Msaada jamani kijana anachezea uwanja wa baba!

Msaada jamani kijana anachezea uwanja wa baba!

Imenisikitisha sana lakini ndio maisha haya na ndio watoto wa kizazi cha . com hao. Ushauri wangu ni huu we mwambie rafikio kuwa hayo ndio maisha na ajikaze kama mtoto wa kiume, namaamuzi afanye ya busara, kumuacha mke wa sasa je ataacha wangapi? na wa mwanzo alimuacha hatimaye yametokea haya! Na kutomlipia mtoto ada eti kwakuwa amekula chakula cha baba, hii sasa itakuwa ni kumkatili kijana, yeye akae nae na waongee baba na mtoto, wote wanaume hao hakuna aibu hapo watamaliza tuu, wanaume kwa wanaume huwa hawana beef za muda mrefu, hasa ikizingatiwa mtoto na baba! Msisitize mwenzio maamuzi ya busara na sio maamuzi ya hasira!
 
Ingekuwa ni mimi ndiyo nimeombwa ushauri huo ningemwambia in Black and White kuwa afuatilie kwa undani na kama akigundua kuwa mambo hayo ni ya kweli basi afanye taratibu za talaka na kumfungulia kesi ya jinai.
 
Ingekuwa ni mimi ndiyo nimeombwa ushauri huo ningemwambia in Black and White kuwa afuatilie kwa undani na kama akigundua kuwa mambo hayo ni ya kweli basi afanye taratibu za talaka na kumfungulia kesi ya jinai.

hizo kesi zinakuwaga ngumu kweli mara nyingi mashahidi huwa wanabadilika (wanakana ushahidi wao wa mwanzo) hivi hizi kesi mkubwa zianitwaje tena??
 
huenda mama mwenyewe ALITAKA😀😀

Huyo mama ni malaya wa mchana! Baba amsamehe mwanae, ila huyo mama aachane naye! Lazima huyo mama alimwekea vijimitego vya kimapenzi huyo kijana zikiwemo pombe mpaka dogo akajikuta kaingia mtegoni!
 
Ingekuwa ni mimi ndiyo nimeombwa ushauri huo ningemwambia in Black and White kuwa afuatilie kwa undani na kama akigundua kuwa mambo hayo ni ya kweli basi afanye taratibu za talaka na kumfungulia kesi ya jinai.

Mkuu mkeo kutembea na mtoto wako wa kumzaa ni kosa la jinai ?
 
Mkuu mkeo kutembea na mtoto wako wa kumzaa ni kosa la jinai ?

ni kosa la jinai kabisa na sheria ya adhabu ya makosa y ajinai imeweka hilo wazi....

sema huwa ni tatizo sana kweny eushahidi wa kesi za namna hiyo.......
 
Geoff sio hivyo hata kama unauchu wa namna gani huwezi kutembea na mtoto wa mume wako for GODS sake, khaaaaaa.!!!!

Kwa siku hizi ni rahisi jambo la aina hiyo kutokea hasa ukizingatia kwamba huyo mama na watoto wa mzee wote ni vijana, yaani umri uko sawa, au unakaribiana. Pili, siku hizi kwa kuiga uzungu unakuta vijana wa kiume na mama zao wa kambo hawaweki umbali katika mahusiano. Unakuta wamebanana tu pale nyumbani na hata maongezi hawaogopani wala kuchagua maneno. Kumbe unakuta wanazoeana kupita mipaka. Tatu, suala la mzee wa mtungini (aka pombe/bia). Huyu ndo shetani wa yote. Kama wako vijana, wamezoeana na wanatokea wanakunywa pombe ya kutosha ikawakolea, hawatahitaji wala kutongozana kwani mazingira hayo tu yatawafanya wajikute wanavinyonga. Wazee wenzangu, natoa ushauri: tuoe wa umri wetu, viajana tuwaachie wengine.
Pili huyu mwenye kesi hii nampa pole. Akubali matokeo/ukweli. Hao wawili hawaachani ng'o! Hata washauriweje! Jamaa aamue moja: au anawavumilia na kujifanya haoni au anamwachie mtoto mke, yaani anatoa talaka.
 
Mie nimekwisha acha kushangaa katika jambo lolote,maana ya kushangaza yamekuwa hayahesabiki kwa sasa.
 
Ha ha ha, nimecheka mbavu sina!!! Tatizo mnaacha kuoa wake wanaoendana na umri wako basi unaishia kuoa mke umri sawa au pengine mdogo kuliko kijana wako!!! Halafu pengine anavutia!!! What do you expect?? Reap what you sow!!

Halafu inapendeza zaidi pale mzee mzima anaamua kuoa binti house girl!! Halafu wanabaki wote na house boy!!! tena wa umri wake!!! Maajabu hayo!!! Ndiyo maana baadhi ya family wakifanya DNA matokeo yataleta vita kuu ya 3 ya dunia!!! Lo, ya sodoma na gomora haya!!
 
ha ha ha, nimecheka mbavu sina!!! Tatizo mnaacha kuoa wake wanaoendana na umri wako basi unaishia kuoa mke umri sawa au pengine mdogo kuliko kijana wako!!! Halafu pengine anavutia!!! What do you expect?? Reap what you sow!!

halafu inapendeza zaidi pale mzee mzima anaamua kuoa binti house girl!! Halafu wanabaki wote na house boy!!! Tena wa umri wake!!! Maajabu hayo!!! Ndiyo maana baadhi ya family wakifanya dna matokeo yataleta vita kuu ya 3 ya dunia!!! Lo, ya sodoma na gomora haya!!

mie ndo maana nipo curious kujua umri wa hawa watu 3 wahusika hapo juu....
 
Hii hata uiweke vipi!! Jamaa inabidi aache mke, na masaidie kijana amuache huyo dada... the main reason hapa ni kwamba amekataa.. which means she doesnt regret or even having any remose nor guilty consciousness!!

Hamfai kabisa huyo mama... na huyo kijana ana matatizo makubwa ya akili kwani hata kusimamisha kwa mama yako ni laana ya kufa mtu!! Mama ni mama, as long as umeshampa hiyo heshima either biological au mlezi

DN
 
ni kosa la jinai kabisa na sheria ya adhabu ya makosa y ajinai imeweka hilo wazi....

sema huwa ni tatizo sana kweny eushahidi wa kesi za namna hiyo.......

Kwa hiyo hata mwanaume akitembea na mdogo au dada yake na mkewe ni kosa la jinai?
 
Back
Top Bottom