Msaada karibu napata presha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada karibu napata presha

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NyaniMzee, May 9, 2011.

 1. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  Wana JF, na hasa wale wenye weledi na mambo ya ndoa.

  Mke wangu niko naye miaka 3. Tuna mtoto 1 wa miaka 3. Nimemfungulia biashara nzuri, anaingiza pesa nzuri tu kwa siku. Usafiri nimempa wa kumpeleka kazini kwake na kumuwahisha home. Tatizo moja linanikwaza: nikitaka kujua maswala yanayohusu pesa au marafiki zake hata wa kike tu, basi majibu yake huwa ni mkato na ya jeuri, na hachelewi kusema usinisimange au kama umechoka niambie.

  Kuepuka shari mimi huwa najishusha na kumtuliza kuwa haikuwa kwa nia ya kumkwaza bali kama mume nina haki kujua. Hajui kusema samahani hata pale anapogundua alikosea kauli. Sasa haya maisha dawa yake nini? Nami sitaki kuzurura, napenda niishi naye kama ahadi ya ndoa.

  Wakuu mawazo yenu please!
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Kha!!! Yaani natamani huyo mwanamke ningekuwa mimi hakyamungu vile dah mwanaume mpole hivi.....ngoja niperuzi nitarudi kwa ushauri
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Jamani.....pole kwa kupata mkorofi wako!
   
 4. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mtafutie nyumba ndogo....saa nyengine tunakuwaga na kiburi tukiwa hatuna ushindani,:bange::bange::bange:
   
 5. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  Pauline,nyumba ndogo ndogo tu ukilala mguu inatokeza nje!! sidhani kama ni suluhisho labda la mwisho wa yote.
   
 6. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  waoo,natamani nipate mume kama wewe...inaelekea umstraabu sana,sijui ufanyeje but you can try kuwaita wazee au wamama anaowaheshimu waongee naye na kumuambia hilo jambo hupendezwi nalo.........au tafuta muda abao mko wote happy,mmerelax umwambie kwa upole kuwa hupendi tabia yake ya kujikweza kama anakupenda atakusikiliza,ila huyi bidada inaelekea anasumbuliwa na pepo la ubinafsi na kujikweza,muombee yatoke lol
   
 7. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  NyaniMzee,humu MMU kuna thread kafungua Lizzy leo title yake ni 'upole'hebu isome yote hadi mwisho,ina page kama 9 hivi),majibu yote ya swali lako utayapata hapo.Kila la kheri.
   
 8. V

  Vumbi Senior Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kuhusu suala la fedha hiyo ni haki yako kujua mapato na matumizi vinginevyo hiyo biasha inaweza kufa na hasara itakuwa kwa familia na siyo kwa mke wako. Kinachotakiwa ni kumuelimisha mkeo juu ya umuhimu wa kukagua hiyo biashara tumia lugha nzuri, ukiona anaendelea kukataa jua kuna mchezo anakuchezea kwenye hiyo biashara.

  Wakati mwingine unatakiwa usimame kama baba ili uweze kufanya maamuzi yenye maslahi kwa famili na siyo kukubali kila jambo analotaka mkeo hata kama lina hatarisha uchumi wa familia. Unatakiwa umueleze kwa ufasaha ni nini unakitaka kwenye hiyo biashara na utaratibu wako wa ukaguzi ili hiyo biashara iweze kuwa na manufaa kwa familia na hapo siyo suala la kwamba anataka au hataki bali ni utaratibu anaotakiwa kuufuata kwa maslahi ya biashara na familia. Siyo kila jambo ndani ya nyumba baba unatakiwa ucheke cheke na kukaa kimya, mengine unatakiwa uwe na kura ya veto.

  Kuhusu kuwafahamu marafiki zake sijafahamu wewe unawataka kwa lengo gani. Wanaume hatuwauliza wake zetu marafiki zako ukitaka kuwafahamu unaweza bila hata kummuliza. Je mkeo haalikwi kwenye tafrija yoyote? huwa hatembelei mtu yoyote? hatembelewi na mtu yoyote? etc. Suala la kutaka kufahamu marafiki zake kwa kumuuliza yeye mwenyewe achana nalo linaweza kukuingiza kwenye mgogoro usiyokuwa wa lazima.
   
 9. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  Vumbi,nashukuru kwa mawazo yako. nadhani bado nitapata mengi toka kwa wadau.
   
 10. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Pole kaka! hii ndo dunia, kuna watu wa kila aina.
   
 11. S

  Sweetlol Senior Member

  #11
  May 9, 2011
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole sana.ila huyo mwanamke anabahati.embu mpe mkwara baridi.usimuulize kitu,chelewa kurudi na uwe bizze na simu yako hata kama unawasiliana na washkaji.atabadilika tu huyoo.
   
 12. LD

  LD JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nipe nafasi nimsaidie kujibu kabla hujauliza, labda atajifunza. Ila simama kama mwanaume mwaya, kwa hekima na akili. Akibisha mrudishe nyumbani aache hio biashara, labda ndo inampa kiburi.
   
