ok, kwa kuanzia, acha matumizi ya sabuni za kemikali na mafuta, paka ya kawaida.
Maji ya kuoga uwe unachemsha kwanza yawe vuguvugu.
kama vinawasha sana, tafuta vidonge kwa prednisolone kunywa 20mg mara moja kwa siku kwa siku 3, kisha punguza dozi mpaka 15mg mara moja kwa siku kwa siku 2, kisha 10mg mara moja kwa siku kwa siku 2 tena. sehemu nyingi kidonge kimoja kina 5mg sasa hapo utatumia hesabu tu.
wakati huu huo tafuta calamine lotion uwe unapaka kama mafuta kwenye ngozi.
kama unahisi na kahoma homa, ungeza amoxycillin dozi ya siku 5, ila kama hakuna homa hata kidogo hiyo acha.
usipende kukaa kwenye joto sana, kama ni usiku unalala vaa kinguo chepesi tu(hapa simaanishi usijikinge na baridi kama ipo), pia kuoga angalau mara 2 mpaka 4 kwa siku, yani mwili usikae na jasho mda mrefu.
.......................
Swali, hivyo vipele ukivitoboa vinatoa maji, usaha au damu?