Msaada karibu napata presha

Mkuu pole kwa hayo yanakukuta. Kwa kuwa anasema kama umemchoka umwambie tu hapo lazima kuna jambo limejificha na wala usidhani masihara, kuna kitu anajivunia tu na wewe anakuona kwa sasa huwezi kumbabaisha especially kama kuna mtu pembeni na hiyo ni ngumu wewe kujua. Kwa kujihami usijue ndio maana anakujia juu coz ameshajua udhaifu wako kuwa akikupnadishia wewe unaua soo kwa kuwa mpole.

USHAURI MZURI

1. Wewe ndiye uliyemfungulia biashara anayofanya na kupata kipato kizuri tu, pia usafiri umempatia (ana bahati sana ya kupendwa ila hapendeki huyu dada) kwa hiyo hakuna tatizo la wewe kumuogopa, hapo unaibiwa mkuu lazima kuna mtu ana-msugua pembeni bila wewe kujua. Chukua hatua haraka mkuu/ tena faster! Hatua gani sasa ya kuchukua?

2. Mtegee ishu kidogo tu, muulize kwa upoleeee kabisa akikujia juu, we ni mwanume na ndio uliyemuoa hivyo mrudishe kwao kwa mapunziko bila kumwambia lini utamfuata au mwambie rudi nyumbani kwenu na utakapoona umebadilika tabia na kutambua mimi ni mume wako hapo ndipo urudi lakini usirudi kabla ya miezi 6 au 3 hata kama akijua kosa lake!

3. Endapo ukiona amefurahia kurudi kwao na huku anakujibu kwa jeuri basi ujue hapo huna ndoa mkuu lazima ujue kuna mtu anachakachua tu hiyo kitu but ukiona anakuwa mpole ghafla usibadili uamuzi muache aende akajifunze na akirudi kuja kutubu hatarudia tena.

NB: akifurahia kurudi kwao basi ndani ya mwezi 1 utajua nani anasugua huyo mashine na hapo ndo utajua jeuri ya mkeo inatoka wapi.

Pili usimruhusu kuondoka na mtoto, mwambie aende na mtoto amwache home lkn akilazimisha basi muachie mtoto aende nae!

CHUKUA HATUA HARAKA SANA MKUU
SAWEBOY I like your idea
 
Wanawake wengine bwana, watu wanatafuta waume wa kuwauliza tu za kazini hakuna, yeye kapata mume ,kafunguliwa biashara, na bado hata hampi feedback mumewe, lol natamani nimjue nimpe darasa namna ya kuishi na mume mwaminifu kama wewe. Kuwa imara wakati unamuuliza mkazie macho ili akuone una maanisha na hakuna mzaha. Eti sio sie tunataka kujua mume anapata sh ngapi , na vitega uchumi vyote? inakuwaje sie hatutaki kuwajulisha vyetu? Mie hata sielewi kabisa
Kuhusu marafiki vumbi kasema yote na kama humuoni na rafiki basi labda hana marafiki
 
Kama hela kwako si tatizo acha kumuuliza kuhusu hiyo biashara ili mradi mambo ya unyumba akubanii. Kama ulimpa biashara expecting atachangia kupunguza ugumu wa maisha, basi mpe masharti awe ananunua chakula ndani au analipa fee za watoto, make her contribute. Na akianza kuwa na majukumu fixed mbona mwenyewe atatoa feed back kuwa biashara haiendi.

Lstly, kumchunguza ni muhimu, si umesikia siku hizi kuna mashorobaro wanapenda kweli wanawake wanao drive! Tena kuna na serial killer. Watch her movement kama responsible husband!
 
da mkeo mjasilia mali kwan hyo pesa akipata anapeleka wap kaz unayo bro pole sana
 
Muombe sana MUNGU aliekupa Mke ndio huyo huyo atakaemrekebisha, usimwamini mwanadamu
 
Mheshimiwa, ulikosea kwenye msingi sasa hata ukiziba nyufa bado haitasaidi!
Cha kufanya chukua hatua ya kumuweka chini na hata akija juu au akikujibu majibu ya mkato demand ujue ukweli, una haki na wajibu wa kujua ukweli kuhusu mwenzako. kumbuka nyie SIO WAWILI TENA BALI NI MWILI MMOJA, SASA SIRI ZA NINI?
 
pole kaka....Muombe tu Mungu na si kila ushauri hapa una maana pembua kuhusu kumfanyia jeuri sidhani kama itakuwa ni busara sana.....tok to her....asipokusikia mtoe dukani weka kijana akiwa jueri zaidi wahusishe wazazi kumbuka mna mtoto sasa maamuzi mengine huwa ni mabaya kwan huwezi jua nae atareact vipi...take it slowly........Mungu akuongoze.
 