 13. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  mpeleke kijeshi we c kila k2 umemfanyia halafu analeta nyodo! Kama vp tia chaka
   
 14. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwani wewe hufiki kazini kwake? Huangalii hata alivyopanga bidhaa! Angalia usijekuta maboksi matupu merembeshewa duka baba.
  Kawaida ya wanawake ingawa sio wote huwa na mashoga ambao sio wazuri. Ushauri wao huwa mbovu sana. Wanachojali wao ni kujaza matumbo yao tu. wanaitwa wapambe hao. Angalia wasije wakawa wamemwingiza kwenye mtandao wa kipuuzi maana wanawake wa mjini hawakawii.
  Tafakari chukua hatua!
   
 15. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Nyanimzee hizo ndo changamoto za maisha! Labda nikuulize katika maisha yenu mmempa Mungu nafasi gani? Kama hamna hofu ya Mungu shetani ni rahisi sana kuchukua nafasi. Mbaya zaidi, shetani hana sura moja, leo anakuja kama mbwa, kesho chura, keshokutwa anakuja kama malaya, then kiburi. Njia yake ni moja muangalie aliyekuumba, huwezi amini, sala inanguvu ya ajabu sana.
  Nimefurahi ulivomjibu Pauline, thats the way to go brother. Giza halishindwi kwa giza, bali giza hushindwa kwa mwanga.
   
 16. SAWEBOY

  SAWEBOY JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  Mkuu pole kwa hayo yanakukuta. Kwa kuwa anasema kama umemchoka umwambie tu hapo lazima kuna jambo limejificha na wala usidhani masihara, kuna kitu anajivunia tu na wewe anakuona kwa sasa huwezi kumbabaisha especially kama kuna mtu pembeni na hiyo ni ngumu wewe kujua. Kwa kujihami usijue ndio maana anakujia juu coz ameshajua udhaifu wako kuwa akikupnadishia wewe unaua soo kwa kuwa mpole.

  USHAURI MZURI

  1. Wewe ndiye uliyemfungulia biashara anayofanya na kupata kipato kizuri tu, pia usafiri umempatia (ana bahati sana ya kupendwa ila hapendeki huyu dada) kwa hiyo hakuna tatizo la wewe kumuogopa, hapo unaibiwa mkuu lazima kuna mtu ana-msugua pembeni bila wewe kujua. Chukua hatua haraka mkuu/ tena faster! Hatua gani sasa ya kuchukua?

  2. Mtegee ishu kidogo tu, muulize kwa upoleeee kabisa akikujia juu, we ni mwanume na ndio uliyemuoa hivyo mrudishe kwao kwa mapunziko bila kumwambia lini utamfuata au mwambie rudi nyumbani kwenu na utakapoona umebadilika tabia na kutambua mimi ni mume wako hapo ndipo urudi lakini usirudi kabla ya miezi 6 au 3 hata kama akijua kosa lake!

  3. Endapo ukiona amefurahia kurudi kwao na huku anakujibu kwa jeuri basi ujue hapo huna ndoa mkuu lazima ujue kuna mtu anachakachua tu hiyo kitu but ukiona anakuwa mpole ghafla usibadili uamuzi muache aende akajifunze na akirudi kuja kutubu hatarudia tena.

  NB: akifurahia kurudi kwao basi ndani ya mwezi 1 utajua nani anasugua huyo mashine na hapo ndo utajua jeuri ya mkeo inatoka wapi.

  Pili usimruhusu kuondoka na mtoto, mwambie aende na mtoto amwache home lkn akilazimisha basi muachie mtoto aende nae!

  CHUKUA HATUA HARAKA SANA MKUU
   
 17. KWI KWI

  KWI KWI JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu wakati mwingine mwanamke anavutiwa,anasikiliza na atakuzimia kuliko ''only if you can Ignore her for a little while''.....she will come to her sense.
   
 18. e

  ejogo JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bwana NyaniMzee, nakushauri kaa na mkeo umweleweshe kwanini unataka kujua hayo mambo unayomuuliza. Labda anadhani kwa kumuuliza hivyo unakuwa kama unamnyanyasa kwakuwa umempa hiyo biashara. Mweleweshe tu role yako ni nini na yakweke ni ipi kwenye kuiendeleza familia yenu. Mara zote mweleze ukweli kwajinsi unavyojisikia na msisitize na yeye awe anakuambia jinsi anavyojisikia kuhusu wewe, kwani kukaa kimya kunaweza kuleta big prob. hapo baadae.
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  May 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Nawe anza kumfanyia vituko japo siku mojamoja...
   
 20. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  Wakuu. Mawazo yenu nayathamini mnanipa faraja. I will soon take a hardline decision naona nyumba inataka kuwa ndogo and I am not prepared. Nina value ndoa lakini I don't give damn a shit! Wacha nimweke under probation for a while or else atajikuta kwao. We only live once na tunataka tuishi kwa amani na raha. Naendelea kuwasikiliza idea zenu ni helpful kwa kweli
   
Loading...