mbagokizega
Senior Member
- Oct 22, 2016
- 111
- 297
Habari zenu wataalam.
Nimetembelea jukwaa lenu nikiwa na imani nitapata majibu juu ya hiki nitamanicho kujua.
Ni hivii mi ninamiliki gari ambalo linanisumbua sana na limefanya nigombane na mafundi wengi kwa tabia yao ya kutokuwa na uhakika kwamba ni kifaa kipi kilichoharibika matokeo yake kuniingiza ktk hasara ya kununua kifaa Fulani kumbe gari lina lengine kabisa.Leo nikiwa garage mitaa ya sinza tukakutana watu zaidi ya watatu ambao lalamiko letu lilikuwa ni hili la mafundi wabahatishaji wanavyotutia hasara kwa kutibu kitu kingine kumbe gari lina dosari nyingine matokeo yake kila Siku unaambiwa tatizo jipya.
Ktk maongezi yetu nikamsikia jamaa mmoja akisema kwamba bora aende kwa wachina akatoe elfu 30 akapime gari ambapo kipimo hiko kinaonesha ni kifaa gani kinachosumbua hivyo shughuli ya ukarabati huwa rahisi na ya uhakika.
Ombi langu kwenu wanajukwaa mnisaidie kuniambia kifaa hiki kinaitwaje kwani nimepata wazo la kukinunua na kutumia fursa hii kujiingizia kipato kupitia huduma hii.naomba kujua
Kinaitwaje?
Kinafanyaje kazi?
Kinapatikana kwa gharama gani?
Naweza kukipataje?.
Natumai shaka yangu nimeileta ktk jukwaa husika hivyo ninaamini nitapata majibu ya kuridhisha na hatimaye niweze kufanya uamuzi.
Ahsanteni