Brojust
Member
- Sep 17, 2016
- 60
- 92
Samahani kwa mwandiko mbovu kidogo ila naandika nikiwa nina hasira sana baada ya jamaa yangu kuniletea taarifa nimekosa zaidi ya mil 2 kizembe sana.
Mimi ni kijana wa taaluma ya sheria na biashara, naweza sema nina kipaji maana nimekuwa msaada kwa watu wengi sana, na pia kuna wengine wamekuwa wakifanya mimi kuwa kama daraja kwako, sio kwamba nipo competent hapana ila nina inborn character ambayo naweza fanya jambo lako likafanikiwa tena kiurahisi tena kwa gharama ndogo sana.
Sasa hapa katikati nilifungua ofisi (mpaka leo ipo) maeneo ya Buguruni. Namshukuru Mungu nilianza kwa masihara tu ila baada ya watu kujua huduma zangu nikaanza kuaminika sana (hata na watu wa humu JF).
Shida ni moja, kwa siku za karibuni nimekuwa napata hali isiyo eleweka, naweza kufunga office hata wiki mbili bila sababu yoyote na wala hata simu sipokei, baadae akili inarudi naambiwa yaani watu walikuwa wananitafuta sana na nimekosa hela kabisa.
Mara ya kwanza niliona ni kawaida tu nikaenda kanisani, nikasali lakini labda mniambie nakosea wapi jamani.
Yaani kwa kifupi, huwa na loose kila kitu hadi nauli nakosa, ila nikija ofisini nikianza kufanya kazi ndani ya muda mchache tu hata wiki mbili, kazi zinachangaya napata clients wapya na madili kibao, nikianza ku take off tu sijui kitu gani huwa kinaniingia basi wale wateja wote nawapoteza na hata kuingia madeni fedheha pamoja na kuitwa tapeli.
Yaani hii hali inaniumiza sana sababu baada kama ya wiki moja ndio akili inakuja na nagundua kwamba nina office. Wakati mwingine nachelewesha kazi za watu na mambo mengi kibao.
Juzi tu kulikuwa kazi yaani ya bure kabisa kuna documents fulani hivi kuziandika na kufuatilia vibali kwenye taasisi fulani. Mteja alifika almost 2M sasa huyo jamaa aliyemleta ameniambia alinitafuta karibia siku 4 mpaka kazi akaenda kumpa mtu mwingine. Mimi simu sipokei nimekaa tu sehemu sijielewi ila muda huo nakuwa nakunywa pombe.
Jamani naomba kusaidiwa, mbona nasali sana au sijui kusali? Nina laana? Mbona naomba toba kila siku? Nalogwa (hapa sina uhakika sababu ninasumbuliwa sana na ndoto za ajabu)?
Nifanye nini? Vijana wenzangu wanaendelea mimi nipo pale pale! Nina taaluma, nina office tena ya kwangu, ila maisha yangu hayaeleweki?
Naomba msaada jamani wa kiroho au kimwili.
Mungu awabariki.