Msaada: Jiko la umeme lina shoti

Msaada: Jiko la umeme lina shoti

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Posts
15,295
Reaction score
10,965
Wakuu jiko langu la umeme la plate nne na oven linapitisha umeme wa shoti. Tatizo liko hivi, hata ukiwa umezima socket ya ukutani ya jiko umeme ubapita na unarusha sana kwa shoti. Nilishamleta fundi akirekebisha tatizo linatokea tena baada ya muda mfupi. Kwa sasa limeunguza plate kubwa mbili. Ninaomba sana wataalam wa umeme hususan, wa majumbani na majiko wanisaidie utaalam ili nijue tatizo na tiba sahihi. Shukrani wakuu.
 
Kama hata ukizima ukutani bado linapiga shoti, basi tatizo sio jiko. Tatizo lipo kwenye wiring yako au kuna kifaa kingine cha umeme kinasababisha shoti katika hiyo nyumba aidha katika chumba chako au chumba kingine,(Tatizo kama hili linaitwa EARTH LEAKAGE, yaani kuna muingiliano kati ya LIVE na EARTH).

Solution:
1. Tatuta screwdriver Tester, nenda kwenye soket , zima socket ya jiko chomoa plug ya jiko kama inachomoka kama haichomoki ndenda kwenye soket nyingine yoyote, chomeka tester kwenye EARTH Connector ya socket(lile tundu la juu katikati) angalia kama tester itawaka, endapo itawaka basi ume prove kwamba kuna EARTH LEAKAGE.

2. endapo tester itawaka, basi zima na uchomoe kwenye soket vifaa vyote vya umeme nyumba nzima(vyumba vyote, hata kwa majirani kama wapo). na uendelee kupita earth leakage(rudia hatua namba moja hapo juu ) kama tester haitawaka, basi anza kuchomeka (Kurudishia kwenye socket) kifaa kimoja kimoja huku unaendelea kupima Earth leakage hadi utakapopata kifaa kinachosababisha earth leakage.

3. Kama tester itakuwa inawaka hata baada ya kuchomoa vitu vyote basi tatizo lipo kwenye wiring(Especially darini).

NB: vifaa vinavyoweza kusababisha tatizo hilo ni pamoja na:
  • Firidge
  • jiko la umeme
  • rice cooker
  • microwave
  • all ovens
  • bath heater (All heaters)
  • pasi
  • na vifaa vyote vyenye plug za pini tatu (3 pins plug)

Mkuu ymollel heshima yako. Ninashukuru sana kwa technical expertise. Nitafanya kazi na fundi mguu kwa mguu. Hili tatizo limetutesa sana kwa muda. Likirekebishwa linajirudia baada ya muda mfupi. Kwa hakika utaalam wako hapa ni unique maana mafundi wawili lakini hakuna aliyefanya details hizi. Keep it up mkuu.
 
Ymollel ninakushukuru sana. Kwa kufuata ushauri wako fundi alikuja na tatizo liligundulika na kutibika. Mungu ninayemuamini na akubariki kwa ukarimu wako. Nawe ukirimiwe popote utakapohotaji.
 
Kama hata ukizima ukutani bado linapiga shoti, basi tatizo sio jiko. Tatizo lipo kwenye wiring yako au kuna kifaa kingine cha umeme kinasababisha shoti katika hiyo nyumba aidha katika chumba chako au chumba kingine,(Tatizo kama hili linaitwa EARTH LEAKAGE, yaani kuna muingiliano kati ya LIVE na EARTH).

Solution:
1. Tatuta screwdriver Tester, nenda kwenye soket , zima socket ya jiko chomoa plug ya jiko kama inachomoka kama haichomoki ndenda kwenye soket nyingine yoyote, chomeka tester kwenye EARTH Connector ya socket(lile tundu la juu katikati) angalia kama tester itawaka, endapo itawaka basi ume prove kwamba kuna EARTH LEAKAGE.

2. endapo tester itawaka, basi zima na uchomoe kwenye soket vifaa vyote vya umeme nyumba nzima(vyumba vyote, hata kwa majirani kama wapo). na uendelee kupita earth leakage(rudia hatua namba moja hapo juu ) kama tester haitawaka, basi anza kuchomeka (Kurudishia kwenye socket) kifaa kimoja kimoja huku unaendelea kupima Earth leakage hadi utakapopata kifaa kinachosababisha earth leakage.

3. Kama tester itakuwa inawaka hata baada ya kuchomoa vitu vyote basi tatizo lipo kwenye wiring(Especially darini).

NB: vifaa vinavyoweza kusababisha tatizo hilo ni pamoja na:
  • Firidge
  • jiko la umeme
  • rice cooker
  • microwave
  • all ovens
  • bath heater (All heaters)
  • pasi
  • na vifaa vyote vyenye plug za pini tatu (3 pins plug)
Mkuu umenisaidia na mimi, nadhani ndio ugonjwa wangu huu ahsante mkuu ,kwa mafundi tulionao itabidi niiprint hii post yako nimkabidhi bwana umeme wangu aifanyie kazi!
 
Back
Top Bottom