Msaada jamani kijana anachezea uwanja wa baba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada jamani kijana anachezea uwanja wa baba!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sajenti, Mar 18, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wana-JF naweka thread hii baada ya kumaliza kuongea na simu na rafiki yangu kipenzi aliyeko morogoro. Ni kwamba huyu bwana ni mtumishi wa serikali aliwahi kuzaa watoto wawili na mdada mmoja huko nyuma mtoto wa kwanza ni wa kiume kwa sasa ana miaka 24 anasoma IT kwenye chuo kimoja hapa Dar na mtoto wa pili ni msichana yuko kidato cha tano. Huyu bwana baadae alioa mke mwingine kwa ndoa ya serikali (hakumuoa mzazi mwenzie). maisha yao ya ndoa na mkewe kwa ufahamu wangu yalikuwa ya furaha sana na nimekuwa nikiwatembelea huko morogoro kila ninapopata nafasi ya kuwa huko. Leo amenipigia simu alichonieleza kimenistua sana na bado siamini ingawa yeye amenithibitishia kuwa hilo jambo limefanyika. Ni kuwa pamoja na kuoa mke mwingine alikuwa akiishi na hao watoto wake aliozaa na huyo mama wa kwanza. Lakini hivi karibuni amegundua kuwa kuwa huyu mke wake ana uhusiano wa kimapenzi na mtoto wake wa kiume alliyemzaa kwa mama wa kwanza.

  Jamani, ni story ambayo sikuitarajia so nikawa namhoji sana huyu bwana angalau anithibitishie nini kilichomfanya amini hivyo. anachoniambia ni kuwa aliwahi kutonywa na jirani yake kuhusu nyendo za mke wake na kijana kuwa waliwahi kukutwa kwenye bar moja wakiwa chakali na mikao yenye mashaka. Pili jamaa alikuta ujumbe kwenye simu ya mkewe kutoka kwa huyo kijana (kumbuka jamaa anaifahamu namba ya kijana wake) ingawa mama ame-save kama "My baby boy". Ujumbe ulisomeka hivi " mummy i miss you so much maisha hapa chuoni ni ya upweke sana...hebu fanya mpango uje angalau nipumzike maana huwa nafurahia sana mapigo yako...I love u'" alipombana mkewe kuhusu huu ujumbe mke alilia sana na kudai kuwa huenda aliyeandika huo ujumbe alitumia simu ya huyo kijana na pia akatuma katika namba ya huyo mama kwa makosa. Jamaa anasema alimpigia simu kijana wake na kumuuliza kuhusu huo ujumbe kijana baada ya mkwara mwingi na vitisho vya kuacha kumlipia ada ya chuo kama hatosema ukweli...kijana alikiri kweli kuwa ameshatembea na huyo mama mara kadhaa tangu xmas mwaka jana. pia huyo mama alikuwa na safari ya kuja Dar (huyo mama wazazi wake wako hapa Dar) so huja Dar mara kwa mara kama kunakuwa na matatizo ya kifamilia na inasemekana kuwa week end ya wiki hii alikuwa na mpango wa kuja hapa mjini.

  Jamaa amenielza kuwa yuko njiani kuja Dar ingawa hakunielez kwa uwazi kuwa ujio wake una madhumuni gani..Kuja kwa wakwe zake? au anamfata kijana wake. kwa kuwa ni rafiki yangu sana na mara nyingi anapokuja hapa mjini hufikia nyumbani kwangu nategemea kuzungumza naye zaidi juu ya hili suala lakini jamani mtoto wa kiume kafanya hayo aliyofanya.Jamaa ameniuliza swali kuwa kama ningekuwa ni mimi kwenye hali kama hiyo ningechukua uamuzi gani kwa kweli sikuwa na jibu la haraka maana nilihofia ushauri mwingine unaweza kumu-influence mtu kufanya jambo la hatari...Jamani hebu tushauriane huenda nitapata clue ya nini cha kumshauri jamaa yangu...
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  this must be serious!
  ANYWAY
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Geoff unajua nilipokuwa naongea na jamaa nilikuwa natetemeka sasa sijui ni woga au hasira...ila mh!!!
   
 4. Mwananzuoni

  Mwananzuoni JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 288
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Tulia kwanza, kwa vile issue umeisikia leo, baada ya siku kadhaa utakuwa umepata muda wa kutafakari ushauri kutoka kwa may be wana JF au sehemu nyingine kabla ya kushauriana na huyo bwana.

  Kijana anaonekana hatari sana huyo, hata dadaye inawezekana alishamptia!.

  Duuuh
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  who is to blame?....(IF I MAY ASK)
   
 6. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyo mtoto atalaaniwa, unakumbuka Reubeni mtoto wa Yakobo alishawahi kuala na mke wa babayake, na hakubarikiwa kabisa kati ya watoto kumi na wawili wa israel. maumbile yake na maumbile ya baba yake yaliingia sehemu moja, ni uchafu uliopindukia. pole kwa kijana, atalaaniwa, hawezi kukipanda kitanda cha baba yake akawa sawa.

  kwa huyo mwanamke, kama ananisikia humu, aombe Mungu amsameha haraka, aokoke (hata huyo kijana), aachane na uchafu huu. kama hatafanya hivyo, balaa nyingi sana zitamfuata, na atavuna matunda ya hayo anayopanda. kama hakuwa na aibu ya kuvua nguo mbele ya mtoto damu ya mume wake, akamuonyesha maumbo yake sawa na anavyomwonyeshaga mume wake, basi huyo hana hata chembe ya aibu, na hivyo ni mtu hatari sana, anawezafanya lolote. ni kitu cha ajabu hakika.
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ...na huyo mama?
  Alibakwa?
   
