Msaada: Jinsi ya Kumaster Manual Car!

Manual raha sana aiseee.
Lakini kubwa na la kuzingatia,ukipata dharula ya tairi mfano ikapasuka we komaa na usukani tu,usiguse brake wala clutch na hili linaweza kuwasaidia hata wenye auto cars,usiguse brake...
Kwa madereva stadi wanaelewa hili.
Na kama uelewi bora uulize
 
Kama unaweza kuendesha Automatic basi kwenye manual nenda kwenye miinuko sehemu ambapo ukiachia brake gari inarudi nyuma.Hapo jifunze kubalance brake,MOTO na clutch.
Usilazimishe kukalili jinsi ya kuondoka,KIKUBWA ISIKILIZE GARI INATAKA GEAR NO NGAPI.
Utazoea tu muda sio mrefu hata mlimani unasimama kwa kutumia clutch na moto bila brake.
Ha ha ha mimi mlimani huwa na simama na accelarator tu kwenye auto
 
Binafsi naamini dereva hajakamilika kama hawezi kuendesha gari za Manual transmission. Mkuu big up kwa kuamua kujifunza gari za manual
Elewa kuna driver-proffesional(kazi ya udereva) na driver(anaendesha gari) lakini si kama kazi huyu auto inamtosha.
 
Hivi vitu ni interest ma commitment juu ya ufuatiliaji! Binafsi gari nilijifunza kiajabu sana. Kwa mara ya kwanza mie niliendesha gari ikiwa ni automatic soon baada ya kununua.
Nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja alinipa maelekezo ya nadharia tu huku akinionesha namna ya kuondoa na vitu muhimu kama indicators, taa, breki na vitu vingine. Sikukaa kwenye steering wheel nikajaribu.

Ila siku nimenunua gari yangu I just worked on the ABC of the guy na nikaendesha ndinga hadi home safe and sound. Tangu hapo nimeendesha almost kila kona ya nchi hii.

Nikaja nikapata hamu ya kujua namna ya kuendesha manual. Hapo nilizama Youtube nikala tutorials za kutosha kuanzia hill start, city driving na vitu vingine.
Siku nikaja nikakaa kwenye Isuzu KB old model. Niliipiga kutoka Chanika hadi Kigamboni (zama za pantoni)na nikarudi salama salmini. Tangu hapo najiendeshea gari za MT na AT bila shida.
Naweza kuhitimisha kwa kusema jambo la msingi ni kuweka nia ya dhati kwa kila unachotaka kufanya na pia ufuatiliaji wa karibu
 
Hivi vitu ni interest ma commitment juu ya ufuatiliaji! Binafsi gari nilijifunza kiajabu sana. Kwa mara ya kwanza mie niliendesha gari ikiwa ni automatic soon baada ya kununua...
Kwa hiyo leseni yako ya magumashi mkuu ?
 
Kwa hiyo leseni yako ya magumashi mkuu ?

Hivi issue ni leseni au skills?

Maana yake tusiamini sana vyeti kuliko skills. Ndio maana kuna watu wana hadi leseni kuendesha mabasi ya abiria ila mpe Rav 4 manual hawezi kuiondoa!

Tusiamini sana vyeti
 
Back
Top Bottom