Msaada: Kaibiwa iPhone halafu mwizi anaonekana Online akichat

.... watanzania tunapuuza sana vitu vya msingi kama ku-set passwords na kutunza IMEI tukiibiwa ndio fahamu zinatujia kuhusu umuhimu wa hivyo vitu! Utakuta kifaa cha gharama lakini wala mtu hajisumbui kuweka basic security settings za kifaa chake; laptops, simu, etc.
Mkuu unaweza kuwa na IMEI namba lakini na simu usiipate utazungushwa miaka jaribu Bahati yako
 
Binafsi nasema hivi hivi,

Ni kweli Hawa jamaa ni wazinguji mara nyingi, ila mimi pia nishashuhudia washkaji zangu wawili wakipewa simu zao na mwizi kulipa faini, bila ya washkaji kutoa chochote wala kupoteza mda mrefu,

Walitoa raarifa wakaambiwa tuna foleni kubwa ya ku track watu kueni na subira, siku ya siku mmoja baada ya mwingine kwa siku tofauti wanapigiwa simu wakachukue simu zao na watuhumiwa wakiwa ndani, wakalipa na faini zote, Na guess what? Mmoja alikamatiwa Mbeya, akaletwa mpaka Dodoma(ilikua ni pale dodoma central)

Huyo mwingine baada ya kumtrack wakapata namba zake za simu Polisi wakampigia ajisalimishe, maana walimtajia eneo alilopo mda huo, watu anao ongea nao kwenye simu, na isitoshe polisi walishaongea mpaka na watu wake wa karibu, jamaa kuona hivyo alijipeleka mwenyewe polisi, bahati mbaya kumbe aliuziwa, lakini No way akatoa simu na mafaini kibao,

Mfano hai Mwingine Mimi kuna demu nirafiki yangu, kipindi nipo chuo, hio siku tumekaa kwenye kibweta tunasoma, alipigiwa Simu na polisi, akaambiwa "hio simu unayotumia ni ya wizi, watu wako unao ongea nao sana ni hawa, umeanza kuitumia siku flani, na sasahivi upo sehemu flani, kwahio simu ina kesi, iwe umeiba wewe au laa ila lete kituoni"

Simu imekata tuu, mtu huyo chini Buuuu!, nikamsaidia pale alipopata network nikamwambia twende usijali, BAHATI nzuri alikua na namba ya aliyemuuzia kufika wakamwambia tuachie, jamaa akadakwa kibabe, akamlipa dada pesa yake, yaliyoendela hatujui.

Kwahio kwa ufupi hawa jamaa uwezo wanao, na wakikusubilisha Pengine wanataka chochote, au Ni foleni, maan ukweli ni kwamba hizo kesi ni nyingi sanaa, au sasa pengine kwa bahati mbaya ni kweli unakula kamba,

Ila Makando kando yao mengi ndio yanafanya watu tusiwaamini.

Lakini pia kumbuka kuriport polisi sio tuu kuipata simu yako, lakini pia, umepoteza simu yako bado una majozi, kumbe inatumika katika uhalifu, unapigiwa simu polisi badala uambiwe njoo uchukue simu yako, unaambiwa wewe kwa kutumia simu yako umefanya matukio haya na haya ya kihalifu... Ukifika utadai "nilipoteza!" ni simple tuu watakuuliza "uli riport?", "hapana", "Ni kwamba ulidharau.." "Kesi juu yako..."

Tena mazingira kama hayo ndio magumu sana kama mtumiaji anatumia namba hio hio tena.
Mshauri aende polisi.

Aksante.
... kwa desturi za watanzania hapa ndipo mamlaka husika zinatakiwa kutoa elimu ya kutosha. Raia wasisitizwe kununua simu kutoka maduka rasmi na sio mikononi mwa watu tena wasiowafahamu! Mtu anakuuzia iPhone laki na wewe kabisa unanunua; dah! Polisi watume SMS mara kwa mara kuwaonya wananchi kununua simu mikononi mwa watu hususan wasiowafahamu na wawaelimishe consequences zake.
 
Back
Top Bottom