Wanawake wengine bwana, watu wanatafuta waume wa kuwauliza tu za kazini hakuna, yeye kapata mume ,kafunguliwa biashara, na bado hata hampi feedback mumewe, lol natamani nimjue nimpe darasa namna ya kuishi na mume mwaminifu kama wewe. Kuwa imara wakati unamuuliza mkazie macho ili akuone una maanisha na hakuna mzaha. Eti sio sie tunataka kujua mume anapata sh ngapi , na vitega uchumi vyote? inakuwaje sie hatutaki kuwajulisha vyetu? Mie hata sielewi kabisa
Kuhusu marafiki vumbi kasema yote na kama humuoni na rafiki basi labda hana marafiki

PENYE MITI KWELI HAPANA WAJENZI,

Swali la Pauline la mnaishije? ni zito sana,kupitia jibu lako unaweza kupata,
kwa nini huyo mkeo anaanza jeuri ktk kipindi kifupi sana cha ndoa yenu,
pia swali la nyumba kubwa, je uelewa wake ukoje?,nalo ni muhimu sana
Isiwe ni aina ya mwanamke anayechukulia kupendwa kama silaha ya kumnyanyasa mwanaume.

Usitafute nyumba ndogo, bali ongea naye pamoja na watu wenu wa karibu mnaowaheshimu, asipokuelewa mpe muda akapumzike kwao kidogo akiwa huko kama hana mpenzi wa pembeni basi atajirekebisha.

KILA jambo likizidi lina ubaya wake Yawezekana upole wako umezidi kipimo, so yeye anauchukulia ndivyo sivyo kabisa.
Natamani kama ungekuwa wangu.....lol

HONGERA SANA UAMINIFU WAKO,NA ENDELEA KUWA MWAMINIFU NA KUIHESHIMU NDOA YENU, NAAMINI HILO NI WIMBI TU LA KUPITA KUWENI MAKINI,
LISIJEZAMISHA NDOA YENU. POLE SANA, USIPATE PRESSURE ILA HAKIKISHA UNALIPATIA UFUMBUZI HARAKA.
 
Pole sana kaka...Muombe Mungu akupe busara katika hili,tok to her...asiposikia mtoe dukani weka kijana then akiwa jeuri bado washirikishe wazazi....
 
Msamehe tu na unavyosidi kumuignore atajiona mjinga mwenyewe
 
PENYE MITI KWELI HAPANA WAJENZI,

Swali la Pauline la mnaishije? ni zito sana,kupitia jibu lako unaweza kupata,
kwa nini huyo mkeo anaanza jeuri ktk kipindi kifupi sana cha ndoa yenu,
pia swali la nyumba kubwa, je uelewa wake ukoje?,nalo ni muhimu sana
Isiwe ni aina ya mwanamke anayechukulia kupendwa kama silaha ya kumnyanyasa mwanaume.

Usitafute nyumba ndogo, bali ongea naye pamoja na watu wenu wa karibu mnaowaheshimu, asipokuelewa mpe muda akapumzike kwao kidogo akiwa huko kama hana mpenzi wa pembeni basi atajirekebisha.

KILA jambo likizidi lina ubaya wake Yawezekana upole wako umezidi kipimo, so yeye anauchukulia ndivyo sivyo kabisa.
Natamani kama ungekuwa wangu.....lol

HONGERA SANA UAMINIFU WAKO,NA ENDELEA KUWA MWAMINIFU NA KUIHESHIMU NDOA YENU, NAAMINI HILO NI WIMBI TU LA KUPITA KUWENI MAKINI,
LISIJEZAMISHA NDOA YENU. POLE SANA, USIPATE PRESSURE ILA HAKIKISHA UNALIPATIA UFUMBUZI HARAKA.

eeeeeeh, yamekuwa hayo tena?
Acha kutamani tamani, na hasa kama una wako ndani nnunu?
 