 8. JS

  JS JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Damn this is serious........lol
  sasa ni kwamba walikuwa hawajuani in the first place kwamba huyu mama ni mke wa baba au inakuaje mpaka wakaanza huo mchezo mchafu????? hebu nijuze hapo kwanza Laligeni.
   
 9. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nadhani hakuna ndoa hapo... divorce is the only solution... my heart with the huband/father may God give him strength to forgive them and go ahead with his life...
   
 10. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mzee inabidi amwachie dogo mke. Hakuna jinsi. Piga ua galagaza hao wawili (mama na mtoto) hawataachana! Kama wamethubutu kuonjana si rahisi kuachishwa utamu na mtu mwingine, labda wenyewe wakosane. Kwa usalama wake jamaa ili asife kwa presha na magonjwa ya moyo yafaa awe mpole, ampishe dogo. Ampe mkewe talaka; na bahati wamefunga ndoa kiserikali. Ni rahisi kutoka kwenye wed-lock. Hii ndiyo shida ya kuwa na watoto wakubwa wa kiume halafu baba unaoa mke mwingine kijana wa umri wao. Unategemea nini!? Wazee oeni wazee wenzenu!
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Huyu mama Mchafu jamani sijawahi kusikia unakula kuku na mayai yake mungu Msamehe mama huyu na amuonyeshe njia ya haki ..
  Kijana nae sijui kama akili yake iko salama ...Mungu hebu njoo unusuru hiki kizazi
  tunafanya mambo makubwa na mazito bila kukuogopa wewe
  MMH ..very bad
   
 12. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  whats so funny about this:confused:
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Incest!
  wameshanogewa kuvunja mwiko, hakuna ushauri hapo ila akubaliane na hali iliyopo, au aachane na mkewe.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kuwa makini na rafiki yako asijekuwa na hasira akafanya jambo baya kwa mwanae na mkewe ..Pls kaa nae chini na uongee nae kwa utaratibu ili ajue ni maamuzi gani ya kuchukua baada ya hili
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,368
  Likes Received: 22,231
  Trophy Points: 280
  Dhambi hurithi kizazi hata kizazi.
  Aangalie kwenye ukoo wao, kuna dhambi ya namna hiyo ilishawahi fanyika....
  Wakemee na wavunje laana.
   
 16. JS

  JS JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Did i mention or expressed anywhere that this is funny Noname????
   
 17. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Opps u did not? what did u mean by lol? ... anyway forget it... sorry my bad
   
 18. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyo mtoto ni damu yake milele so hawezi tengana nae. Kama huyo mwanamke ameweza kucheat kwa mtoto wa mumewe, vp akijazwa ujinga na wengine wa mbali kabisa wasiojumjua mumewe wala kujulikana nae? Hapo ni maamuzi ya kutafuna jongoo. Yaani naiona divorce nje nje.
   
 19. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..JS sio kwamba walikuwa hawajuani kuwa huyu ni mke wa baba na huyu ni mtoto wa mume...Unajua mpaka muda huu bado inaniumiza kichwa lakini kinachonijia akili nadhani yule mama alichukua muda kujenga mazingira ya kumnasa kijana. kama umesoma vizuri hiyo story mara ya kwanza walionekana bar wakiwa mtungi....sasa sijui kama kuanzia hapo mama ndio akafunua au vipi. Lakini nami nawaza kitu kingine tofauti kuhusu jamaa sijui kuwa anamtosheleza mama vizuri au sijui ndio hayo mambo ya safari kila siku mama kaona kuliko kudoea kwa jirani atafune kilicho karibu...yaaani nina maswali mia kidogo...Duh!!
   
 20. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Du! ni vugumu kuwa na ushauri wa haraka na utakaoaminika kuwa wa busara zaidi. Lakini, ningeomba wewe ujaribu yafuatayo kwa usalama wa familia hiyo.

  1. Uwelewe tu kwamba mama bado hajakiri kosa, na huwa ni vigumu kumsamehe asiyekiri kosa. Hivyo, apewe talaka kama matunda ya alichokipanda.

  2. Jaribu kukaa na kila mmoja (baba, mama na kijana) kwa wakati wake ukimsoma na kumdadisi kuhusu hili. Utapata ukweli na utaweza kutoa ushauri wa kufaa.

  3. Jaribu kumweka mzee huyo katika hali ya "FREE OF MIND", na ajisikie huru kufanya uamuzi wowote bila kusambaratisha familia yake.

  4. Ikiwezekana mfiche huyo mzee kwa muda asikutane na mmoja wa hao maagent wa ibilisi, ili aweze kujirefresh mind.

  5. Please, what's matter is PEACE OF MIND, kama hana mtoto na huyo mama basi ampishe kijana wake kwa moyo mweupe na awaachie wakaanze maisha yao tu mbali kidogo.

  6. Hata wewe mwenyewe jaribu kutulia kwanza uone kama mzee anakuja juu kwa kiasi gani na yuko tayari kutoa uamuzi upi badala ya upi.
   
Loading...