Natafuta Garage au mafundi bora wa Bodi na Engine za gari za Kijapani, Mwanza.

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Ndugu zangu habari zenu nyote...

Mimi natafuta garage au mafundi bora kabisa wa bodi kwa ujumla wake kwa maana ya kunyoosha na kupiga rangi upya + engine katika jiji la Mwanza....

Nimepata taabu sana kwenye eneo hili. Kuna wakati nilipelekwa gereji moja na rafiki yangu nmoja. Mafundi wa pale wakajinadi kuwa wao mafundi kweli na wataalamu wa uhakika...

Nikawapa gari yangu na kuelewana waifanyie ukarabati wa kutosha gari yangu I we na mwonekano wa upya...

Tukaelewana kwa gharama ya Tshs. 1,500,000 kazi yote...

Nikatoa advance ya Tshs. 800,000 na nikaambiwa niende kuchukua gari yangu baada ya wiki mbili...

Iliwachukua mwezi mzima kufanya kazi ile tena ktk ubora duni ambao haukunipendeza kabisa maana haulingani na thamani ya fedha niliyotoa...

Tulizozana sana siku nakwenda kuichukua gari yangu kwa sbb hawakufanya kazi ktk viwango tulivyokubaliana. Sikutaka maneno, nilichukua gari yangu na kuondoka....

Toka hapo natafuta mafundi walio serious na kazi yao, gharama nafuu na wanaofanya kazi ktk viwango vinavyokubalika...

Mpaka sasa, gari inataka matengenezo ya bodi na engine. Kama kuna fundi mwaminifu Mwanza, tafadhali tuwasiliane...
 
Garage moja ipo pale veta igogo mkabala na ofisi za bonde la ziwa victoria jirani na ofisi za GPSA.. au mcheki huyu fundi wa hapo 069 274 9814 hawatakuangusha
Asante sana. Nimewasiliana nao. Nitafika kuona, taratibu zao na kazi zao kabla ya kuwapa gari zangu...
 
Back
Top Bottom