waoo,natamani nipate mume kama wewe...inaelekea umstraabu sana,sijui ufanyeje but you can try kuwaita wazee au wamama anaowaheshimu waongee naye na kumuambia hilo jambo hupendezwi nalo.........au tafuta muda abao mko wote happy,mmerelax umwambie kwa upole kuwa hupendi tabia yake ya kujikweza kama anakupenda atakusikiliza,ila huyi bidada inaelekea anasumbuliwa na pepo la ubinafsi na kujikweza,muombee yatoke lol

3 yrs waanze kuita wasuluhishi? hapana kabisa! tena kwa jambo kama hilo, ote ndao, kuna mambo na mambo jamani.
 
kwani kaka kuanzia mnaanzana ulikuwa huwajui frnds zake? au umeona mabadiliko gani kwasasa mpaka unataka kuwajua? kuhusu pesa wengine tunadanganyaga tu cku zinasonga, nimepata shs 100 kumbe 250, labda na uchaga umenikaa kwenye damu kujiteeta kwenye pesa nakujua sana.
 
Pole sana, hivi huyo mwanamke ni kabila gani? Unajua, wapo wanawake ambao wakati mwingine wakionyeshwa wanapendwa sana basi anajishau! huyo mkeo ndiyo type hiyo, amesahau ghafla mara baada ya kupata mafanikio. Sasa,kwanza fuatilia biashara yake kwa karibu sana na kama ana kijana au binti anamuuzia huyo anaweza kuwa anajua mambo fulani atakusaidia, si bure lazima kuna kitu hapo. Siku nyingine chukua gari lake na tembea nalo the whole day hilo lako liache somewhere kwa muda fulani umuone responce yake. Na wewe kuwa wazi na mapato yako kwake, ili uwe na sababu ya kumuambia kwanini yeye hataki ujue kuhusu biashara yake wakati wewe unamuambia kila kitu? Vile vile, mueleweshe ili ajue mnapokuwa kwenye ndoa vitu vyote ni vyenu si vya mtu binafsi ndiyo maana unamuuliza.

Kuhusu marafiki kama alivyosema Saweboy, marafiki zake huna haja ya kumuuliza utawajua tu kutokana na shughuli mbalimbali, na hata wanaomtembelea. Binafsi mume wangu hajawahi kuniuliza marafiki zangu na wala sijawahi kumuuliza marafiki zake ila anawajua marafiki zangu wote nami nawajua marafiki zake wote.

Pole ndg yangu pia Muombe Mungu sana ili ambadilishe mkeo ili ndoa yenu iwe ya amani, kuzungumza kwa pamoja kama ni muelewa ndiyo the best solution!
 
Wakuu. Mawazo yenu nayathamini mnanipa faraja. I will soon take a hardline decision naona nyumba inataka kuwa ndogo and I am not prepared. Nina value ndoa lakini I don't give damn a shit! Wacha nimweke under probation for a while or else atajikuta kwao. We only live once na tunataka tuishi kwa amani na raha. Naendelea kuwasikiliza idea zenu ni helpful kwa kweli
ndugu yangu kwanza pole.pili hongera kwa ujasiri na busara ktk hiyo issue.kuwa mpole sio ujinga.Biblia inataka wanaume kuishi na wake zao KWA AKILI na ndo ulivyofanya! Ushauri 1.usimrudishe kwao 2.nahic nawe umechangia hali aliyo nayo mkeo maana km had leo hujui aina ya rafiki wa mkeo napata shida kujua mwanzo wa uchumba wenu ulikuwa wa aina gani.3. Tafuta kitabu kiitwacho NDOA YANGU,NINGEJUA kitakusaidia sana kujua wapi umechangia tatizo lako na kwanini ndoa nyingi hazina amani na zinavunjika
 
Simama kama mwanaume muulize panapotakiwa kuuliza,asipotoa ushirikiano kuwa mkali kama akizidisha ukorofi funga biashara yake,wewe ni mwanaume lazima uwe kiongozi wa familia!
Nimependa huu ushauri. Chukua nafasi yako kama mwanaume. Usimbembeleze, anaonekana sio mwelewa.
 
Nimependa huu ushauri. Chukua nafasi yako kama mwanaume. Usimbembeleze, anaonekana sio mwelewa.

Sweetlady niko hapa.

Nna mpango wa kuwakodi Majembe Auction Mart waje wanisaidie kudai deni langu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom