gynozol ni kiboko ya hyo kitu pia na wewe jitibu kwanza loh
Kumuambukiza mwenzangu sikatai, inaweza kuwa sawa. Ninachotaka kujua hayo maambukizi yangu mimi (ugonjwa) yapo ndani? Maana nje kwwnye ngozi sina dalili zozote za fangasi. Na kama maambukizi yapo ndani tiba yake nini?
 
Kumuambukiza mwenzangu sikatai, inaweza kuwa sawa. Ninachotaka kujua hayo maambukizi yangu mimi (ugonjwa) yapo ndani? Maana nje kwwnye ngozi sina dalili zozote za fangasi. Na kama maambukizi yapo ndani tiba yake nini?
Kuna fangas za via vya uzazi na sio ngozi
 
Habari wanajamvi?

Mke wangu amekuwa anasumbuliwa sana na kuwashwa sehem zake za siri, na kuna kipindi ilifikia akawa anatoa uchafu mweupe una harufu mbaya. Baada ya kufatilia ikaonekana ni fangasi...

Sasa si upime izo fungus na kutibu mzee gono ya nn tena
 
Jibu
Hii ni virginal inflammation ( candida) Mkuu hapo tatizo unatibu dalili na sio chanzo, chanzo cha magonjwa ni ulaji wa hybrid foods badala yake ni kula organic foods, kama hupo karibu na mtoa tiba asili anaweza kukusaidia. Kama uzito wake ni mkubwa ajitahidi kupunguza uzito. Kama huko Moshi niweza kukusaidi.
 
Hapa sasa nakuelewa. Vipimo vinafanyika vipi mkuu?
Mkuu huoni kama unahitaji kumuona daktari?? Maana hospital ndio watakwambia wanatakiwa wakupime nini na nini ili kuona watakutibu vipi ikiwa tatizo litaonekana!
 
Kama unazama chunvini inaweza kuwa sababu.

Fanya mapenzi kistaarabu hilo tatizo linaweza kuisha lenyewe... Kumbuka mate ni acid
 
inawezekana pia huwa unatumia mate kama kilainishi..huwa kinasababisha fungus pia...kama si hivyo basi wewe pia una maambukizi.
 
Tatizo limeanza lini mkuu?

Kama lilianza immediately baada ya kuanza kukutana kimwili basi mbegu zako ndo zina shida!!!
 
Back
Top Bottom