Mkuu, kuliko kuhangaika na hiki kitu kimoja kwa nini usidevelop passion ya muziki na ukajifunza from scratch, ukafanya makosa machache ambayo yatakufanya uwe producer mzuri zaidi. Utajipatia kazi yenye malipo mazuri na kukutana na watu wanaopenda muziki kama wewe.
Ingia Youtube pitia walkthrough ya fl studio. Lakini usitake kukariri vitu just angalia vitu muhimu na jinsi ya kuvipata. Kama Piano roll, drum kits, installing VST plugins, effects, baadhi ya mbinu katika piano roll n.k.
Baada ya hapo ukajifunza Music Theory, kuna youtube channel ya Hack Music Theory wako vizuri sana, watakupa na free ebook ujifunze music theory. Baada ya hapo unaweza ukajifunza hata instrument moja ili kupanua wigo wa ujuzi wa muziki. Then ukaanza kutengeneza beats.
Cha muhimu kuwa experimental sana. Jaribu kutengeneza vitu original na vya kwako mwenyewe. Utafurahia sana na itakuongezea hata ubora wa maisha yako. Muziki ni tiba nzuri sana. Imagine unaamka asubuhi unatengeneza kitu ambacho hakikuwepo bado, thats creativity.
Nikipata muda ntatupia baadhi ya kazi zangu uzisikilize.
Niache Nteseke