Msaada jamani kijana anachezea uwanja wa baba!

Wana-JF naweka thread hii baada ya kumaliza kuongea na simu na rafiki yangu kipenzi aliyeko morogoro. Ni kwamba huyu bwana ni mtumishi wa serikali aliwahi kuzaa watoto wawili na mdada mmoja huko nyuma mtoto wa kwanza ni wa kiume kwa sasa ana miaka 24 anasoma IT kwenye chuo kimoja hapa Dar na mtoto wa pili ni msichana yuko kidato cha tano. Huyu bwana baadae alioa mke mwingine kwa ndoa ya serikali (hakumuoa mzazi mwenzie). maisha yao ya ndoa na mkewe kwa ufahamu wangu yalikuwa ya furaha sana na nimekuwa nikiwatembelea huko morogoro kila ninapopata nafasi ya kuwa huko. Leo amenipigia simu alichonieleza kimenistua sana na bado siamini ingawa yeye amenithibitishia kuwa hilo jambo limefanyika. Ni kuwa pamoja na kuoa mke mwingine alikuwa akiishi na hao watoto wake aliozaa na huyo mama wa kwanza. Lakini hivi karibuni amegundua kuwa kuwa huyu mke wake ana uhusiano wa kimapenzi na mtoto wake wa kiume alliyemzaa kwa mama wa kwanza.

Jamani, ni story ambayo sikuitarajia so nikawa namhoji sana huyu bwana angalau anithibitishie nini kilichomfanya amini hivyo. anachoniambia ni kuwa aliwahi kutonywa na jirani yake kuhusu nyendo za mke wake na kijana kuwa waliwahi kukutwa kwenye bar moja wakiwa chakali na mikao yenye mashaka. Pili jamaa alikuta ujumbe kwenye simu ya mkewe kutoka kwa huyo kijana (kumbuka jamaa anaifahamu namba ya kijana wake) ingawa mama ame-save kama "My baby boy". Ujumbe ulisomeka hivi " mummy i miss you so much maisha hapa chuoni ni ya upweke sana...hebu fanya mpango uje angalau nipumzike maana huwa nafurahia sana mapigo yako...I love u'" alipombana mkewe kuhusu huu ujumbe mke alilia sana na kudai kuwa huenda aliyeandika huo ujumbe alitumia simu ya huyo kijana na pia akatuma katika namba ya huyo mama kwa makosa. Jamaa anasema alimpigia simu kijana wake na kumuuliza kuhusu huo ujumbe kijana baada ya mkwara mwingi na vitisho vya kuacha kumlipia ada ya chuo kama hatosema ukweli...kijana alikiri kweli kuwa ameshatembea na huyo mama mara kadhaa tangu xmas mwaka jana. pia huyo mama alikuwa na safari ya kuja Dar (huyo mama wazazi wake wako hapa Dar) so huja Dar mara kwa mara kama kunakuwa na matatizo ya kifamilia na inasemekana kuwa week end ya wiki hii alikuwa na mpango wa kuja hapa mjini.

Jamaa amenielza kuwa yuko njiani kuja Dar ingawa hakunielez kwa uwazi kuwa ujio wake una madhumuni gani..Kuja kwa wakwe zake? au anamfata kijana wake. kwa kuwa ni rafiki yangu sana na mara nyingi anapokuja hapa mjini hufikia nyumbani kwangu nategemea kuzungumza naye zaidi juu ya hili suala lakini jamani mtoto wa kiume kafanya hayo aliyofanya.Jamaa ameniuliza swali kuwa kama ningekuwa ni mimi kwenye hali kama hiyo ningechukua uamuzi gani kwa kweli sikuwa na jibu la haraka maana nilihofia ushauri mwingine unaweza kumu-influence mtu kufanya jambo la hatari...Jamani hebu tushauriane huenda nitapata clue ya nini cha kumshauri jamaa yangu...

kuna mahali nilishuhudia kisa kama hiki ila ni kinyume chake..kwamba baba ndo anagonga binti wa kufikia..........sasa hapo kwa kipimo cha maumivu ni yupi anaumia zaidi? ......baba kugongewa mkeo na mwanao? Au mama kuibiwa mume na binti yako?:shut-mouth:
 
Back
Top Bottom