Msaada jinsi ya kuongeza CD4

sowmya

Senior Member
Jul 9, 2016
109
40
Ndugu yangu wa karibu sana anatatizo la HIV muda mrefu sasa ila tatizo lake CD4 zimeshuka sana zipo 18 na uzito 45 hawez kutembea mwenyewe na pia anasumbua sana kula chakula

Je ni dawa zipi zinaweza ongeza CD4 kwa haraka zaidi?
 
Kwanza ale chakula ili apate Ngitu ya kutembea pili auzurie clinic ya wagonjwa wa ukimwi atapata dawa nzuri za kuongeza cd4
 
Ndugu yangu wa karibu sana anatatizo la HIV muda mrefu sasa ila tatizo lake CD4 zimeshuka sana zipo 18 na uzito 45 hawez kutembea mwenyewe na pia anasumbua sana kula chakula

Je ni dawa zipi zinaweza ongeza CD4 kwa haraka zaidi?
Pole sana ndugu. Kuna drip za maji ambazo mgonjwa huwekewa zinaitwa kwa kifupi RL. Zinapatikana Pharmacy kubwa za mjini dar moja wapo ni ile ya posta mpya jengo la benjamini mkapa. Ukimpa hiyo swala la kula uandae bajeti yake maana atahitaji chakula kama mchwa. Mimi si mtaalam wa afya lakini nilishauriwa kwa ndugu yangu ambaye alikuwa hali kwa siku sita mfululizo lakini baada ya kuwekewa drip mbili za RL akaamka na kuanza kula mwenyewe. bei yake drip moja ni Tsh 32,000
 
Ndugu yangu wa karibu sana anatatizo la HIV muda mrefu sasa ila tatizo lake CD4 zimeshuka sana zipo 18 na uzito 45 hawez kutembea mwenyewe na pia anasumbua sana kula chakula

Je ni dawa zipi zinaweza ongeza CD4 kwa haraka zaidi?
Kuna issue nyingi sana kuhusiana na kupandisha CD4. Lakini kwa ufupi kupandisha CD4 kwa dawa nje ya ART bado ni ndoto. Hebu note hivi vitu.

1. Ukianza kutumia dawa za VVU huku CD4 zikiwa chini sana, huwa vigumu sana kupandisha CD4 zaidi ya 100. Unajua ile reserve ya immune function inakuwa depleted. Ndio maana sasa tunasema kila mgonjwa mwenye HIV aanze dawa bila kujali ana CD4 ngapi.

2. CD4 count inaweza ikawa hata chini ya 10 na bado dawa zako zikawa zinafanya kazi vizuri sana. (Yaani hata ukipima uwingi wa wadudu wa VVU kwenye mashine wasionekane). Lakini kwa sababu CD4 zako ziko chini unakuwa bado una risk ya kupata magonjwa nyemelezi na kansa zinazohusiana na VVU kama Kaposi's Sarcoma kwani hizo CD4 ndizo hupambana na hayo magonjwa nyemelezi.

3. Ni kweli ni muhimu kupandisha CD4 count, lakini si kila kupanda kwake kuna tafsiri ya kuendelea vizuri. Kuna CD4 zinaweza zikawa zimepanda lakini zikawa non-functional (yaani zisizofanya kazi). Watu watasema kunywa hiki na kile, lakini do they increase production of functional CD4 count au wajifurahisha tu.

4. Mashine zinazopima CD4 count huwa hazipimi kama absolute number. Ila kuna vitu huvipima na kisha kupiga mahesabu kupata value ya absolute CD4 count. Hutumia formular hii:

Absolute CD4 count = %age of CD4 x Total White Blood Count.

Hizo Total White Blood Count (kwa kifupi WBC, ndio ni jumla ya chembechembe nyeupe za damu, ambayo inahusisha pia CD4 cells) na hiyo %age of CD4 count ni asilimia ya chembechembe zenye CD4 katika chembechembe zote za damu).

Hivyo kuwapo kwa WBC katika formular hii huwa kuna affect Absolute CD counts zinazopimwa.

Mifano ukipata magonjwa nyemelezi au yasiyo nyemelezi au dawa zitakazosababisha White Blood Count zipande basi ukipima CD4 count zako zitaonekana ziko nyingi pasipo ukweli na vivyo hivyo baadhi ya magonjwa au dawa vinavyoshusha chembechembe nyeupe za damu (WBC) zitasababisha absolute CD4 count ionekane imeshuka pasipo uhalisia.

Kwa hiyo issue ya kupandisha CD4 sio nyepesi kama inavyoongelewa kwenye mitandao.

By the way mpaka sasa tafiti zimeonesha hakuna dawa inayoweza ikapandisha functional CD4 zaidi ya hizi dawa za kupunguza makali ya VVU.
 
kwa iyo mkuu unamsaidiaje mawazo nini kimsaidie cd4 zipande
 
Mkuu kama CD4 hazipandi kunaweza kukawa na vitu viwili vikuu.

1. Dawa haifanyi kazi vizuri (treatment failure) kitu ambacho katika kliniki yake wanaweza wakagundua.

2. Dawa zinafanya kazi vizuri lakini mgonjwa alianza tiba akiwa na CD4 chache sana. Hivyo immune recovery kwake imekuwa shida.

Hapo kwenye 1 anaweza akabadirishiwa dawa au akasisitizwa utumiaji sahihi wa dawa. Lakini kwenye 2 mgonjwa ataendelea na dawa anazotumia kwani zinafanya kazi.

Cha muhimu kujua ni kutotegemea dawa nje ya ART kukupandishia CD4.

Kula chakula bora, tumia hata hizo supplements ili uwe na afya njema. Lakini issue ya kutumia dawa fulani kwa nia tu ya kupandisha CD4 hiyo haipo.

Tunadanganyana sana na kuibiwa pesa katika upandishaji wa CD4.
 
Ndugu yangu wa karibu sana anatatizo la HIV muda mrefu sasa ila tatizo lake CD4 zimeshuka sana zipo 18 na uzito 45 hawez kutembea mwenyewe na pia anasumbua sana kula chakula

Je ni dawa zipi zinaweza ongeza CD4 kwa haraka zaidi?
ebu mkuu unaweza kutusaidia alianza kutumia dawa akiwa na cd4 ngapi? na ana Muda gani toka aanze kutumia dawa za arvs?
 
Back
Top Bottom