Msaada jamani

Msaada jamani

Idimulwa

Platinum Member
Joined
May 27, 2011
Posts
6,263
Reaction score
5,429
Wakuu hali huku kitaa ni ngumu sana,najaribu kuchakalika lakini mambo bado ni tight,sasa nahitaji na mi nafasi ya u green guard ili nijiunge kambini hatimaye nishiriki kwenye harakati za uchaguzi mdogo kule Arumeru Mashariki.
Naomba anayejua taratibu za kujiunga na kiwango cha elimu kinachotakiwa ani mwagie hapa jamvini bila kusahau kunijuza wapi ni peleke cv yangu,make kuna watu nasikia wali make sana kule Igunga.
 
Ndio maana umepuuzwa hamna aliyechangia. Pumba tupu!
 
mimi ndo sijaelewa
unasema green card au ubunge ni kipi kati ya hivi.
 
mimi ndo sijaelewa
unasema green card au ubunge ni kipi kati ya hivi.

Kiongozi mie nataka u green guard tu unanitosha,kipindi cha uchaguzi mdogo wa Igunga walipiga kambi na kufanya mafunzo yao pale Misigiri
,Singida
 
Badilisha kichwa cha habari dogo. ndio mana wa2 wanakupuuza.
POPOBAWA.
 
mimi ndo sijaelewa
unasema green card au ubunge ni kipi kati ya hivi.

Anataka kuwa GreeGuard, kikosikazi cha vijana wa Chama cha Mapinduzi, kinacholinda kura na mazabe mengine kama hayo.
 
Ni rahisi. Jifanye hazikutoshi, pitapita mbele ya magamba huku ukiwaponda chadema ile mbaya, tena tishia kabisa kuwa mwaka huu utaua mtu. Nakuambia hiyo ni qualification ya juu sana, kesho unaitwa tu kwenye u green guard.
 
Asante mkuu,God bless u
 
Asante mkuu,God bless u

Anza kazi sasa, tena anzia karibu na ofisi za uvccm karibu na eneo la kampeni, jifanye mwendawazimu siyo mwendawazimu, kichaa siyo kichaa, ponda chadema ile mbaya, onyesha punch kama mbili tatu. Utashangaa unakuwa mkuu wa magreen guard, fungu unapewa wewe, then wenzako watakuja kukumwagia tindikali usoni kidooogo tu!
 
lol kazi ipo hapa
 
nenda umoja wa vijana CCM utapata majibu murua kabisa.Nalog off
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom