Namna ya kusafisha pasi yako

Njia ingine nzuri ya kusafisha pasi ni hii,

1) Unaiwasha pasi (unaiacha mpaka ipate moto)

2) kisha unaweka adol juu ya pasi (sehemu ya uchafu) ikiyeyuka unafuta na taulo ulioiloeka kwenye maji na ukaikamua kabla ya kufutia pasi hiyo. fanya hivyo mpaka uchafu wote utoke.
 
Attachments

  • 033f3da5256511ffe3ff8b646147d818.jpg
    033f3da5256511ffe3ff8b646147d818.jpg
    67.8 KB · Views: 443
Ukishindwa hizo zote tumia kidonge au tembe kadhaa za Panadol.

Washa pasi yako na rekebisha moto usiwe mkali sana.

Inamisha pasi kiasi kwamba kitako chake kielekee juu, weka kidonge cha Panadol sehemu yenye uchafu juu ya kitako cha pasi hadi kitapoañza kuyeyuka.

Tumia kitambaa kufuta uchafu huo kwa kutumia kile kimiminika kitokanacho na Panadol inayoyeyuka.

Fanya hivyo hadi kitako kitapotakata.

NB:
Sina uhakika na madhara kwa mwili kutokana na moshi au gesi yoyote itokanao na Panadol iyeyukayo/iunguayo.

Muhimu hakikisha unakwepa kuuvuta moshi huo.
 
!
!
Samahani sana wadau.....Naomba kwa anayejua njia ya kuondoa uchafu kwenye pasi, moja na mbili ni nini cha kuzingatia ili uchafu huo usijirudie katika [asi ya umeme.

Pasi ya nyumbani kwangu khaaa ni tabu sana, yaani chini ina uchafu flani hivi umeganda na mara kwa mara umekuwa ukikwamisha utanashati wangu ama kwa kuchafua nguo nyeupe au kwa kunilazimisha kuvaa nguo bila kupiga pasi. Naomba mwenye kujua anisaidie
 
Chukua panadol au paracetamol weka pasi yako ipate moto vya kutosha igeuze uibane vizuri chukua vidonge vyako kimoja kimoja au viwili. Viwili chukua gazeti au box nene weka vidonge vyako juu yaa pasi sehemu husika yenye uchafu ,vidonge vikianza kuyeyuka kama nyloni anza kuvisugulia pale uchafu wote utaondoka kama bado ongeza vidonge.

WARNING : HAKIKISHA UJIUJI ULE WA ZILE DAWA UNAO YEYUKA AUKUDONDOKEI MAANA NI ZAIDI YA UJI WA NYLON UTALIA KILIO CHA PAKA MWIZI ALIYE PIGWA AU UTALIA KAMA VILE UMESIKIA JINA LAKO KWENYE LIST YA RC WAKATI UNAJUA WAZI HAUFANYI HIYO BIASHARA
PILI ULE MOSHI WA DAWA UNAO TOKA BAADA YA DAWA KUYEYUKA UNAUMIZA SANA SO JITAIDI KUWEKA MBALI NA PUA YAKO PIA UKIMALIZA KUSUGUA FUTA NA GAZETI
 
Chukua panadol au paracetamol weka pasi yako ipate moto vya kutosha igeuze uibane vizuri chukua vidonge vyako kimoja kimoja au viwili. Viwili chukua gazeti au box nene weka vidonge vyako juu yaa pasi sehemu husika yenye uchafu ,vidonge vikianza kuyeyuka kama nyloni anza kuvisugulia pale uchafu wote utaondoka kama bado ongeza vidonge.

WARNING : HAKIKISHA UJIUJI ULE WA ZILE DAWA UNAO YEYUKA AUKUDONDOKEI MAANA NI ZAIDI YA UJI WA NYLON UTALIA KILIO CHA PAKA MWIZI ALIYE PIGWA AU UTALIA KAMA VILE UMESIKIA JINA LAKO KWENYE LIST YA RC WAKATI UNAJUA WAZI HAUFANYI HIYO BIASHARA

Baking soda vijiko viwili, maji safi kijiko kimoja (kijiko cha chakula).

Changanya, paka chini kwenye pasi kisha futa na kitambaa laini, kaza mkono.
Hiyo baking soda nayo ni vijiko vya chakula? Napaka na kufuta na kitambaa pasi ikiwa ina moto au ikiwa kawaida?
 
Au chukua mshumaa, washa pasi yako ipate moto mkali, then chukua mshumaa paka kwenye pasi yako pale penye uchafu then chukua still wire weka kwenye kupasio halafu sugua na utaona majibu yake.
 
Chukua mzizi wa msaguneda unapatikana eneo la Bujora kule mwanza sugulia itakuwa safi, pia kabla ya kutumia pasi kemea kwani kuna pepo/jini linapenda kukaa kwenye pasi.
 
Back
Top Bottom